Wanablogu Wa Asia Kusini Na Tuzo Ya Nobeli Ya Amani Aliyopewa Obama

Picha kwa hisani ya http://www.flickr.com/photos/marcn/2174935053/ na imetumika chini ya hati miliki huria

Picha kwa hisani ya http://www.flickr.com/photos/marcn/2174935053/ na imetumika chini ya hati miliki huria


Rais wa Marekani Barack Obama amepokea tuzo mashuhuri ya Nobeli ya Amani leo. Kwa mujibu wa kamati ya Nobeli (Obama) amestahili kupokea tuzo hiyo kutokana na “juhudi zake za kuimarisha diplomasia ya kimataifa na ushirikiano baina ya watu”.

Hili limekuwa ni jambo la kushangaza kwa watu wengi duniani. Kwa nadharia tuzo hii inapaswa kutolewa kwa mtu au shirika lililojihusisha katika kupata ufumbuzi wa mgogoro mrefu wa kijeshi. Lakini kumeshawahi kuwepo na utofauti huko nyuma na Obama ni mmoja wa hali hizo tofauti kwani alianza kazi ya urais baada ya kupendekezwa mwezi Februari.

Gazeti la The New york Times limetoa muhtasari wa baadhi ya marejeo ya maoni kutoka duniani kote. Sasa hebu na tuangalie jinsi wanablogu na wale wanaoblogu makala fupi fupi kutokea Asia Kusini wanavyoelezea maoni yao kuhusu habari hii.

Kutokea Bangladeshi, An Ordinary Citizen haamini na anasema kuwa tuzo hiyo imetolewa kabla ya wakati wake.

Tunazienzi juhudi zake za kuleta amani ambazo huwa anazianzisha tu na bado tunasubiri matokeo.
Je si kweli kwamba muda bado haujafika kwake kuipokea tuzo hiyo? Hatuna hakika ni kwa jinsi gani (tuzo hii) itaathiri mtazamo wake.

Mwanablogu wa India Churumuri anayo maswali kadhaa rahisi:

Je Obama anastahili tuzo hii? Je amefanya jambo lolote linaloihalalisha? Je kwa kumpa kijana mbichi kama huyu, wakati wa uchanga wa urais wake, kunawashusha hadhi wale wote waliofanya kazi ngumu na kwa muda mrefu ili kuipokea? Au haidhuru chochote, kwani tuzo ya Nobeli ni tuzo ya kisiasa aliyopewa Yasser Arafat na Menanchem Begin? (kama vile ambavyo yeyote aliyewahi kusoma The Prize kilichoandikwa na Irvin Wallace anaweza kufahamu)

Na bado kutokea India, Zooni ni mshabiki wa Obama, lakini ameshangazwa pia:

Ok kabla haujafikiria vibaya mimi si kati ya wale wanaomchukia Obama… ninampenda vilivyo, nimeandika makala ya kumpongeza kwa ushindi wake wa urais, je ameshinda nini na kwa sababu ipi, alikuwa kazini kwa wiki 2 tu wakati alipopendekezwa (mapendekezo yalikoma tarehe 1 Februari). Nadhani Obama alishinda tuzo kutokana na kampeni yake kabambe!

Kutokea Pakistan, Temporal wa blogu ya Baithak amekuwa mkali kidogo katika maoni yake:

Mwaka huu unaweza ukawa ndio mwaka ambao utaashiria kuanza kushuka kwa tuzo ya Nobeli. Wanakamati walikuwa wanakula au kuvuta kitu gani?

Rais Obama anaweza kustahili tuzo hii katika miaka ijayo. Lakini sio katika wakati huu. Ndio kwanza ameanza jitihada na ado hajaacha alama yake kwenye amani ya dunia.

Mwanablogu wa Ki-Sri Lanka Indi.ca anafikiri kuwa tuzo hii itamuumiza Obama nyumbani (Marekani):

Nafikiri kuwa Obama ni mtu muungwana zaidi anayetembea katika uso wa dunia hii leo. Hata hivyo, sidhani kama ameshafanya kile ambacho anataka kukifanya. Nobeli inaweza kumsaidia kinadharia, lakini inaweza kumuumiza nyumbani (Marekani).

Wanaondika blogu fupi fupi duniani kote walikuwa wametingwa leo kwa kuelezea mshangao na kutoamini baada ya kuzisikia habari. Yafuatayo ni baadhi ya maoni kutoka kwa watumiaji wa Twita wa Asia Kusini:

@vijaysankaran: Tuzo ya nobeli sasa imekuwa kama Bharat Ratna… inahusu wewe ni nani, na siyo ulichokifanya-)

@tantanoo: kwa hiyo Bush alitangaza vita, Obama anaomba amani na kushinda tuzo ya Nobeli. Mahesabu mazuri.

santhemant: “rais wa Marekani Obama apokea tuzo ya Amani kwa kuendesha VITA sehemu nyingi.. kwa kuiunga mkono Pakistani na kupuuza nchi za kidemokrasia kama vile India.

saniakhan: sijui kama naweza kuunga mkono ushindi wa Rais Obama wa Tuzo ya Nobeli huku kukiwa na ndege za kivita za drones huko Pakistan bado zikiendelea kupiga.

YusufKhan: Guantanamo bado iko wazi, ndege za drone bado zinaangusha mabomu huko Pakistani, vita bado vinaendelea huko Iraq/Afghanistan, na bado Obama anashinda tuzo ya Amani ya Nobeli. Yay.

@TinyToots: mimi pia ninahitaji Tuzo ya Amani ya Nobeli. Kila siku ninajiepusha na kuwafanyia fujo watu wengi. Kwa nini hakuna mtu anayenipendekeza?

@OldmonkMGM: mchague mtu asiyefanana na wengine: Dalai Lama, Mother Teresa, Martin Luther King, Barack Obama.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.