Global Voices Yazindua Ushirikiano na Shirika la NACLA

Global Voices na Shirika la Marekani Kaskazini Linaloshughulika na Amerika Kusini (NACLA) kwa pamoja wameanzisha ushirikiano ambao utaunganisha dira ya ‘Sauti za Dunia’ ya uanahabari wa kiraia pamoja na ile ya NACLA ya uchambuzi na utoaji wa elimu, lengo likiwa ni kuwaletea wasomaji wetu habari halisi na za kina kutoka katika eneo hili la Latini Amerika.

NACLA, lililoanzishwa mwaka 1966, ni shirika huru, lisilo la kimaslahi lililo na lengo la “kuendeleza maarifa bila mipaka” kwa njia ya kutoa taarifa na uchambuzi kuhusu Latini Amerika pamoja na hali tete ya ushirikiano kati yake na Marekani:

“tunaamini kuwa maarifa ni muhimu sana katika mabadiliko, kwa hiyo, tunatumia muunganiko wa kipekee kabisa wa taarifa/uanaharakati wa vyombo vya habari na elimu ya kawaida ili kuwapatia watu vitu wanavyovihitaji ili kuweza kuuelewa vizuri ulimwengu na kisha kuwa na uwezo wa kuubadili”

NACLA logo

Kila mwezi, waandishi wa GV(Sauti za Dunia) na NACLA watakuwa wanafanya kazi kwa pamoja ili kutoa habari zitakazokuwa zinazungumzia mada moja. Podikasti yenye mahojiano, uchambuzi na taarifa za ziada kuhusiana na mambo yaliyojadiliwa kwenye makala mbalimbali zitapatikana kila mwisho wa mwezi.

Safari za Wahamiaji

Tunaanza ushirikiano wetu kwa kuanza na mada ya “Safari za Wahamiaji”. Mwezi Julai tutakua tukizungumzia kwa mapana kabisa mambo yanayohusiana na uhamiaji: kutoka kwenye Mswada wa Uhamiaji ambao kwa sasa unajadiliwa katika bunge la Marekani, hadi kwenye habari kuhusu safari ngumu na ndefu za wahamiaji kutoka Kaskazini mwa Amerika kupitia Amerika ya Kati hadi nchini Mexico.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.