· Julai, 2009

Habari kuhusu Habari Kuu kutoka Julai, 2009

Afrika: Ujio wa Mkonga wa Seacom Wazua Mjadala

Ujio wa mkonga unaopita chini ya bahari utakao ongeza uwezo na kupunguza gharama za intaneti barani Afrika umewasha majadiliano na mvuto katika ulimwengu wa blogu wa Afrika. Seacom, ambayo inaunganisha Afrika Kusini, Tanzania, Kenya, Uganda na Msumbiji na Ulaya pamoja na Asia, ilianza kutumika moja kwa moja Alhamisi, kwa kuziunganisha nchi za Afrika ya mashariki na Afrika ya kusini kwenye mtandao wa dunia wenye wigo mpana.

Kongo Brazzaville: Uchaguzi wa Rais Wakatisha Tamaa

Siku ya Jumapili, Julai 12, watu wa Jamhuri ya Kongo walipiga kura katika uchaguzi ambao ulisusiwa na viongozi wa Upinzani kwa madai kwamba usingekuwa huru wala wa haki. Denis Sassou N’Guesso, ambaye ameitawala Kongo kwa takribani miaka 25 kama mkuu wa nchi, anatafuta kipindi kingine cha miaka saba madarakani. Pamoja...

Afrika: Wanablogu wamwombolezea Michael Jackson

Barani Afrika, wanablogu wanatoa heshima zao za mwisho kwa Michael Jackson baada ya kifo chake hivi karibuni kwa kutuma picha, video za muziki, mashairi pamoja na tafakari. “Pumzika Kwa Amani” anaandika Mwanablogu wa Kenya WildeYearnings. “Sasa unalo anga zima kucheza kwa madaha kwa staili ya kutembea mwezini…”

Afrika Kusini: Kuvuvuzela au Kutovuvuzela?

Mjadala kuhusu kifaa maarufu kinachoitwa vuvuzela kinachopigwa na mashabiki wa mpira wa miguu Afrika Kusini umetawala katika blogu mbalimbali duniani tangu kuanza kwa Kombe la Mabara la mwaka huu nchini Afrika Kusini, lililohitimika wiki iliyopita. Waandishi wa habari, watazamaji wa televisheni, makocha na baadhi ya wachezaji wa kigeni walitoa wito wa kusitisha matumizi ya kifaa hiki katika Kombe la Dunia la 2010 nchini Afrika Kusini. Mabishano haya yana sauti kubwa kama chombo chenyewe.