Habari kuhusu Indonesia

Hotuba ya Ushindi ya Rais Mteule wa Indonesia

  29 Julai 2014

Rais mteule wa Indonesia Joko Widodo or Jokowi alitoa hotuba ya ushindi akitambua moyo wa kujitolea ulioonyeshwa na wananchi: Uchaguzi huu wa rais umechochea mtazamo mpya chanya kwetu, na kwa taifa letu kwa ujumla. Uhuru wa watu na uwajibikaji wa kisiasa vinashamiri katika nyoyo za kizazi kipya. Moyo wa kujitolea...

Msongamano Gerezani Nchini Indonesia

  2 Novemba 2013

Leopold Sudaryono anakabiliana na tatizo la msongamano wa magereza nchini Indonesia. Mwaka wa 2011, kulikuwa na wafungwa 144,000 kwenye nchi. Magereza yaliripotiwa kuwa na msongamano mkubwa na asilimia 45 kwa wastani. Miongoni mwa mambo yanayochangia tatizo ni ukosefu wa chaguzi za adhabu mbadala katika kesi na ucheleweshaji katika utawala wa...

Hali ya Uislamu Katika Asia ya Kusini

  27 Julai 2013

Murray Hunter wa Chuo Kikuu cha Malaysia Perlis anajadili hali ya jamii ya Kiislamu katika Asia ya Kusini pamoja na masuala yanayohusiana na kukua kwa Uislamu katika eneo hilo. Umaskini, kujua kusoma na kuandika, elimu, kuhamishwa, ukabaila, ukosefu wa ajira, ukandamizaji, na udhibiti ni mambo yanayowaonea Waislamu ndani ya ASEAN. Serikali pamoja na...

Athari za Mazingira kwa Uchimbaji Madini Nchini Indonesia

  13 Juni 2013

Makala iliyochapishwa katika mtandao wa mongabay.com imefichua athari za uharibifu wa kimazingira ziazotokana na shughuli za uchimbaji madini katika maeneo ya vijiji nchini Indonesia. Baadhi ya wanazuoni wanahofia kwamba maeneo mengi nchini Indonesia yana kiwango cha juu kabisa cha zebaki duniani.

Asia ya Kusini Mashariki : Ngono na Udhibiti wa Mtandao

  26 Julai 2010

Uratibu wa maudhui katika intaneti unaonekana kana kwamba ni kinyume na demokrasia lakini serikali za Kusini Mashariki mwa Asia zinaweza kuhalalisha kitendo hicho kwa kuzusha haja ya kuwaokoa vijana kutoka kwenye janga la tabia za ngono holela.