Julai, 2013

Habari kutoka Julai, 2013

Benin: Kampeni ya Kusaka Wahalifu Yawagawa Wananchi

  7 Julai 2013

Ikiwa imezinduliwa na wizara ya Mambo ya Ndani, Ulinzi wa Umma na Dini, kampeni ya Djakpata yenye lengo la kuwasaka wahalifu wote wanaojihusisha na shughuli zisizo halali ambazo zinaweza kuhatarisha hali ya utulivu ya wananchi wa Benin. Hata hivyo, kwa siku chache zilizopita, wananchi wamekuwa na maoni tofauti sana kuhusu jambo hili.

Misri yasema: “HAYAKUWA mapinduzi ya kijeshi”

Hatua ya Marekani kuingilia masuala ya ndani ya Misri - habari zinazotangazwa mashirika ya habari, hususani CNN, kuhusu siasa zinavyoendelea Misri - zilikumbana na moto jana usiku. Kung'olewa kwa rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi baada ya kudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja tu madarakani kuliamsha shamra shamra nchi nzima, pamoja na vurugu kati ya wafuasi na wapinzani wa Morsi.

Mama na Watoto Wake Wauawa kwa Kucheza kwenye Mvua

  6 Julai 2013

Mama na watoto wake wawili wa kike waliuawa kwa kufyatuliwa risasi mara baada ya watu watano waliokuwa wamefunika nyuso zao kuvamia nyumba alimokuwa akiishi mama huyu na watoto wake katika mji mdogo wa Chilas nchini Pakistan, tukio linalosadikiwa kuwa ni la mauaji ya kulinda heshima. Video iliyorekodiwa kwa simu inayowaonesha wasichana hao wakicheza kwenye mvua imekuwa ikisambaa kiholela na ambayo imeonekana kama ni kashfa na hivyo kuharibu heshima ya familia.

Misri: Wafuasi wa Morsi Wapambana na Waandamanaji Wanaompinga Morsi

Mapambano yaliyotarajiwa kati ya wafuasi wa Muslim Brotherhood na waandamanaji waliotaka rais wa zamani wa Misri Mohamed Morsi aondoke yametokea leo [June 6, 2013]. Ilikuwa kama mchezo wa kuigiza na ulionekana moja kwa moja kwenye televisheni, na ulirushwa kwa moja kwa moja na vituo vya televisheni vya ndani na vile vya kimataifa. Watu wasiopungua 17 waliuawa na zaidi ya waandamanaji 400 wakijeruhiwa katika mapigano nchini kote Misri leo, tukio ambalo mitandao mingi ya kijamii inalielezea kama "lililotarajiwa" na "linalosikitisha."

China Yawaamrisha Vijana Kuwatembelea Wazazi Wao

  6 Julai 2013

Wiki hii, China imeanza kutumia sheria mpya inayowataka watoto waliokwisha fikia umri wa kujitegemea kuwa na mazoea ya kuwatembelea wazazi wao, hali iliyopelekea sheria hii kudhihakiwa na watumiaji wa tovuti ya jukwaa maarufu la wanablogu la China lijulikanalo kama Sina Weibo.

Je, Ziara ya Obama Barani Afrika ni Neema au Hasara?

Rais wa Marekani Barack Obama amemaliza ziara yake ya siku sita katika nchi tatu za Kiafrika, Senegali, Afrika Kusini na Tanzania, mnamo Julai 2, 2013. Obama alitangaza mradi mpya, "Umeme Afrika", kukuza matumizi ya umeme mara dufu katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara. Maoni ya watu duniani kote juu ya umuhimu na matokeo ya ziara hiyo yamegawanyika mno.

Obama Barani Afrika: Vita ya Kibiashara na China?

Rais Obama ametembelea bara la Afrika kwa ziara iliyokuwa imepangwa kati ya tarehe 26 mpaka Julai 3, 2013. Hivi karibuni alikuwa nchini Afrika Kusini baada ya kutembelea Senegali na baadae aliitembelea Tanzania. Wachambuzi wengi wanaoiona safari hiyo kama mpango wa kushindana , kama jaribio la Marekani kupambana na mafanikio ya kiuchumi ya China katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Raia wa Misri Wamng'oa Morsi Madarakani

Mohamed Morsi, ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha Muslim Brotherhood siyo tena Rais wa Misri. Morsi ameondoshwa madarakani baada ya kutumikia kwa mwaka mmoja kama Rais mara baada ya maandamano makubwa nchini kote Misri yaliyomtaka kujiuzulu, maandamano hayo yalianza mapema mwezi Juni 30. Mkuu wa majeshi ya Misri, Generali Abdel Fattah Al Sisi, katika matangazo ya mojakwa moja dakika chache zilizo pita, alisema kuwa, Jaji Mkuu wa Mahakama ya Katiba ndiye atakayekuwa Rais mpya wa mpito na kwamba serikali ya kitaifa ya Kiteknokrasia itaundwa.