Wanapanda mabasi, treni, na ndege, si tu kwa lengo la kusafiri lakini pia kutengeneza michoro ya wasafiri.
Wachoraji ndani ya vyombo vya Usafiri ni kundi la mtandao wa Facebook lilianzishwa zaidi ya mwaka uliopita kwa ajili ya kuonesha kazi za wasanii wanaotumia vizuri muda wao kwa kuchora kile wanachokiona wanapokuwa kwenye mazingira ya usafiri wa umma. Kundi hili halichapishi tu michoro ya wa-Singapore lakini pia wasanii wa nchi nyingine.
Mchoraji na mwalimu wa Singapore Erwin Lian, mmoja wa waanzilishi wa kundi hilo, anaelezwa kwa nini anafikiri mfumo wa usafiri wa umma ni jukwaa sahihi kwa wasanii:
Ninafikiri mfumo wa usafiri wa umma unatengeneza eneo lenye upekee na utulivu. Unakuwa na sanduku linalosafiri (usafiri wa umma) likiwa na matairi au mabawa yanayoweza kubeba watu wa aina tofauti, kwa sababu kimsingi usafiri huo unawapeleka watu hao eneo linalofanana. Hilo linanivutia; kwamba watu wanakwenda mahali kwa pamoja. Pia, ukweli kuwa kuna nyuso mbalimbali za kuchora ndani ya chumba kidogo hilo tu linanisisimua. Nilifundishwa sanaa ya uchoraji kwa mfumo uliozoeleka, lakini usafiri wa umma unaleta ladha ya kipekee, salama na madhari iliyofungwa pamoja kunisaidia kufanya kile ninachokipenda.
Anaongeza kwamba wazo la Uchoraji ndani ya usafiri wa Umma lilitokana na mradi kama huo unaofanyika nchini Canada:
Nilihamasishwa mno na treni za Canada na kule wana mradi unaoitwa “Kuchora mistari” ambapo wanawakaribisha wachoraji kutuma kazi zao na kazi hizo zibandikwa kwenye treni kwa maonesho. Nilifikiri hiyo ilikuwa ni hatua muhimu kwa ajili ya kuwatangaza wasanii husika.
Alvin Mark Tan, mwanachama mwingine wa kikundi hicho cha wachoraji, anashangazwa kugundua kuwa watu wengi wanakuwa hawana habari ya kile kinachofanyika pale wanapokuwa wamepanda mabasi na treni:
Kwamba watu kwa ujumla wanaweza kuwa wamekodolea simu zao, hawana habari kuwa ninawachora, au hata kutambua kuna kitu kinaendelea pembeni yao.
Alitengeneza kipande kidogo cha video ya maelekezo kwa lengo la kudokeza namna uchoraji huo wa ndani ya vyombo vya usafiri vya umma unavyofanyika: