Oktoba, 2009

Habari kutoka Oktoba, 2009

Marekani: Wanandoa wa rangi tofauti wanyimwa cheti cha ndoa

  25 Oktoba 2009

Juma lililopita huko Hammond, Louisiana, wapenzi wawili walituma maombi ya kibali cha kufunga ndoa na walikataliwa kwa misingi ya rangi zao tofauti. Afisa wa kutathmini na kuandikisha nyaraka (Muamuzi wa Amani) alidai kuwa “ndoa baina ya watu wa rangi hazidumu” na alisema kuwa anafanya hivyo “kwa ajili ya watoto.”

Uanaharakati na Umama Barani Asia

  24 Oktoba 2009

Je, mwanamke anatoa sadaka zipi ili kupigania jambo analiamini? Je, watoto wake wanaathiriwa vipi na mateso yanayoelekezwa kwake? Makala hii inachambua kwa kifupi maisha ya wanawake wanaharakati katika Asia ambao pia ni ma-mama.

China: Ndoto ya Nobel

Kila mwaka, wakati wa kutangaza mshindi wa Tuzo ya Nobel unapowadia, Wachina hugubikwa na hamasa fulani hivi. Endapo mshindi ni yule wa asili ya Uchina, basi wao hufurahi sana. Lakini mara baada ya kupita siku chache, furaha hiyo huanza kupoa au hata kugeuka na kuwa simanzi. Mwaka unaofuata wakati unapowadia tena, hali hujirudia tena kama hapo awali.

Ghana: Siku ya Kublogu mwaka 2009

Kwenye siku ya Kublogu Kwa Vitendo Duniani, Waghana waliwahoji viongozi wa dunia, walichachafya karatasi za Benki ya Dunia, walitambulisha tovuti mpya na walijiuliza ni kwa nini kulikuwa na majadiliano machache sana yanayohusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa nchini – na pia walitambua kwamba kuna mambo fulani nchi kama Ghana zinayafanya vyema.