Podikasti ya Je, unasikiliza? inaangazia baadhi ya habari zilizoandaliwa na chumba cha habari cha Global Voices. Katika toleo hili, tunaangazia suala la utamaduni wa kahawa nchini Jamaika; a matembezi ya kihistoria katika nchi kubwa ya Kiislam duniani; na hali ya kufungwa gerezani na ISI na wakati huo kupata fursa ya kuishi kwa ajili ya kusimulia. Pia tunakujuza kuhusu Mwimbaji maarufu wa Makedonia asiyefahamika na mwisho, tunakurudisha nyuma miaka mia moja kwenye harakati za Ethiopia za kukabiliana na ukoloni wa wazungu. Katika toleo hili, Kilicho cha zamani ni kipya.
Shukrani za pekee zimwendee Kat Batuigas kwa kutuwezesha kuandaa toleo hili na wachangiaji wa Global Voices Emma Lewis na Endalk kwa kutusaidia kwenye upande wa masimulizi pamoja na kuripoti — sambamba na Filip Stojanovski, Juke Carolina, Joey Ayoub, na Elias Abou Jaoude — habari tulizosheheni katika matangazo haya ya sauti.
Katika kipindi hiki, tunasindikizwa na muziki wenye haki miliki ya Creative Commons kutoka maktaba ya Free Music, ikiwa ni pamoja na Please, listen carefully by Jahzaar; Good Riddance by Ars Sonor; Flute Fleet by Podington Bear; Vintage Frames by Kai Engel; Backward by David Szesztay; na Modulation of the Spirit by Little Glass Men.
Picha inayopamba habari hii ni ya “Ngazi za Kanisa” iliyopigwa mbele ya Kanisa la Mt. Mary wa Kiyahudi huko Axum, Ethiopia. Picha kwa hisani ya mtumiaji wa Flickr A.Davey (CC BY 2.0).
Podcast: Play in new window | Download