Indonesia: Tetemeko Kubwa Laikumba Sumatra

Tetemeko kubwa la ardhi limeikumba Padang, Sumatra Magharibi mnamo majira ya saa 11 jioni siku ya Jumatano.

Filamu ya video iliyotumwa na mtumiaji wa Youtube aliyeko Padang:

Tetemeko la ardhi lililotokea chini ya bahari lenye ukubwa wa vipimo vya Rikta 7.6 limesababisha madhara makubwa kwa majengo na kujeruhi watu, hasa katika maeneo ya Pariaman, sehemu ya pwani ya Padang.

Picha iliyowekwa kwenye Twitpic na marcellodecaran

Picha iliyowekwa kwenye Twitpic na marcellodecaran


Tahadhari ya kimataifa ya Tsunami [id] ilitolewa nchini Indonesia, Thailand, Malaysia pamoja na India, lakini iliondelewa baada ya kama saa moja hivi baadaye.

Shirika la Habari la Indonesia Antara liliripoti kuwa idadi ya waliofariki imefikia 75, lakini inaweza kuongezeka kwani bado kuna watu waliofunikwa chini ya kifusi, na wengine wengi bado wameamua kukaa nje [id] ya nyumba zao kwa kuogopa mitetemo mingine inayoweza kutokea.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Mamlaka ya Taifa ya Kudhibiti Majanga (BNPB) Purnomo Sidik huko Antara, makao makuu ya BNPB mjini Jakarta hayajapokea taarifa ya kina kutoka maeneo yaliyoathirika kutokana na mawasiliano mabaya huko Sumatra ya Magharibi.

Asilimia hamsini ya mji imeharibiwa na safari za ndege ziingiazo Padang zilisitishwa kufuatia uharibifu uliotokea kwenye barabara za kiwanja cha ndege cha Minangkabau.

Ulimwengu wa Twita wa Indonesia umejaa salamu za masikitiko, habari mpya kutoka kwa ndugu na ripoti za misaada.

henzter: ndiyo kwanza nimepokea majibu ya ujumbe wa simu ya mkononi kutoka kwa jamaa yangu @ sumbar: bado ninamtafuta kaka. *Ninaomba dua*

martimanurung: Majimbo ya Kusini na Kaskazini Sumatra yatalisaidia jimbo la Sumatra Magharibi katika misaada ya tetemeko.

veraalexandra: Mungu tafadhali wasaidie kaka na dada zetu walioko Padang… wape nguvu na uvumilivu.. amen.

aditdmid: bru lht dmpak gempa Padang td sore. evakuasi mlm ni trhmbt hjn deras & mati lstrk,75% kota lumpuh. smg para krbn dbri kkuatn&ktabahn. amin.

aditdmit: nimeshuhudia matokeo ya tetemeko la Padang, jioni hii uokoaji umeahirishwa kutokana na mvua kubwa pamoja na kukatika kwa umeme, asilimia 75 ya mji umepooza. Tunatumaini waathirika watapata nguvu na uvumilivu. Amen.

Makamu wa Rais, Jusuf Kalla, alifupisha ghafla ya kuwaapisha wabunge wa bunge jipya na aliwatuma mawaziri sita kwenye eneo la tukio kutathmini madhara yaliyotokea.

Aulia: Tuliwapigia kura. Ombi letu rasmi la kwanza ni kuwataka kutoa michango kutoka mifukoni mwenu kwa ajili ya waathirika wa tetemeko. Wanahitaji (michango) kuliko nyinyi mnavyohitaji.

Majira ya saa 5:45 usiku darlingalih anasema:

darlingalih: RT @isatbb: Jaringan data GPRS ISAT aman terkendali di Padang, anjuran komunikasi ke Padang via fitur BB: Email, BBM, YM, FB. Please RT

darlingalih: RT @isatbb: GPRS Indosat’s [kwa mujibu wa mwandishi: huduma ya pili kwa ukubwa ya simu za viganjani nchini Indonesia] imerudi tena huko Padang, tunawashauri kuwasiliana na padang kwa kutumia nyenzo za Blackberry: barua pepe, BBM, YM, FB.

Waziri wa Ustawi wa Jamii Abu Rizal Bakrie amesema kuwa uharibifu wa miundombine uliosababishwa na tetemeko la hivi karibuni unaweza kulingana na ule uliosababishwa na tetemeko la mwaka 2006 huko Yogakarta.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.