Mwanaharakati Raia wa Singapore Ahukumiwa Kifungo cha Siku 16 Jela kwa Kuzungumza na Joshua Wong Kiongozi wa Vijana wa HK

Jolovan Wham, kupitia Twitter.

Ujumbe ufuatao uliandikwa na Holmes Chan na kuchapishwa na vyombo vya habari vya Hong Kong tarehe 21 ya mwezi Februari, 2019. Toleo lililohaririwa lilichapishwa tena na Global Voices chini ya maudhui ya mkataba wa ushirikiano.

Jolovan Wham, mwanaharati Msingapore amehukumiwa kifungo cha siku 16 kwenda jela kwa kukataa kulipa faini kwa kosa la kufanya mazungumzo ya wazi na Joshua Wong, mwanaharakati wa kidemokrasia kupitia mtandao wa Skype mwaka 2016. Yupo nje kwa dhamana wakati akisubiri rufaa yake.

Wham ni mwanaharakati anayejulikana kwa kampeni zake za kutetea haki za wafanyakazi wa kigeni, uhuru wa kutoa maoni katika Singapore na mageuzi ya sheria za nchi za kuwekwa kizuizini na hukumu ya kifo.

Mwezi uliopita, Wham alikuwa ameshtakiwa kwa kufanya mkutano haramu kwa kuwa mwenyeji wa jukwaa la Novemba 2016 liliokuwa na mada juu ya “uasi wa raia na harakati za kijamii” ambao ulihudhuriwa na Joshua Wong na wanaharakati wa vyombo vya habari vya ndani. Wham aliambiwa na polisi kwamba anahitaji kuwa na kibali cha kuruhusu Wong kuzungumza, lakini aliendelea bila kuwa nacho.

Tarehe 21 Februari, Wham alipigwa faini na mahakama S $2,000 (sawa na dola za kimarekani 1476) kwa kuandaa mkutano wa wazi bila kibali cha polisi. Pia alipigwa faini ya S $1,200 (sawa na dola za kimarekani 886) kwa kushindwa kutia saini maelezo ya polisi.

Vyombo vya habari vya Singapore vililipoti kwamba Wham alikataa kulipa faini, na mahakama ikamhukumu siku 16 kwenda jela kwa kushindwa kulipa faini. Sambamba na mkutano haramu, pia Wham alishtakiwa kwa kukataa kutia saini maelezo ya ushahidi uliotolewa na polisi. Wakati anakataa kutia saini alisema kuwa hakupewa nakala ya maelezo hayo.

Wham anatarajia kukata rufaa kupinga maamuzi ya Jaji. Ameachiwa kwa dhmana ya S $8,000 (sawa na dola za kimarekani 5,906), hii ni kutokana na ripoti za vyombo vya habari.

Mkutano unaohojiwa uliandaliwa na Mtandao wa Jumuia kwa Vitendo ambao ni shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na uhuru wa kutoa maoni katika mji mkuu wa nchi. Wham alisema kuwa polisi walimwambia ilikuwa ni lazima kupata kibali cha kazi na cha polisi kwa wazungumzaji watakao hudhuria ambao hawatoki Singapore- hata kama watazungumza wakiwa mbali kupitia kiunganishi cha video.

Baada ya tukio, Wham alihojiwa na polisi kwa muda wa dakika 45. Hatimaye alishtakiwa mwezi Novemba 2017, lakini shauri halikuletwa mahakamani hadi Januari 2019.

Joshua Wong aliiambia chombo huru cha Hong Kong (HKFP) kuwa mashtaka ya Wham ni “aibu na ukosefu wa haki wa kutisha,” na anasikitika kwa hukumu hiyo.

Jolovan alinikaribisha kwa ukarimu ili kubadilishana na Jumuia ya Singapore uzoefu nilionao juu ya harakati za kupigania uhuru na haki katika Hong Kong- inashangaza matokeo yake ni kwamba Jolovan amekuwa muhusika wa udharimu.

Ningependa kueleza heshima na pongezi zangu kwa uvumilivu wa Jolovan na matamanio yangu kwa watu wa Singapore ni kuwa siku moja waweze kufurahia uhuru na demokrasia ya kweli.

‘Upindishwaji wa sheria’

Waandishi wa Singapore na mshiriki kutoka Global Voices Kirsten Han ambaye alikuwa pia msemaji kwenye Jukwaa la Wham alilaani na kusema hukumu ni “ya kikatili”.

[Mkutano] haukuwa na madhara yoyote juu ya amani na utulivu wa watu ila ni upotoshaji wa sheria kwa kutangaza kuwa mkutano haramu kwa sababu tu mtu asiye Msingapore alizungumza kwa kiunganishi cha video, hii inaonesha sheria za Singapore zilivyo na namna zinzavyotumiwa kuzuia uhuru wa raia wa Singapore…Asingehukumiwa kama hukumu ingezingatia haki.

Pia, Han alipinga sababu zilizotolewa za kumshtaki. Kutokana na chombo cha habari cha NewsAsia, Mashtaka yalieleza kuwa watu “maelfu” walikuwa wamealikwa na watu 366 walionesha wangehudhuria mkutano huo.

Hata hivyo, Han alisema tukio lile lilihudhuriwa na watu waliozidi kidogo 60 na “lilikuwa la kiwango kizuri”. “Hata ukumbi haukuwa mkubwa” aliongeza.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.