Habari kutoka Oktoba, 2009
Big Brother Africa msimu wa IV: Mageuzi yameanza
Big Brother Africa 4: Mapinduzi ni mfululizo wa nne wa vipindi vya kituo cha televisheni vinavyoonyesha maisha halisi vya Big Brother Africa, vilivyoanza Septemba 6, 2009. Kipindi hicho kimeshaanza kuzua mijadala na maoni kwenye mtandao wa intaneti kutoka kwa wanablogu na wasomaji wao.
Wanablogu Wa Asia Kusini Na Tuzo Ya Nobeli Ya Amani Aliyopewa Obama
Rais wa Marekani Barack Obama amepokea tuzo mashuhuri ya Amani ya Nobeli leo. Wanablogu na wanaoblogu habari fupi fupi huko Asia kusini wanaelezea maoni yao kuhusu habari hiyo.
Gabon: Upinzani waendelea kupinga matokeo ya Uchaguzi
Wapinzani wa kisiasa wa Gabon wanaonyesha muungano wa vyama vya siasa kupinga matokeo ya uchaguzi wa mwezi Agosti, ambayo yalimkabidhi urais mwana wa mtawala wa kiimla aliyepita, Omar Bongo. Wanasiasa na raia wanaikemea Ufaransa kwa kuingilia siasa za nchi hiyo.
Ukraine: Babi Yar
Ukrainiana anaandika kuhusu mauaji ya kimbari ya Babyn Yar/Babi Yar
Australia: Wanawake wa Kenya wakataliwa haki ya ukimbizi
Wanawake wawili wanakabiliwa na uwezekano wa kutimuliwa kutoka Australia baada ya maombi yao ya kuomba hifadhi kukataliwa, pamoja na hatari wanayoweza kuipata ya kulazimishwa tohara ya kike ikiwa watarudishwa nyumbani.
Indonesia: Tetemeko Kubwa Laikumba Sumatra
Mji wa mwambao wa Padang, Sumatra Magharibi umeharibiwa tena na tetemeko la ardhi.