Habari kuhusu Habari Kuu kutoka Mei, 2013
Ijue Mauritania kwa Jicho la Msanii wa Kireno
Msanii wa Kireno Isabel Fiadeiro anayeishi katika mji wa Nouakchott, Mauritania, ambako anachora na kuendesha maonyesho ya kazi ya sanaa. Fiadeiro vilevile huchora madhari kwa kuyatazama, hujaza blogu yake anayoiita Michoro nchini Mauritania na michoro ya maisha ya kila siku katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Global Voices ilizungumza na Fiadeiro kuhusu kazi yake ya sanaa na namna michoro yake ilivyomsaidia kuifahamu Mauritania.
VIDEO: Namna Watu Wawili Tofauti Walivyopinga Dhuluma na Kushinda
Mkhuseli "Khusta" Jack na Oscar Olivera waliongoza harakati tofauti za kiraia zisizohusisha vurugu, moja ikiwa ni Afrika Kusini mwaka 1985 nyingine ikiwa ni Bolvia mwaka 2000. Video iliyoandaliwa na Shule ya Uandishi wa Weledi inasimulia habari zao
Mwandishi Habari za Kiraia wa Miaka 14 Auawa Akiripoti Mapigano Nchini Syria
Omar Qatifaan, mwanaharakati wa Habari mwenye umri wa miaka 14 ameuawa akiwa katika jitihada za kutangaza habari za mapigano kati ya vikosi vya kijeshi vinavyoiunga mkono serikali na vile vya waasi katika eneo la Daraa al-Ballad kusini mwa Sryria karibu na mpaka wa Jordan.
Je, Baada ya miaka 50, Chama Tawala cha Malaysia Kitashinda Uchaguzi?
Malaysia wnaajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa 13 utakaofanyika Mei 5. Maudhui yanayotawala duru za kampeni za uchaguzi huo ni matarajio makubwa waliyonayo wananchi, au 'ubah' kwa lugha ya wenyeji. Je Chama tawala cha Barisan Nasional, kilichokaa madarakani kwa miaka 50, kitaendelea kutawala nchi hiyo?
Jamhuri ya Dominika: Mwanafunzi Auawa kwenye Maandamano
Mnamo siku ya Alhamisi ya tarehe 8 Novemba, 2012, Chuo Kikuu cha Santo Domingo kiligeuka kuwa uwanja wa maandamano yanayopinga mpango wa serikali kubana matumizi. Wakati wa maandamano, polisi walisababisha kifo cha mwanafunzi wa udaktari mwenye miaka 21, William Florián Ramírez. Haikuchukua muda mrefu sakata hilo lilihamia katika mitandao ya kijamii.
Saudi Arabia Yawanyonga Raia Watano wa Yemeni na Kutundika Miili Yao Hadharani
Raia watano wa Yemeni waliotiwa hatiani kwa mauaji na ujambazi walinyongwa kwa kukatwa kichwa nchini Saudi Arabia na miili yake kuanikwa hadharani huko Jizan, mji ullio kusinimagharibi mwa nchi hiyo. Picha za miili hiyo ikining'inia kwenye kamba hewani ilisambaa kwenye mtandao wa Twita na facebook kama hatua ya wa-Yemeni kupinga ukatili huo.
Rafael Correa Aapishwa kwa Kipindi cha Tatu Kama Rais wa Ekuado
Rafael Correa ameapishwa kuingia ikulu kama Rais wa Jamhuri ya Ekuado kutawala mpaka 2017..
Mwanamke Aokolewa Kwenye Kifusi Baada ya Siku 17
Siku ifananayo na ile iliyogharimu maisha ya watu mara baada ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa tisa huko Savar pembezoni mwa mji mkuu wa Banglasesh, Dhaka, idadi ya watu waliofariki imeongezeka hadi 1,055 , idadi inayopelekea tukio hili kuwa tukio lililowahi kuua watu wengi zaidi tokea lile la tarehe 9/11 kulipotokea mashambulizi ya kigaidi, mfanyakazi mwanamke ajulikanaye kwa jina la Reshma Begum amekutwa akiwa hai mara baada ya kuzuiwa na kifusi cha jengo hilo kwa siku 17.
Pakistan: Imran Khan Aanguka na Kuumia Akiwa Kwenye Jukwaa la Kampeni
Aliyekuwa mchezaji maarufu wa kriketi na kisha kuamua kuwa mwanasiasa, ambaye kampeni yake ina tumaini kubwa la kuleta "Pakistan Mpya" aliyeweza kushawishi idadi kubwa ya vijana pamoja na wapiga kura wanaotokea mijini katika mikutano yake, alivunjika vifupa vitatu vya uti wa mgongo pamoja na mbavu baada ya kuanguka kutoka kwenye winchi iliyokuwa katika kimo cha futi 15 mda mfupi kabla ya kuhutubia. tukio hili limeonekana kuliunganisha tena taifa hili lililojigawa kwa visasi vinavyotokana na uchaguzi utakaofanyika mapema wiki hii.
Bangladesh: Waislamu Wadai Wanawake Wabaki Majumbani
Wanachama wa kikundi chenye msimamo mkali cha Kiislamu nchini kimewashambulia wanahabari wa kike waliokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kiuandishi wakati kikundi hicho kilipokuwa kikifanya maandamano katika jiji la Dakar kudai kutumika kwa sheria kali za kiislamu, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku wanawake kuchanganyika na wanaume. Mpaka madai yao yatakapotekelezwa, chama hicho kimejiapiza kulitenga jiji la Dhaka na sehemu nyingine za nchi hiyo ifikapo Mei 5, 2013 kwa kuwaweka wanaharakati wake katika maeneo sita ya kuingilia jiji hilo.