Indonesia: Maandamano ya Kupinga Bei ya Mafuta Yatikisha Majiji

Miji kadhaa nchini Indonesia ilitikiswa na maandamano yenye lengo la kupinga ongezeko la bei ya mafuta katika wiki chache zilizopita. Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya nchini humo kuna ripoti kwamba [id], baadhi ya maandamano hayo yaligubikwa na vurugu zilizosabisha watu kujeruhiwa.

Mwanzoni, serikali ya Indonesia ilikuwa na mpango wa kuongeza bei ya mafuta (petroli) kuanzia tarehe 1 Aprili. Hakukuwa na tamko rasmi kuhusu marekebisho ya bei ya mafuta. Kwa sasa, mafuta yanayopatiwa ruzuku ambayo katika nchi hiyo hujulikana kama Premium huuzwa kwa kiasi cha IDR 4,500 (sawa na dola 0.50 au shilingi 800) kwa lita. Bila kuwa na ruzuku hiyo, Premium huuzwa kwa kiasi cha IDR 8,400 (dola 0.92/shilingi 1,450) kwa lita.

Protesters near Parliament Building. Photo from Flickr page of Djembar Lembasono used under CC License

Waandamanaji wakiwa karibu na Jengo la Bunge. Picha kutoka ukurasa wa Flickr wa Djembar Lembasono na imetumika chini ya leseni ya CC

Mwandishi wa habari na mpiga picha za video Gianrigo Marletta, anayeishi jijini Jakarta alipandisha picha hii ya video kwenye YouTube.

Maandamano yaliyofanyika mwezi uliopita na uwepo wa askari jeshi kwa wingi [id] ili kuzuia vurugu kwenye maandamano, jambo linaloleta kumbukumbu za vurugu zilizopata kutokea katika taifa hili kuhusiana na suala la mafuta. Mwaka 1998, nchi iliingia kwenye machafuko baada ya mpango wa serikali wa kuongeza bei ya mafuta. Maduka yanayomilikiwa na raia wa Indonesia wenye asili ya Uchina yalichomwa moto na watu wenye hasira, baadhi ya wanawake walibakwa, waandamanaji wanafunzi walitekwa nyara na kuuwawa kwa risasi, na mwishoni, rais aliyetawala Indonesia kwa miaka mingi zaidi, Suharto alilazimika kujiuzulu.

Katika mtiririko wake wa matukio kwa kufuata mpangilio wa muda, mtumiaji wa Twita @cuapolitik alisema kwamba wakati umefika wa kuongeza bei ya mafuta. Anajenga hoja kwamba:

3. Jk BBM tak naik, subsidi untuk solar premium th 2012 ini bs melonjak dari Rp123,6 T menjadi Rp191,1 T. #BBM
4. Pdhl, subsidi itu akan lbh brmanfaat kl dipake utk infrastruktur atau tuk peningkatan pendidikan n ksehatan. Lbh terasa utk rakyat. #BBM
5. Msyrakat yg krang mampu akan menikmati manfaat jk BBM subsidi naik. Sebab, msyrkat kurang mampu bukan konsumen BBM yang terbesar. #BBM
6. Harga jual bbm subsidi yg terlalu rendah dibanding di LN mendorong penyelundupan penyelewengan. Yg untung ya para penyelundup. #BBM
7. Krn subsidi, harga jual bbm subsidi di dlm negeri jauh lebih murah daripada harga barang yang serupa di negara2 tetangga. #BBM
8. Itu sebabnya, para penyelundup justru menikmati perbedaan harga ini, hingga merugikan keuangan negara dan kita semua #BBM
11. Slama ini org2 bilang pmrntah hanya ambil kbjakan menaikkan #BBM subsidi. Salah. Ada kbjakan lain utk atasi defisit. #BBM
17. Kbjakan subsidi ini adlh kbjakan dr masa lampau. Dl bs subsidi, krn kt eksportir. Tp skrg kt importir, n sdh keluar dr OPEC #BBM
18. Slain itu, dl knsumsi BBM kt rendah, jauh brbeda dgn skrg. Karenanya kbjakan subsidi hrs diubah perlahan. #BBM

Kama tusipoongeza bei ya mafuta, ruzuku kwa ajili ya mafuta ya dizeli na premium katika mwaka 2012 itapanda kutoka kiasi cha IDR 123.6T hadi IDR 191.1T.
Kwa kusema kweli, ingefaa ruzuku (kwenye bajeti) zielekezwe kwenye miundombinu, elimu, na kuboresha afya. Watu watanufaika zaidi kwa njia hiyo.
Watu wa hali ya chini watanufaika zaidi kutokana na ongezeko la bei, kwa sababu wao ndiyo walaji wakubwa wa bidhaa za mafuta.
Bei ya mafuta yenye ruzuku iko chini mno ikilinganishwa na bei katika nchi nyingine, jambo hili husababisha biashara haramu na matumizi yasiyofaa. Walanguzi katika jambo hili ndiyo wanaonufaika hapa.
Kwa sababu mafuta yanapata ruzuku hapa, bei hapa nchini iko chini sana kwa kulinganisha na nchi jirani.
Kwa hiyo, walanguzi wananufaika sana na tofauti hii kubwa ya bei, kwa hiyo wanaishia kuumiza uchumi wetu na sisi sote.
Wakati wote huu, watu wanadai kwamba serikali ilitunga sera ili kuongeza bei ya mafuta. Hiyo si sahihi, ni sera yenye lengo la kudhibiti nakisi.
Ruzuku kwenye mafuta ni sera iliyopitwa na wakati. Wakati ule tuliweza kuwa na ruzuku kwa sababu tulikuwa ni taifa linalosafirisha (mafuta) kwenda nje. Hivi sasa sisi ni taifa linaloagiza mafuta kutoka nje, sisi siyo tena wanachama wa OPEC (Umoja wa Nchi zinazozalisha Mafuta Duniani).
Zaidi ya hayo, zamani zile tulikuwa na matumizi ya chini ya mafuta, ambapo hivi sasa hali iko tofauti kabisa. Kwa hiyo, sera ya ruzuku kwenye mafuta haina budi kubadilika taratibu.

