Vumbi la Uchafuzi wa Mazingira Larudi Nchini Indonesia

Haze in Sumatra. Photo by @jgblogs

Vumbi mjini Sumatra. Picha ya @jgblogs

Karibu matukio 500 ya moto wa msituni yalirekodiwa katika kisiwa cha Sumatra mwezi Agosti matukio ambayo yalisababisha vumbi nene kutimka angani Riau nchini Indonesia na hata katika baadhi ya maeneo ya Malaysia. Uchomaji wa misitu ni unasemekana kusababishwa na shughuli za kilimo cha mashamba makubwa ya mafuta ya mawese, makubaliano ya uuzaji wa kuni, na mashamba ya mashapo. Shule kadhaa zilifungwa katika jimbo la Riau wakati wa vumbi hilo baya lilipoonekana tena wiki iliyopita.

Vumbi linalosababishwa na uchafuzi wa mazingira ni tatizo la mara kwa mara katika eneo hilo linalosababishwa zaidi na matukio ya moto wa msituni nchini Indonesia. Mwezi Juni, vumbi nene kiliifunika Singapore na maeneo mengi nchini Malaysia.

Forest fire hotspots in Riau, Indonesia. Image from Eyes on the Forest.

Maeneo yanayoonesha matukio ya moto wa msituni jimboni Riau, Indonesia. Maeneo yenye rangi ya manjano  ni mashamba makubwa ya mawese.  Picha ya Eyes on the Forest [Macho Misituni].

Kwenye mtandao wa Twita, Wa-Indonesia walionyesha wasiwasi wao juu ya kurejea tena kwa vumbi hilo huko Sumatra.

Kama Rais wa Indonesia [anayefahamika kwa kifupi kama SBY, Susilo Bambang Yudhoyono, waambieni wamiliki wa mashamba ya mawese wachome moto zaidi ili [Rais SBY] aone kwa macho yake vumbi hili linafananaje

Ardhi inateketea vibaya kwa moto kwa siku mbili huko Medan, imeacha vumbi jeusi kwenye pikipiki yangu kwa masaa nane tu

Huko Penang, vumbi hilo liliathiri wakazi wengi. Kwa bahati nzuri, vumbi lilikuwa tayari kimekwisha mwishoni mwa wiki iliyopita.

Vumbi hili linanizuia kufanya mazoezi ya kukimbia kimbia

Hatimaye, hakuna vumbi zaidi. Safi. Hatimaye naweza kuona mawio ya jua. Alhamdulillah. Asubuhi njema

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.