Habari kuhusu Singapore

‘Mazungumzo ya Kitaifa’ Nchini Singapore Yatafanikiwa?

Katika juhudi za kupangilia mustakabali wa Singapore, serikali imezindua “mazungumzo ya kitaifa” yatakayodumu kwa mwaka mmoja ili kukusanya maoni ya watu. Baadhi ya wananchi wameupokea mpango huo kwa mikono miwili lakini pia wapo wengine wanaoupinga wakiuona kama mbinu tu ya kujiweka karibu na wananchi.

27 Oktoba 2012

Singapore: Maoni ya Waziri Yasababisha Tafrani Mtandaoni

Fahamu kwa nini sentensi hii “Nilipofanya uamuzi…” imezua tafrani mtandaoni nchini Singapore inayotokana na kauli iliyotolewa na waziri mwandamizi wa nchi hiyo. Hiyo ni kufuatia uamuzi wa serikali kupunguza mishahara ya wanasiasa ambao ni kati ya watu wanaolipwa zaidi duniani.

16 Januari 2012

Singapore: Wanablogu Waikosoa Ilani ya PAP

Chama kinachotawala Singapore, People’s Action Party (PAP), kilitoa ilani yake ya uchaguzi tarehe 17 aprili, 2011, ambayo mara moja ilikosolewa na wanablogu wengi kwa “kutokuwa wazi”. PAP tayari kimekuwa madarakani kwa miongo mitano. Uchaguzi mkuu nchini humo umefanyika tarehe 7 Mei.

12 Mei 2011

Udhibiti Nchini Singapore

Singapore imesababisha kelele kubwa baada ya kupiga marufuku filamu ya aliyewahi kuwa mfungwa wa kisiasa na kumkamata mtunzi Mwingereza wa kitabu kilichoandiaka kuhusu adhabu ya kifo nchini humo. Wanablogu wanajadili.

5 Agosti 2010

Singapore: Kampeni ya “Kataa Ubakaji”

Nchini Singapore, mara nyingi kumbaka mke wako hakuchukuliwi kama tendo la kubaka. Waandaji wa kampeni ya “Kataa Ubakaji” wanataka kukomesha sheria inayokinga ubakaji ndani ya ndoa kwa kuzindua kampeni ya kukusanya saini ambazo zitawasilishwa kwa watunga sera. Wengi wa raia wa mtandaoni wanaiunga mkono kampeni hii.

23 Disemba 2009