Mwanablogu Sony Haryo Prabowo aliandika makala kwenya blogu yake blog, akisema kwamba waandamanaji kwenye miji ya Makassar, Sulawesi wamewalenga visivyo wauzaji rejareja wa mafuta:

sekian banyak SPBU di Indonesia, Pertamina hanya memiliki 74 di antaranya (sumber: Pertamina Retail). Ribuan lainnya dimiliki oleh dealer (swasta).  Dengan demikian, perbuatan para pendemo yang merusak SPBU telah membuat hilangnya lahan mencari nafkah bagi seorang wiraswasta, bahkan mereka juga menghilangkan lapangan kerja andai SPBU tersebut benar-benar berhenti beroperasi.

Kutoka kwenye vituo mbalimbali vya mafuta nchini Indonesia (kwa kuzuia jina lake), Pertamina inamiliki vituo 74 tu (chanzo: Pertamina kitengo cha rejareja). Vituo vingine kwa idadi ya maelfu vinamilikiwa na watu binafsi. Kwa hiyo, kile wanachofanya waandamanaji, yaani kuharibu vituo vya mafuta, sanasana ni kuwakosesha tu wamiliki hao binafsi mapato yao ya kila siku, na vilevile kupoteza kazi za walioajiriwa hapo hasa kama vituo hivyo vitaacha kuendelea kufanya biashara.

Sony alihitimisha kwa kusema:

Demo yang mereka lakukan juga menutup jalan, merusak kendaraan pribadi, bahkan kendaraan pengangkut minuman ringan ternama yang mungkin seringkali mereka minum. Saya ingin mengajak para pembaca berdiskusi dan merenung. Dalam demokrasi, demonstrasi memang boleh dilakukan, bahkan harus. Namun, harus selalu diingat bahwa demonstrasi harus dilakukan dengan dasar yang benar dan dengan akal sehat. Demonstrasi yang terjadi di Makasar ini membuktikan ada sebagian mahasiswa di Indonesia ini tidak menggunakan akal sehat dalam berpikir. Mereka hanya ingin melampiaskan apa yang mereka inginkantanpa berpikir apa kerugian yang mereka sebabkan. Bahkan lucunya lagi mereka melakukan demo seakan-akan tahu masalah yang mereka hadapi.

Waandamanaji pia walizuia mitaa, walivamia magari binafsi, na hata mahali fulani waliteka nyara lori la kusambaza vinywaji baridi. Ninawaalika wasomaji kujadili na kutafakari. Katika demokrasia, maandamano yanaweza kufanyika. Hata hivyo, ni lazima tuanzishe maandamano hayo kwa sababu za msingi na kuelewa vema kile tunachokipigania. Maandamano yaliyofanyika katika jiji la Makassar yanathibitisha kwamba baadhi ya wanafunzi hawatumii hata ule uelewa wa msingi. Wanafanya tu yale wanayofanya bila kutafakari hasara wanazoweza kusababisha. Lililo la kuchekesha zaidi ni kwamba wanaelekea kuandamana pasipo kuelewa kwa dhati nini hasa kinachowafanya waandamane.

Watumiaji wa Twita wameongeza ukubwa wa wavuti wa blogu ndogondogo ili kutoa ripoti kuhusu mapigano yaliyoibuka kati ya polisi na wanafunzi jijini Jakarta. Vilevile walijadiliana endapo ongezeko la bei lilikuwa jambo sahihi.

@ikovoz: Issue korban meninggal di bentrok salemba itu hoax. skg di RSCM 3 org mahasiswa dan 1 satpam yg msh dirawat

@ikovoz: Uvumi kuwa kuna mtu aliuwawa wakati wa mapambano yaliyotokea Salemba ulikuwa uwongo mtupu. Hivi sasa wanafunzi watatu na mlinzi mmoja wanapatiwa matibabu huko RSCM  (Cipto Mangunkusumo Hospital).

@LBH_Jakarta: Polisi melakukan sweaping ke LBH,47 ditangkap paksa.6 ditangkap di samping LBH.Total 52 org dibawa paksa ke Polda.

@LBH_Jakarta: Polisi walikuwa wakifanya kamatakamata katika Taasisi ya Msaada wa Kisheria(LBH), wanafunzi 47 wametiwa mbaroni. Sita walikamatwa karibu na Ofisi za LBH. Jumla ya wanafunzi 52 walipelekwa kituo kikuu cha wilaya cha polisi.

@komar_hidayat: Terlepas harga BBM naik atau tdk, apakah ada tanda2 nasib rakyat akan membaik?Terbuka lapangan kerja baru?

@komar_hidayat: Licha ya kuongezeka kwa bei ya mafuta ya petroli, je, kuna kiashiria chochote kuonyesha kwamba maisha ya watu yanakuwa bora zaidi? Je, kuna kazi zaidi zinapatikana?

@BankDunia: 40% penerima manfaat langsung subsidi #BBM bagi rumahtangga adalah 10% rumahtangga terkaya

@BankDunia: Asilimia 40 ya wale wanaonufaika na mpango wa ruzuku ni kaya, kati ya hizo, asilimia 10 ni zile zenye hali bora ya kimaisha.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.