Asia ya Kusini Mashariki : Ngono na Udhibiti wa Mtandao

Kuratibu vilivyopo kwenye mtandao siku hizi inaonekana kama ni kitendo kinachopinga demokrasia lakini serikali za Kusini Mashariki mwa Asia zinaonekana kuweza kuhalalisha vitendo hivyo kwa kudai kuwa vinatokana na haja ya kuwaepusha vijana na majanga ya tabia za ngono za hovyo hovyo.

Mpango wa Indonesia wa kuuchuja mtandao wa intaneti na mambo yote “mabaya” kwa kutumia timu maalumu ya kuchuja media-anuai uliwekwa pembeni mwezi wa pili mwaka huu baada ya kupingwa vikali na wananchi. Leo, pendekezo hilo limeamshwa upya kutokana na kuwepo kwa mkanda wa kutia aibu wa ngono wa mtu maarufu ambao unaendelea kuwastua wote watoto na watu wazima katika nchi yenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu duniani. Baada ya kurasimisha sheria ya kupinga picha za ngono miaka miwili iliyopita, Indonesia sasa inataka kuanzisha orodha ya visivyotakiwa mtandaoni kama namna ya kuitikia haja ya makundi ya kihafidhina ya kulinda maadili ya vijana.

Mkasa wa kutia aibu wa ngono wa watu wanaojulikana sanawa namna hiyo uliibabatiza sana nchi ya Ufilipinomwaka jana ambao ulifagia njia ya kuanzishwa kwa sheria inayozuia kuangalia mambo ya nguoni. Mtandao wa intaneti pia ulilaumiwa kwa kusambaza papo kwa papo kanda za hizo za ngono na hivyo watunga sheria kuamua kupitisha mswaada wa makaosa ya kimtandao.

Huko Kambodia, serikali inapendekeza kuanzishwa kwa kituo cha taifa cha usambazaji ili kudhibiti watoa huduma za intaneti, kituo hicho kina nia ya kuimarisha usalama wa kwenye mtandao dhidi ya picha za ngono, wizi pamoja na uhalifu mwingine wa kwenye mtandao. Rasimu ya sheria hiyo bado haijakamilika lakini inategemewa kuwa serikali itafuatilia hatua hii kwa makini hasa baada ya kukaribia kushindwa kuzuia upakiaji holela kwenye simu za viganjani na kwenye intaneti wa wa picha za uchi za wanawake waliokuwa wakioga hekaluni zilizopigwa kinyume cha sheria .

Kusini mashariki mwa Asia serikali hazihitaji kutokee shutuma za ngono ndipo ianze kuchunga mtandao kwani huweza kutumia sababu nyingine yeyote, kama usalama wa taifa, kuchuja na kufuatilia vilivyopo kwenye mtandao. Kwa mfano, Thailand ilikuwa ya kwanza kufungatovuti 100,000 fkutokana na kuwa na mambo “hatari”. Huwaadhibu wanablogu,waandishi na waratibu wa tovuti kwa kukiuka sheria inayoulinda ufalme dhidi ya aibu. Vietnam ilishutumiwa na Google na McAfee kwa kufanya mashambulizi ya mtandaoni dhidi ya baadhi ya tovuti, hasa tovuti zinazoandika kuhusu uchimbaji wa madini yanayotengeneza bati, ambao ni mjadala tata nchini humo.

Lakini uratibu wa mtandao unaosukumwa na siasa mara nyingi huwa unakumabana na upinzani mkubwa sana kutoka kwa watumiaji wa mtandao na mara nyingi huamsha lawama nyigi sana kote ulimwenguni, hasa kutoka kwa vyombo vya habari na mashirika ya haki za binadamu. Serikali zinaweza kuwapuuzia wakosoaji wenye kelele nyingi lakini pia zinaweza kupoteza umaarufu. Serikali zenye vifungu vya demokrasia haziwezi kumudu kuwa na ujanja wa kuratibu vinavyokuwepo kwenye mtandao kwa muda mrefu. Lakini kuratibu mtandao ili kuzuia picha za ngono na vitendo vingine visivyo na maadili huamsha lawama chache sana na za chini chini. Imekuwa ni ujanja salama kuzuia tovuti “haribifu”. Myanmar’s Sera ya uratibu wa mtandao ya Myanmar iliyosimikwa na utawala wa kijeshi imetambuliwa kuwa ndio iliyo katili kuliko zote ulimwenguni kwa uamuzi wake wa kuyapiga marufuku majarida mawili ya kila wiki kwa kuchapisha picha za wanawake wanamitindo wakiwa nusu uchi japo hawakupata kukosolewa sana na wanaopenda demokrasia.

Hatua kali za kutaka kuondoa ngono na picha za ngono mtandaoni inaweza kuwa ni dalili ya kuibuka upya kwa uhafidhina katika nchi nyingi za Kusini Mashariki mwa Asia. Karata ya maadili inachezwa ili kurudisha hali inayokubalika, hisia na tabia halali kati ya watu hata kama njia itumikayo haitaheshimu tofauti za mila na desturi kati ya watu wa kanda hiyo. Wakati Indonesia ilipopitisha sheria ya kupinga picha za ngono, Gavana wa Bali aliipinga kwa vile sheria ilikuwa ile ilikuwa kinyume na tamaduni za za eneo hilo ambako kuweka sanamu za uchi zenye kuamsha hisia bado zina nafasi na zinakubalika. Wakati Kambodia ilipozizuia tovuti zinazoonesha picha za ngono, iliijumuishareahu.net kwa kuwa na vielelezo vya kisanii vyawachezaji wa zama wa Apsara walio matiti wazi pamoja na askari wa Khmer Rouge.

Tatizo jingine ni maelezo yasiyoeleweka ya lipi hasa linaloweza kuitwa ni la ki ngono, lisilo la kistaarabu, lisilo la kimaadili, na la nguoni. Wanaharakati wa Kifilipino wana mashaka kuwa muswaada wa uhalifu wa mtandaoni sasa unaweza kufanya kuwa kinyume cha sheria kuchapisha au kupakia maudhui yaliyo kinyume cha tafsiri ya serikali ya vitu vyenye heshima, maadili na sawa.

Serikali zimefuzu nyenzo na mbinu za kuchuja habari kwenye vyombo vya habari vya kitamaduni. Hivi sasa wanaijaribu mipaka ya udhibiti wa kwenye mtandao. Mpango wa Indonesia wa kusimika orodha marufuku ya kwenye intaneti unapaswa ufuatiliwe kutokana na athari zake kwenye eneo hilo. Indonesia ina watumiaji wa intaneti zaidi ya milioni 40 na imetambuliwa kama makao makuu yaTwitter katika Asia. Kama Indonesia itafanikiwa katiaka kuchuja yaliyopo mtandaoni, nchi nyingine katika eneo hili zinatarajiwa kufuata mfano huo.

Kuuchunga mtandao hakuishii tu kuzuia upatikanaji wa taarifa, bali pia hudhoofisha mshikamano wa watumiaji wa intaneti katika mtandao. Ili kuwakinga vijana wasio na hatia, njia rahisi ni kuwapa elimu muafaka wazazi na hao vijana na jamii kwa ujumla kuhusiana na faida na hasara za kuuvinjari mtandao.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.