Big Brother Africa 4: Mapinduzi ni mfululizo wa nne wa vipindi vya kituo cha televisheni vinavyoonyesha maisha halisi vya Big Brother Africa, vilivyoanza Septemba 6, 2009. Mfululizo huu wa nne utakuwa hewani kwa siku 91 na mshindi atarudi nyumbani na kitita cha dola za kimarekani 200,000.
Kipindi hicho tayari kimezua mijadala mtandaoni kama ilivyokuwa kwa Big Brother III.
Accra Conscious anatundika taarifa za muhimu kuhusu kipindi hicho:
Muda wa kulala hautakuwa ule ule tena kwa sababu washiriki wote 14 wanashindania kupata usiku mtulivu wa kupanga namna ya kuzikamata Dola za Kimarekani 200,000 kama zawadi!
Habari zaidi kuhusu BBA Mapinduzi.• Fedha za zawadi ya Big Brother Africa ya mwaka huu imezidishwa mara dufu –sasa itakuwa Dola za Kimarekani 200,000, bahati nasibu ya ‘mshindi anachukua zote’.
• Msimu huu mpya una uwezo kama mara mbili zaidi wa uonekanaji na uwezo wa sauti kuliko ilivyokuwa msimu wa 1, 2 au wa 3: kutakuwa na kamera 40, ‘zinazoangalia kila kitu, na kufahamu yote’na vipaza sauti 100.
• Sheria za zamani za kuzuia njama kwenye jumba zimeondolewa na sasa washiriki watakuwa huru kuunda makundi, kujadili mikakati wazi wazi na kucheza mchezo kwa njia tofauti kabisa.
• Mwaka huu, watazamaji watatakiwa kuwapigia kura washiriki wanaowataka wabaki kwenye jumba badala ya kuwapigia kura wakaazi wanaotaka watoke.
• Mwaka huu kutakuwa na washiriki 14 watakaoishi kwenye jumba, ikilinganishwa na 12 wa misimu iliyopita, mwaka huu utajumuisha washiriki kutoka Msumbiji na Ethiopia. Nchi nyingine 12 ni: Angola, Botswana, Ghana, Kenya, Malawi, Namibia, Naijeria, Afrika Kusini, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.
Rafiq anaandika kuhusu huduma ya bure ya SMS kwa jili ya kuwapigia kura washiriki:
Unapokuja wakati wa kupiga kura kwenye Big Brother Africa 4: The revolution kutuma SMS nyingi au kupiga kura kunaweza kuwa ghali sana. Kwa bahati kuna njia mbadala unazoweza kuwapiga kura kwa wakaazi wa jumba la Big Brother Africa kwa njia ya Mtandao na…*drum roll* MXit.
Hii ni njia ya haraka na rahisi kwa watumiaji milioni 14 wa huduma ya change MXit ili kuwapigia kura washiriki wawapendao wa BBA 4. Ninaona kuwa huu ni ushindi mkubwa kwa huduma ya MXit katika mchakato wao wa usiokoma wa kuwafikia watumiaji wengi zaidi barani kote Afrika. Nitaijaribu ili nipate kiasi fulani kabla na baada ya takwimu kutoka nchi zote 14 ambako washiriki wa BBA wanatoka na kuona kama idadi ya MXit kweli inaongezeka ndani ya sehemu hizo.
David Ajao hafurahii kushangiliwa kwa vitendo vya mahusiano ya kiholela-holela ya kimapenzi kwenye kipindi hicho:
Kusuasua au tahadhari yangu kuhusu Big Brother Africa siku zote imekuwa ni kule kushabikiwa kwa mahusiano holela ya kimapenzi.
Noni anafikiri kuwa toleo la mwaka huu la Big Brother linachefua:
BIG BROTHER INACHEFUA MWAKA HUU! WAVULANA WANA SURA MBAYA! KWA NINI BIG BROTHER MTUKATISHE TAMAA HIVI? HAKUNA HATA WAVULANA 2 AU 3 WENYE SURA NZURI KWENYE JUMBA LILE! NIMEKATISHWA TAMAA.
