Habari kuhusu Singapore

Singapore: Wanablogu Waikosoa Ilani ya PAP

  12 Mei 2011

Chama kinachotawala Singapore, People’s Action Party (PAP), kilitoa ilani yake ya uchaguzi tarehe 17 aprili, 2011, ambayo mara moja ilikosolewa na wanablogu wengi kwa “kutokuwa wazi”. PAP tayari kimekuwa madarakani kwa miongo mitano. Uchaguzi mkuu nchini humo umefanyika tarehe 7 Mei.

Udhibiti Nchini Singapore

  5 Agosti 2010

Singapore imesababisha kelele kubwa baada ya kupiga marufuku filamu ya aliyewahi kuwa mfungwa wa kisiasa na kumkamata mtunzi Mwingereza wa kitabu kilichoandiaka kuhusu adhabu ya kifo nchini humo. Wanablogu wanajadili.

Singapore: Kampeni ya “Kataa Ubakaji”

  23 Disemba 2009

Nchini Singapore, mara nyingi kumbaka mke wako hakuchukuliwi kama tendo la kubaka. Waandaji wa kampeni ya “Kataa Ubakaji” wanataka kukomesha sheria inayokinga ubakaji ndani ya ndoa kwa kuzindua kampeni ya kukusanya saini ambazo zitawasilishwa kwa watunga sera. Wengi wa raia wa mtandaoni wanaiunga mkono kampeni hii.

Afya Duniani: Siku ya Vyoo Duniani Yatoa Harufu

  25 Novemba 2009

Ingawa inaweza kusikika kama masihara, Siku ya Vyoo Duniani inatilia maanani kwenye suala ambalo si la mzaha linalowakwaza karibu nusu ya watu wote duniani – ukosefu wa vyoo na mfumo wa usafi.