Yaliyojiri Wiki Hii Hapa Global Voices: Kuchezea Amani

Matangazo ya yaliyojiri wiki hii hapa Global Voices yanaangazia baadhi ya habari kubwa zilizojitokeza kwenye habari zetu za Global Voices. Wiki hii, tunaongea na mhariri mshiriki wetu wa zamani wa mradi wa RuNet Echo Tanya Lokot na mhariri mshiriki wa sasa RuNet Echo Isaac Webb kuhusu mapingano yanayoendelea kati ya Ukraine na Urusi na maoni ya raia wa Ukraine kwa hali hii.

Tunakuhabarisha pia habari za watu wa kawaida wanaokabiliana na hali ya kunyimwa haki zao nchini Singapore, India na Brazil. Na, tukirudi Ukraine, tunasikia maoni ya Mkurugenzi Mtendaji wa Global Voices Ivan Sigal kuhusu hali tete ya amani katika mji mmoja usio mbali sana na uwanja wa vita.

Shukrani nyingi kwa Raphael Tsavkko Garcia, RezwanMong Palatino na waandishi, watafsiri na wahariri wetu wote waliwezesha kipindi hiki kufanikiwa.

Katika kipindi hiki, tunasindikizwa na muziki wenye haki miliki ya Creative Commons kutoka maktaba ya Free Music, ikiwa ni pamoja na Please Listen Carefully wa JahzzarIn The Darkness (No Voices) wa VYVCH; Your Pulse wa Little Glass Men; Long White Cloud wa krackatoaGolden wa Little Glass Men; Waking Stars wa Kai Engel; and Lovely, Lonely (Ala ya muziki) wa YEYEY.

Picha inayopamba habari hii ni ya Alice V/Democratize. Imetumiwa kwa ruhusa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.