Ukiwa umeanzishwa mwaka wa 2011, Mradi wa Kumbukumbu za Singapore unalenga “kukusanya, kuhifadhi na kuhakikishia upatikanaji” wa historia ya Singapore. Zaidi ya hayo, “ina lengo la kutengeneza mkusanyiko wa maudhui ya taifa ikiwa ni pamoja na maandiko, kanda za sauti na video kwa ajili ya kuzihifadhi katika mfumo wa kidijitali, na kuzifanya zipatikane kwa ajili ya ugunduzi na utafiti.” Mradi huu unatarajia kukusanya kumbukumbu wa watu binafsi zipatazo milioni 5 ifikapo mwaka 2015.