Gabon: Upinzani waendelea kupinga matokeo ya Uchaguzi

Kifo cha Omar Bongo, mmoja wa madikteta wa Kiafrika waliokaa kwa muda mrefu zaidi madarakani, mwezi Juni, kilileta matumaini kwamba Gabon ingeanza namna mpya ya siasa. Lakini, alipotangazwa mtoto wa Bongo, Ali Ben Bongo, mgombea wa chama tawala, kuwa mshindi wa uchaguzi wa tarehe 31 Agosti, wachache walishangazwa. Kama mwanablogu mmoja wa lugha ya kifaransa Le petit Quimonte illustre anavyoeleza:

Au Gabon, la Couronne est héréditaire, de mâle en mâle par ordre de primogéniture élue démocratiquement par succession directe au suffrage universel sous protection militaire.

Katika Gabon, Kofia ya uongozi ni ya kurithishana, kutoka kwa mwanamume kwenda kwa mwanamume kwa utaratibu wa kuangalia mzawa wa kwanza, akichaguliwa kidemokrasia kwa kuachiana kwa wazi kupitia haki ya sanduku la kura, chini ya ulinzi wa jeshi.

Na bado wanachama wa upinzani wanakataa kurudi makwao kwa utulivu.

Wiki jana, Vyama vya upinzani vya Gabon viliitisha mgomo wa kitaifa wa siku tatu, kupinga uchaguzi wa mwezi uliopita, na kuonyesha mshikamano na waathirika wa ghasia za baada ya uchaguzi Port Gentil (ingawa kwa mujibu wa habari za kimataifa, wachache sana kama kweli walikuwepo waliitikia wito huo). Gabon Libre Expression (kupitia Afrik.com) linaripoti kwamba baadhi ya wagombea wa upinzani wanatoa matokeo yao mbadala yanayomweka mgombea wa chama cha UPG Pierre Mamboundou mbele ya Bongo, kwa zaidi ya asilimia 68% ya kura zilizopigwa.

Siku ya Alhamisi, wagombea wa upinzani walitoa tamko la pamoja na kwa uchache tisa kati yao wamefungua mashitaka kwenye Mahakama ya Kikatiba ya Gabon wakitoa wito wa kubatilishwa kwa uchaguzi wa Agosti 31, ambapo mgombea wa zamani Runo Ben Moubamba anauita “uchaguzi wa kulazimishia madaraka,” kwa minajili ya udanganyifu wa kura na makosa mengineyo. Mahakama ina mwezi mmoja kufanyia kazi mashitaka hayo, lakini kama makala ya hivi majuzi kwenye Afrik.com inavyosema, kwa jinsi mahakama ilivyofungamana kwa karibu na familia ya Bongo, upinzani unajipa matumaini kiduchu mno ya matokeo mazuri.

Idumu Afrika yenye mizizi ya kifaransa!

Ukaribu wa muda mrefu wa Ufaransa na familia ya Bongo, kwa namna fulani unapaswa kubeba lawama. Waandamanaji wa Port –Gentil walikusudia walizilenga mali zilizomilikiwa na Total, kampuni ya mafuta ya Kifaransa , wakati wa vurugu za baada ya uchaguzi zilizosababisha watu wasiopungua watatu kupoteza maisha yao.

Maandamano ya kupinga uchaguzi huko Paris yamepangwa kufanyika Jumatano hii, na walau kwenye wavuti za habari za ki-Gabon, kuna wito wa kugomea bidhaa za Kifaransa.

Pour Un Gabon Meilleur! anaeleza historia ya makapuni ya Kifaransa huko Gabon, na uhusiano wake wa karibu na familia ya Bongo:

Elf, rebaptisé aujourd’hui Total, est la plus connue des entreprises françaises qui exploite les richesses du Gabon du fait de l’affaire qui à partir de 1994 et jusqu’au procès de 2004 a donné un coup de projecteur sur les liens entre les dirigeants de la société pétrolière, la famille Bongo, la mafia et les sommets de l’appareil d’État français.
Mais en fait, c’est l’ensemble de l’économie du pays qui est sous la coupe de sociétés françaises et il est difficile de toutes les citer. Le clan Bongo est servi au passage, étalant un luxe provoquant au milieu du dénuement. Mais l’essentiel de la richesse produite par les travailleurs du pétrole, des mines, de l’extraction forestière, du transport et des activités portuaires, etc., profite à des patrons et des actionnaires d’entreprises dont le siège est par exemple à Odet dans le Finistère (Bolloré), à la Tour Montparnasse à Paris (Eramet), à La Défense (Areva) ou à Niort (Rougier, pour l’exploitation et le négoce des bois tropicaux).

Elf, ambayo leo imepewa jina la Total, ni kampuni ya Kifaransa inayojulikana zaidi kuliko makampuni mengine ya Kifaransa inayochota utajiri wa Gabon kutokana na utata ulizozuka 1994 mpaka 2004 na ambao umeweka wazi uhusiano baina ya utawala wa kampuni ya mafuta, familia ya Bongo, genge la mafia, na vilele vya vyombo vya kitaifa vya Ufaransa.
Lakini kwa hakika, uchumi wote wa nchi iko chini ya dole gumba la makampuni ya Kifaransa, na ni vigumu kuyataja yote. Ukoo wa Bongo umebaki kuwa na kiburi na majigambo ya ufahari katikati ya ufukara wa kutisha wa wananchi. Lakini utajiri mwingi unaotengenezwa na wafanyakazi (wa Ki-Gabon) wa mafuta, machimbo ya madini, mbao, usafirishaji na bandari wanaufaidi wamiliki na wanahisa wa makampuni hayo ambayo ofisi zao kuu ziko katika sehemu za, kwa mfano Odet (Bolloré), Tour Montparnasse huko Paris (Eramet), La Defense (Areva) au Niort (Rougier, kwa unyonyaji wa biashara ya mbao za ukanda wa kitropiki).

