Saudi Arabia: Familia za Wanaoshikiliwa Gerezani Zaandamana

Familia za watu wanaoshikiliwa gerezani nchini Saudi Arabia zaingia siku ya tatu ya kupinga kushikiliwa bila utaratibu maalum kwa wapendwa wao, ambao wamekuwa mahabusu kwa miaka kadhaa sasa bila ya kusomewa mashitaka yoyote. Siku hii ya tarehe 7 Julai, iliitishwa na makundi ya mawakili yasiyofahamika, ambayo ni @e3teqal [chini ya ulinzi] na @almonaseron [waungaji mkono].

Saudi Arabia ni moja ya nchi chache duniani ambazo bado zipo chini ya mfumo wa utawala wa kifalme na ina rekodi isiyoridhisha kuhusu haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kushikilia gerezani zaidi ya watu 30,000 bila sababu maalum.

Sehemu mbalimbali za dola hiyo, familia za watu wanaoshikiliwa wananing’iniza picha na ishara kama namna ya kushinikiza ndugu zao waachiwe huru. Waliandaa video na vipeperushi vilivyojaribu kuelezea sababu ya kuandamana kwao. Tofauti na siku ya kwanza na ya pili ya kuwatetea watu walioshikiliwa gerezani, safari hii madaraja yalikuwa yakilindwa na askari ili kuzuia watu wasibandike vipeperushi katika madaraja hayo. Aidha, kuta zote zilizoonekana kuwa na ishara yoyote ya kushinikiza kuachiwa kwa wafungwa, zilifutwa mara moja.
Familia iliyotiliwa mkazo zaidi ilikuwa ni ile ya ndugu Abdullah Al-Ayaf. Al-Ayaf amekuwa gerezani kwa miaka sita sasa. Kesi yake ilisikilizwa na hakukutwa na hatia lakini bado anashikiliwa gerezani. Picha yake ilitundikwa nje ya nyumba yao huko Qassim. image

Ghafla, nyumba hiyo ilizingirwa na askari pamoja na Mabahith ( magari ya polisi kanzu). Mmoja wa watu wa kundi la Mabahith aliongea wakati wa mchana na Maha Al-Dhuhaian ambaye ni mke wa Al-Ayaf, mtu huyo aliishiakumtukana mama huyo. Baadae, afisa wa polisi aliongea na mama huyo akiamuru picha hiyo iondolewe. mama huyo pia, alielezea alichofanyiwa na askari kanzu aliyemtukana.

“Sifikiri kama afisa wa usalama yeyote angeweza kutamka maneno yale” afisa wa polisi alimjibu. “Picha hiyo ndiyo iliyotufanya tufike hapa, ni vyema ukaiondoa” afisa wa polisi aliongeza.

“Picha hii inamaanisha kuwa, ninahitaji mume wangu atolewe gerezani. Usiniletee majambazi hapa. picha yenyewe yajieleza” mama huyo anamuambia askari.

Majibizano haya yaliyo katika video yalirekodiwa na Yasser, Al-Dhuhaian pamoja na mtoto wa kiume wa Al-Ayaf. Ofisa alimuuliza Yasser kama alikuwa anachukua video na Yasser alimjibu, “ndio, ninachukua video”. Ofisa huyu alipiga simu ya haraka huku mama yake na Yasser akimuambia, “wapiga simu kutoa taarifa juu ya mwanangu kuchukua video? Usifanye hivyo. Mimi ndiye niliyemuamuru kufanya hivi”

http://www.youtube.com/watch?gl=US&hl=en&client=mv-google&v=eKDgJGYZdkc

Mara tu baada ya video hiyo kuwekwa katika mtandao wa Youtube, ilishambuliwa na virusi. Watumiaji wa Twita wa nchini Saudi Arabia walianzisha kiungo ishara wakimtuhumu mtu wa Mabahith kuwa ndiye anayehusika na kashfa hiyo.

Ilifahamika kuwa, Maafisa wa polisi walimtishia Saleh ambaye ni kaka yake na Yasser kuwa, kama hatawapatia kitambulisho chaYesser, wangeharibu magari yake.

Maha Al-Dhuhaian alitwiti:

@cczz1000: الناس في صلاة الفجر تذكر الله ورجال الشرطة عند بابنا يطالبون تسليم ابنائي لهم والا سيعدم سيارتنا ..اي امن يتحدثون عنه حسبي الله وكفى

Wakati watu wakisali sala ya mapambazuko, polisi walishafika mlangoni kwangu wakinitaka niwatoe watoto wangu vinginevyo wangeharibu gari letu. Ni ulinzi gani huo wanaouongelea?

Siku iliyofuata, yaani Julai 8, polisi walifika tena na kuizingira nyumba wakishinikiza kujitokeza kwa mtoto aliyechukua video ya mahojiano. Wakati huohuo, mfanyakazi kutoka wizara ya mambo ya ndani alipiga simu akiitaka familia iifute video hiyo na kuahidi kuwa wangetimiziwa kile walichokuwa wanakihitaji.

Mara ya mwisho kuongea na Yasser, aliniambia kuwa:

“Baba yangu ataachiliwa siku za hivi karibuni. Sifanyi hivi kwa ajili ya baba yangu. Mimi siyo shujaa, lakini njia ina kiza. Na hivyo, kama siyo sisi wa kuleta mwanga, ni nani mwingine atakayetuangazia njia? blockquote>

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.