Mika anawachambua washiriki:
Jeremy kutoka Kenya anaonekana ni mzuri wa sura, na Itai wa Zimbabwe anaonekana kama ana maumbile makubwa…Siwezi kungeja saa ya kuoga. Hannington wa Uganda anaonekana kama malkia, anajielezea kwa maneno matano (sita) kama “Mimi ni mungu kati ya wanaume” …Ummm poa dada! Ninashangaa jamaa wangapi ni mashoga? Ni suala la kujificha ushoga…? Potelea mbali, Quinn, wa Afrika Kusini alikuwa katika nne bora katika kumtafuta Kijana Mweupe DJ wa YFM.
Na hivyo ndivyo anavyofanya Rafshizzle, mwanablogu kutoka Uganda:
Hannington Kuteesa Kavuma – ni mtoto wa Jaji Kavuma na Mbunge Ruth Kavuma. Ndio kwanza amerudi kutoka Malaysia alikokuwa akisoma kozi ya Teknolojia ya Habari (IT). Huwezi kuamini tulikuwa na huyu jamaa pale kwenye Klabu ya Rugbi ya Kampala na alikuwa hatuambii kitu, naam, kila la heri kwake. Wakati huo huo, Mganda mwingine anaitwa Filbert Okure na bado tunakusanya habari zake kwa bakia hapa hapa. (Wanatuambia, Hannington atatolewa mbu). Haidhuru, Zimbabwe imemtuma Itai Makumbe –mwenye umri wa miaka 31 anayependa siasa. Na ulihisi sawa sawa, wanasiasa wengi wanachosha isipokuwa majamaa kama Ken Lukyamuzi, Rais Museveni na Idd Amin (Mungu Amweke Pema Peponi). Kenya nayo ina wawili Edward Muthusi (kwa jina lingine Teddy) na Jeremy Ndirangu. Naijeria imemtuma Kevin Chuwang – kijana asiye na kazi mwenye miaka 27. Kutoka Botswana: Kaone Ramontshonyana – Kwa kweli nimeshindwa kabisa kumwelewa huyu kijana. Ethiopia inayoingia kwa mara ya kwanza imewakilishwa na Yacob Yehdego –ameahidi kuwa mkweli, jambo ambalo karibu kila Muethiopia hulisema. Jina lake la utani ni Yac. Tunahitaji kungoja…Mwenyeji Afrika Kusini ina Mzungu anayeitwa Quinn Silder –kwa umri wake wa miaka 21, huyu mcheshi mweupe anakuwa mshiriki mdogo zaidi kuliko wote jumbani; pia ni Dj na mtangazaji wa redio kwa hivyo lazima awe mjuzi wa namna ya kuwaburudisha watu. Nchi nyingine inayoshiriki kwa mara ya kwanza, Msumbiji imemtuma Leonel Estevda mwenye umri wa miaka 23.
Pen Powder anakosoa wazo la mwaka huu la Mapinduzi:
Nilikuwa naanza kufurahia mambo mapya kwenye Big Brother Africa Revolution lakini baada ya kushuhudia kuondolewa kwa Ras Wayo na kutotambulishwa mshiriki wa kike wa Ghana, Ninadhani dhana ya mageuzi haikufikiriwa kwa kina chake na pengine si jambo zuri. Mambo mengine yanayotokea hayana maana kabisa katika kina chake: kwa nini wawepo washiriki wengi zaidi kutoka nchi fulani zaidi ya nchi nyingine wakati kwa kweli dhana ya kuwa na kipindi cha bara zima ilikuwa ni kuzileta nchi mbalimbali pamoja. Baada ya kuingizwa washiriki 12 wa kike kwenye jumba jumapili, hivi sasa kuna Wanaijeria 4, Wakenya 2 na washiriki wawili wawili wa nchi nyingine wakati Ghana haina mwakilishi kipindi hiki. Hivi hii ni kwa ajili ya kuongeza mvuto kwa watazamaji? Au baadhi ya nchi zinawakilishwa zaidi kwenye jumba hilo kwa sababu tu M-net/DStv inataka kuvuna faida zaidi kutoka kwenye nchi hizo? Jambo moja la kuchekesha ni kwamba Big Brother imeruhusu “njama za kura” msimu huu na inaonekana kuwa makundi yatatengenezwa kufuata utaifa. Hili bila shaka litatengeneza chuki miongoni mwa washiriki na bado eti M-net wakaja kwa ujasiri kusema kwamba wamebadili kanuni za kupiga kura mwaka huu ili eti watu wapige kura kumwokoa wampendae badala ya kupiga kura kumtoa wasiyemshabikia ili kusisitiza ‘uchanya’ badala ya ‘uhasi.’ Katika tangazo lisilotarajiwa, mwakilishi wa Ghana, Ras Wayo akawa mshiriki wa pili kuondolewa kutoka kwenye jumba la BBA wakati wa kipindi cha kwanza cha Kutolewa kwa mshiriki. Wayoe alipanda jukwaani huku washabiki wa jukwaani wakiliimba jina lake juu ya muziki wa miondoko ya Rege. Alimwambia IK, mwongoza kipindi, kwamba hakustaajabishwa kutoka jumbani na kwamba hafikiri kwamba mwenendo wake wa maisha ya Kirastafariani ilichangia kuwafanya watazamaji kutokumpigia kura. Naam, wa-Ghana hawajastaajabishwa pia kwa sababu lafudhi yake ya Kijamaika ya Patois ilikuwa ni jambo lilizongumzwa sana mara tu alipotambulishwa kwenye jumba hilo. Hivyo, kabla ya yote, ni kwa nini Ras Wayo alichaguliwa kuiwakilisha Ghana? M-net na watayarishaji wa kipindi walimchagua mtu ambaye kwa mtazamo wao angetoa thamani kubwa ya burudani kwa watazamaji kutoka kwenye nchi washiriki.
Narcissus anauliza, “hivi ni mimi tu au ni kila mtu anahisi Itai ni shoga?”:
Hivi vijimambo vidogo vilistua rada zangu za kuwatambua mashoga kufikia upeo wake: Moja ya vipindi anavyovipenda zaidi ni, subiri, America’s Next Top Model (Najua!.) Moja ya tabia zake mbaya ni pamoja na, kujitazama na kujichekelea mwenyewe kwenye kioo (haloo huku ni kujipa umuhimu kupita kiasi, aha). Mwisho, na kwa vyovyote si kwa umuhimu, akishinda mipesa hiyo, anapanga kuzitumia kugharamia safari za London, Paris, New York na Los Angeles, kweli? Wacha!
Hizi mbili ndizo sababu pekee zinazonifanya ‘niweze’ kutazama kipindi hicho. Ninategemea jumba hilo limesheheni vipodozi na Geisha ambavyo “haviishi upesi”, kwa sababu itakuwa wiki ndefu kwa vijana, hebu nicheke mie. Kwa uwazi hata hivyo, Nilitegemea “mapinduzi” zaidi, na si kurejea dhana ambazo zimekwishatumika kule Uhispania katika toleo lao la Big Brother.
Ms B anajichukulia yeye kuwa shabiki “’asiye na aibu wa kipindi hiki cha kuonyesha uhalisia” Anazungumzia urembo wa washiriki wa kike:
Mapodozi yalikuwa ya ajabu, hakuna mwanamke mweusi duniani mwenye mashavu mekundu!!! Hakuna!! Ukitaka mtafute!!! Malkia ‘jike dume’ alikuwa na nyusi ndefu zinazoweza kumdaka nzi na Nonhle alikuwa na kucha zilizopakwa rangi ya njano ambayo haikuwa na cha kusaidia kwenye mavazi yake. Najua wanamitindo mara nyingine huwa hawaoanishi rangi ili kuzioanisha lakini ilionekana kama vile hakuwa na hakika avae vipi. Hatuwezi wote kuwa akina Rihanna sasa, sivyo?
Nachukia wanawake wanapofanya hivyo! Hakuna kinachovutia (kwangu) mtu kuoneakana kama kituko. Kujiremba kunapaswa kuuzidisha zaidi urembo wako, na sio kuuficha. Rahisisheni kazi nyie wajinga!!! Na hawa wanawake wanawakilisha wanawake wengine wa Kiafrika wanapotoka, du masikini!!!