Habari kuhusu Korea Kusini

South Korea: Ahadi ya Rais ya Ustawi Iliyoshindwa Yakosolewa

  30 Septemba 2013

Rais Park yuko kwenye wakati mgumu kwa r  ahadi yake aliyoitoa wakati wa kampeni kuwa angepandisha ruzuku ya pensheni gharama za mafunzo. Wakosoaji wanasema kampeni yake iliahidi kinyume na sera yake kama mgombea mhafidhina, ilimsaidia kuzoa kura katika uchaguzi uliopita. Akaunti ya mtandao wa twita wa @metempirics ilikusanya viunganishi vinavyohusika na...

Korea Kusini: Mpango wa Kuwakutanisha Wenzi Wakwama

  26 Disemba 2012

Mpango mpya kabisa wa kuwakutanisha wenzi kwa njia rahisi katika mkesha wa Krismas nchini Korea Kusini hatimaye ulijikuta ukishindwa kabisa baada ya waliojitokeza asilimia 90 kuwa ni wanaume. Inasemekana zaidi ya watu 20,000 walijiandikisha na hata polisi walikuwepo kufuatia uwezekano wa vitendo vya ngono za kulazimisha. Mtumiaji mmoja wa mtandaoalibainisha [ko]...

Korea ya Kusini: Mabadiliko ya Sheria kuhusu Uzazi wa Mpango Yaibua Mjadala Mkali

  17 Juni 2012

Mamlaka ya Chakula na Dawa ya nchini Korea imetangaza kwamba dawa za kuzuia mimba za dharura zinazofahamika kama 'morning-after pills' zitaanza kupatikana kwa wingi. Hata hivyo, dawa za kuzuia mimba zisizo za dharura zimekuwa dawa za kuandikwa na daktari. Mabadiliko haya ya ghafla kuhusu dawa za kuzuia kuzaliana limeibua mjadala mkubwa mtandaoni.

Korea Kusini: Maombolezo ya Kitaifa ya Mwanamwali wa Kivietnam

  8 Agosti 2010

Mwanamwali mdogo wa Kivietnam aliuwawa na mumewe wa Kikorea nchini Korea. Wanablogu wa Korea wanatoa rambirambi zao kwa kifo kibaya cha mke huyo mwenye umri mdogo huku wakiitaka serikali kutokomeza eneo hili lisiloonekana kwa urahisi la haki za binaadamu, linalohusiana na wachumba kutoka nchi za kigeni.

Korea: Ziara ya Clinton Korea Kaskazini

  12 Agosti 2009

Habari ya kushangaza. Kwa ghafla, Clinton alizuru Korea ya Kaskazini na kama vile 007 aliwarudisha nyumbani wanahabari wawili wa kike ambao walikuwa wameshikiliwa nchini Korea Kaskazini. Kuhusiana na habari hii ya ghafla, hakuna habari zilizowekwa kwenye vyombo vya habari vya umma vya Korea na hata kwenye maoni ya wanablogu. Zifuatazo...

Korea: Wajibu wa Kitaifa Wachuana na Dhamiri

  5 Agosti 2008

Kijana mmoja anayetumikia jeshi kama askari polisi aliamua kutorudi kwenye kikosi alichokuwa akifanya kazi baada ya likizo na alipeleka taarifa kuwa dhamiri yake ilikuwa ikimshtaki. Sababu ilikuwa kwamba dhamiri yake ilimshtaki baada ya kuwa amewanyanyasa raia walioshiriki katika mkesha wa tukio la kuwasha mishumaa. Uamuzi wa kijana huyu umevuta hisia...