
Ndege ya Shirika la Ndege la Singapore Machi 29, 2014. Picha na mtumiaji wa mtandao wa Flickr Aero Icarus. CC BY-NC-SA 2.0
Baada ya habari kufahamika kwamba ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH17 imeanguka mashariki mwa Ukraine, Shirika la Ndege la Singapore liliweka ujumbe huu kwenye mtandao wa Facebook na Twita:
Customers may wish to note that Singapore Airlines flights are not using Ukraine airspace.
— Singapore Airlines (@SingaporeAir) July 17, 2014
Wateja wanaweza kuendelea kufahamu kuwa ndege za Shirika la Ndege la Singapore hazitumii anga la Ukraine
Watumiaji wengi wa mtandao walililaumu shirika hilo la ndege kwa kutokuwa na uungwana. Sophie Chang alitoa maoni kwenye mtandao wa Facebook kwamba “namna nzuri kwa shirika la ndege kufanya ni kutoa pole kwanza.” Lakini Stephen Chapman anaamini kwamba kauli hiyo “ilikusudia kuleta utulivu kwa maana pana.” Ryan Ik alikubaliana na ufafanuzi huo lakini alijisikia “kukosa maneno ya kutoa pole, habari hizo hazikuwa za kiungwana.”
Iwe ni kweli ama la kwamba ujumbe huo ulikosa uungwana, lakini tangu uwekwe mtandaoni umekuwa ukisambaa kwa kasi ndani ya masaa machache.