Australia: Wanawake wa Kenya wakataliwa haki ya ukimbizi


Wanawake wawili wanakabiliwa na uwezekano wa kutimuliwa kutoka Australia baada ya maombi yao ya kuomba hifadhi kukataliwa, pamoja na hatari wanayoweza kuipata ya kulazimishwa tohara ya kike ikiwa watarudishwa nyumbani.

Kwa mujibu wa makala katika gazeti la Australia la The Age, Grace Gichuhi, 22, na Ndikaru Muturi, 21, walifika Australia Julai mwaka jana kwa viza ya kitalii kwa ajili ya Siku ya Vijana Duniani.

Pamekuwepo maoni kadhaa kwa suala hili kutoka kwa jamii ya wanablogu wakubwa wa siasa wa Australia. Mabadiliko wa hali ya hewa na jitihada za kuinua uchumi vilitawala wiki iliyopita.

Lakini makala ya The Age imevutia maoni 54 kutoka kwa wasomaji wa mtandaoni wakionyesha kila kitu ila kutokukubalina vikali na hali hiyo. Maoni yanaonyesha mitizamo tofauti ya mawazo, ikiwa pamoja na:

Waacheni hawa wanawake wakae
Ben | Adelaide – Septemba 22, 2009, 9:30AM

Waliomba. Maombi yao yalitathiminiwa. Maombi yao yamekataliwa. Wapelekeni nyumbani. Suala limeiisha.
David_T – Septemba 22, 2009, 9:34AM

Inasikitishaje kwamba hawa wanawake wawili wanakataliwa hifadhi. Australia ingefanya vyema kuwa na watu wengi kama wasichana hawa na kwa jinsi ninavyoona, wanakaribishwa hapa kwa muda mrefu kadri wapendavyo wao.
jollysroger | Townsville – Septemba 22, 2009, 10:22AM

Kwenye blogu yake, Pocket Carnival, Penny Eager anasema alishawishika kumwandikia Waziri wa Uhamiaji na Uraia, Chris Evans kwenye ukurasa wake wa mtandaoni, kuelezea kukerwa kwake:

Ndio kwanza nimelisikia suala la Grace Gichuhi & Teresia Ndikaru Muturi, wanawake wawili kutoka Kenye waliokataliwa haki ya hifadhi ya ukimbizi.

Ninaamini kitendo cha utesaji cha tohara ni cha kinyume, na kwamba kuwanyima wanawake hawa viza ya ukimbizi ni kuchukua msimamo dhaifu sana kwenye suala hili.

Ninawasihi kuliingilia kati suala hili, sio tu kuwasaidia wanawake hawa , lakini pia kutuma ujumbe wazi kwa Kenya kwamba Australia haivumilii vitendo hivi.

Ni suala la Kidini?
A religious issue?
Aussie News and Views blogu yenye mtindo wa kipekee wa “Kimarekani, Kiastralia, Kiisraeli, Kiingereza ‘yenye kufungamanisha imani za Kiyahudi na Kikristo’ aliweka video fupi ya habari kuhusu wanawake hawa na kuuliza:

Gee ninashangazwa nani anaweza kuwa nyuma ya suala hili? Aina gani ya dini-kifo ya kuabudu shetani inayoweza kuwa bado hai na salama huko Kenya leo ambayo ingeweza kufanya kitu kama hicho kwa wanawake wadogo hivi?

Philip Maguire kwenye Whaddya Reckon? alichukua maoni kadhaa katika posti yake:

Wanawake wawili wa Kenya wa Kikristo watatimuliwa Autralia pamoja na kukabiliwa na kifo au tohara.
Pengine wangewasili hapa huku wamejaa mapesa kwa njia ya jahazi kutoka Indonesia.

Lisa Valentine of Embrace Australia, jamii ya kimtandao ya watu wa kigeni wanaotaka kuishi Autralia, pia walilichukua suala la wasichana hao:
Wote Grace na Teresia sasa wanaogofywa na balaa watakalokabiliwa nalo kama watarudishwa Kenya.
Msemaji wa Idara ya Uhamiaji wa Australia amesema: “Kwa tamko la ukimbizi, hawakuonekana kuhusikana na wajibu iliyonayo Australia kwao kimataifa.
Wasichana hawa, pamoja na Sista Aileen Crowe, mtawa wa shirika la Fransisca anayewatunza, walikata rufaa kwa Waziri wa Uhamiaji, Chris Evans, lakini aliitupilia mbali rufani hiyo. Rufaa ya pili imekatwa tayari na wasichana hawa wanasubiri matokeo lakini wameshaambiwa wajindae kwa kurudishwa kwao.”
Kwa bahati, sheria mpya inatarajiwa kupelekwa Bungeni itakayohakikisha ulinzi kwa wasichana hawa. Sheria inaitwa Hifadhi Kamilifu na inaongeza wigo wa sababu ambazo kwazo mkimbizi aweza kuomba hifadhi.

Kampeni ya mtandaoni
Online campaign
Kwenye Facebook, ukurasa wa “Causes” wenye kichwa cha habari Saidia kuwaokoa wanawake hawa na Tohara, umeanzishwa na Waaustralia wanaounga mkono jaribio la wanwake hawa kukaa Australia. Mpaka sasa, watu 91 wameshajiunga. Habari mpya ilitundikwa Jumanne na Vanessa Muradian:
Hii ni habari mpya kabisa –chanzo kinasema wanawake hawa wamehifadhiwa hapa Australia –mpaka Evans aamue awafanyaje. Iwe atawakataa au vinginevyo, bado tunahitaji kujua…serikali inahitaji kupitisha viza mbadala…ambayo bado ninaitafiti zaidi mpaka sasa –hasa kuhusu Viza hiyo mbadala, ikiwa ‘itakidhi’ Viza ya hifadhi, ILI KWAMBA HAWA wakimbizi waingie kwenye kundi la Viza ya Hifadhi. KWA SASA viza ya hifadhi haiwalindi wanawake wanaokabiliwa na matishio ya TOHARA na mauaji. Muswada ulipelekwa Bungeni mwezi Septemba na hivi sasa chama cha Kiliberali kinaupinga mushwada huo…
Hivi sasa wanawake hawa wanahitaji kuugwa mkono na sisi –Waziri Evans atakuwa akifanya maamuzi kwa kutumia fursa yake ya Hatua za Kiuwaziri.
Ninahisi tunahitaji kuwasiliana naye…
Vilevile na vyombo vingine vya Utawala vinavyoweza kusaidia serikali kupitisha muswada mbadala!!!!!!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.