Alliance Nationale de la Resistance du Tchad, anaonyesha histroria ya muda ambao Ufaransa inahisiwa kujihusisha na uchaguzi, ambayo inapelekea katika nukuu ambayo si maarufu tena ya Robert Bourgi aliyoitoa kwa Le Monde jioni ya uchaguzi: “Nchini Gabon, Ufaransa si mgombea, lakini mgombea wa Robert Bourgit ni Ali Bongo. Sasa, mimi ndiye rafiki ambaye Nicholas Sarkozy anamsikiliza. Bila shaka, wapiga kura wataelewa” [Fr].

Wasomaji wa La Voix Du Peuple Gabonais wanajadili uwezekano wa kugomea bidhaa za Ufaransa. Ondonza anaandika:

je suis entièrement d'accord avec le boycotte, c'est une mesure de pression efficace qui peut amener les francais à revoir leur position, dans la mesure où le chiffre d'affaires de leurs sociétés diminuera à long terme, ils seront obligés de fermer et rentrer chez eux. Pour cela aussi bien les hommes d'affaires, étudiants, touristes et autres ne devraient plus prendre Air france ou Gabon airlines, une alternative sera de prendre la Lufthansa, Ethiopia airlines et autres compagnies. Les automobilistes ne devraient plus consommer le carburant de Total, ni de la Lybian oil. Penser consommer Gabonais maintenant cela fera rehausser le pouvoir d'achat des petits commercants gabonais.
Que Dieu benisse le Gabon

Ninakubaliana kabisa na mgomo huu: Ni zana sawia ya shinikizo linaloweza kuifanya Ufaransa ifikirie nafasi yao…wafanyabiashara, wanafunzi, watalii na wengine kamwe wasipande ndege za Air France au Gabon Airlines, lakini wapande Lufthansa, Ethiopia au makampuni mengine kama mbdala. Madereva wasitumie mafuta ya kampuni ya Total, wala yale ya Lybia. Kufikiria kununua bidhaa zinazotengenezwa na wa-Gabon kutainua uwezo wa manunuzi wa wafanyibiashara wadogo wa ki-Gabon.
Na Mungu aibariki Gabon.

Aligatoire anashangaa namna mgomo huo unavyoweza kufanikiwa, kwa kuzingatia utegemezi uliopindukia wa Gabo kwa mkoloni wake wa zamani:

Boycotter les produits français, je me demande comment? notre économie ne produit rien. Cela suppose boycotter tout les groupes CFAO, CECADIS,TOTAL,SMAG,BNP(bicig) bgfi,crédit lyonnais (ugb), SEEG, LIBERTIS(les bongo). DRAGAGE……commençons donc par créer une banque gabonaise et des entreprises gabonaises. Il faut donc commencer à être décomplexé de l'homme blanc. car bcp d'africains souffrent d'un complexe d'inferiorité face l'homme occidental.Cette lutte doit être d'abord psychlogique et culturelle.Tous nos dirigeants sont à la merci des occidentaux au détriment de leur peuple. Nous sommes dans les mêmes configurations lors de la traite négrière, le chef coutumier et le négrier.

Kugomea bidhaa za kifaransa? Kivipi? Uchumi wetu hauzalishi kitu. Hiyo itamaanisha kugomea makampuni kama CFAO, CECADIS,TOTAL,SMAG,BNP(bicig), bgfi,crédit lyonnais (ugb), SEEG, LIBERTIS, na mengine…tuanze kwa kuanzisha Benki ya Ki-Gabon na makampuni ya ki-Gabon. Tunatakiwa tuanze kwa kujikomboa kwenye vifungo vyetu wenyewe, kwa sababu Waafrika tunateswa na kule kusiona duni dhidi ya mzungu wa kimagharibi. Vita hii ni lazima iwe, kwa kuanzia kabisa, ya kiutambuzi/saikolojia na kiutamaduni. Viongozi wetu wanategemea Magharibi, na kuwaangamiza watu wao wenyewe. Tupo mahali pale pale tulikokuwa enzi za biashara ya utumwa, chifu wa kimila na mfanyabiashara ya watumwa.

Alphonse Obiang, katika maoni aliyoyaacha kwenye Alliance Nationale de la Resistance du Tchad, anaurudisha wajibu kwa wanasiasa wa Ki-Gabon:

Cet article est du grand n'importe quoi!…je ne vois pas ce que paris vient faire là, sauf si vous prétendez que c'est paris qui a contraint les anti-bongo à diviser leurs voix par 22. le résultat est clair: prise en semble, l'opposition dépasse largement les 50%. divisée, ali bongo passe haut la maion. Tout le reste n'est qu'explications facile et foutage dd gueule.

Makala hii imejaa…siwezi kuona kile ambacho Paris imekifanya, labda udai ni Paris ndiyo iliwalazimisha wapinzani wa Bongo kujigawa katika makundi 22. Matokeo yako wazi: kwa pamoja, upinzani ulipata zaidi ya asilimia 50. Ugawanywa, Ali Bongo alishinda kiulaini. Mengineyo zaidi, ni maelezo rahisi na upuuzi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.