Afrika: Ujio wa Mkonga wa Seacom Wazua Mjadala

Ujio wa mkonga unaopita chini ya bahari utakao ongeza uwezo na kupunguza gharama za intaneti barani Afrika umewasha majadiliano na mvuto katika ulimwengu wa blogu wa Afrika. Seacom, ambayo inaunganisha Afrika Kusini, Tanzania, Kenya, Uganda na Msumbiji na Ulaya pamoja na Asia, ilianza kutumika moja kwa moja Alhamisi, kwa kuziunganisha nchi za Afrika ya mashariki na Afrika ya kusini kwenye mtandao wa dunia wenye wigo mpana.

Seacom inaunganisha mwambao wa Afrika ya mashariki na Ulaya pamoja na Asia

Seacom inaunganisha mwambao wa Afrika ya mashariki na Ulaya pamoja na Asia

Miji ya Johannesburg, Nairobi na Kampala iliunganishwa Alhamisi, na Addis Ababa pamoja na Kigali inatarijia kufuata. Ujio wa mkonga huo ulipangwa kufikav mnamo mwanzoni mwa mwezi wa saba, lakini mashumbulizi ya maharamia nje kidogo ya pwani ya Somalia yalichelewesha utekelezaji.

Kiunganishi hiki cha chini ya bahari kinatarajiwa kupunguza gharama za upana wa masafa kwa asilimia 90 na kuongeza uwezo wa makongamano yanayotumia video, urushaji wa matangazo ya televisheni yenye picha za hali juu pamoja na huduma za intaneti zenye mwendo wa kasi kwenye mwambao wa Afrika ya mashariki.

“Mmmh… nasuburi kwa hamu kuanza upakuzi,” anaandika IT blog Kenya.

Huko Uganda, Josh kutoka blogu ya In African Minute ameshaanza kubaini tofauti:

Mbinu inayojulikana ili kuangalia video za YouTube barani Afrika ni kwa kubonyeza alama ya kugandisha video wakati inapoanza, subiri kwa dakika 20 (au zaidi) mpaka hapo video itakapopakuliwa yote, halafu angalia. Leo nipo kwenye sherehe ya kuzindua SEACOM… kwenye kona ya chumba cha kongamano, Peter Mereton Meneja wa ununuzi wa SEACOM, alinipa ishara niionyeshe tarakilishi yenye ukurasa wa YouTube uliokuwa tayari. Tuliizindua Kung Fu Baby na kwa mara ya kwanza katika Afrika, niliona video ya YouTube ikipakuliwa yote na kuchezwa katika sekunde 6.

Munashe wa TechMasai naye anafurahia:

Mkonga wa chini ya bahari wa Seacom tuliouandika kitambo kidogo nyuma umetimia na umeanza kufanya kazi leo. Ni mchakato wa kimapinduzi kutokana na ukweli kwamba nchi ambazo zitautumia hivi sasa, ambazo zinajumuisha kenye, Uganda, Msumbiji, Afrika Kusini na Uganda.

… Ni wakati mzuri kwa Afrika, Ninaweza kudhibitisha hilo kwa Kenya ambayo mpaka hivi sasa ilitegemea setilaiti kwa ajili ya mahitaji yake ya intaneti.

Jeremy, mwanablogu wa Kinaijeria anayeandika katika NaijaBlog, analinganisha Seacom na mikongo mbalimbali ya Afrika magharibi. Afrika Magharibi bado ipo chini:

Afrika ya Mashariki imekwenda na huduma ya masafa mapana ya intaneti… wakati Afrika ya Magharibi bado ipo kwenye sehemu ya kuanzia mbio (kwa kweli, bado ipo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ikijiuliza ni nini cha kuvaa) wakiwa na SAT3 isiyo na manufaa ambayo hukatika-katika, pamoja na Glo1 9je wakandarasi wa Alcatel wamekwama chini ya mabiwi ya mchanga?) na wakandarasi wengine wawili wapya, WACS na Main1 bado wakiwa mbali zaidi ya upeo (mwaka kesho kama tukiwa na bahati). Afrika ya mashariki imekumbatia huduma ya masafa mapana ya intaneti na kushika mbio wakati Afrika ya Magharibi inasuasua na kukodoa macho.

Twita nayo inanguruma na habari za Seacom. Baadhi ya watumniaji wana shauku, wakati wengine wana mashaka:

“Bado sijaweza kuamini kuwa unaweza kupakua mtandao wote wa Intaneti kupitia mkongo mmoja mdogo wa manjano #seacom
ncallegari

“Seacom ilizinduliwa_kwa hakika_leo. Na tuangalie itachukua muda gani kwa mawakala wa intaneti kuongeza kasi na kupunguza gharama…”
dnyaga

‘je ni mimi au ni huduma za intaneti katika Nairobi ambazo zimezorota leo tangu #seacom ilipozinduliwa? Pengine uwezo wa mkubwa wa inteneti unaburudika na mandhari ya bahari kabla ya kutufikia”
mentalacrobatic

Mengi ya mashaka juu ya Seacom yapo kwenye suala la bei: japokuwa baadhi ya wataalamu wa mambo wanadai kuwa gharama za upana wa masafa zitashuka kwa asilimia 90, wengine wanaamini kwamba makato ya gharama yanaweza yakawa madogo zaidi. Kachwanya anaandika:

Katika dunia sawa gharama zinapaswa zishuke kwa zaidi ya asilimia 90, hivi sasa inawagharimu mawakala wa kutoa intaneti dola 6500 za Kimarekani (takriban Shilingi 487500 za Kenya) kwa kila kipimo cha Megabiti za upana wa masafa, lakini shika pumzi yako, usitarajie miujiza katika hili. Hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa UUnet Tom Omariba alidai kuwa mikonga itashusha gharama kwa asilimia 20-30.

Mwanablogu TrueKenyan guswa na suala la uwazi:

Seacom wamekataa katu kutuwekea wazi, sisi walaji wa intaneti, ni mawakala gani wa kusambaza intaneti walionunua upana wa masafa kutoka kwao. Hivyo bado tupo kizani na hatufahamu ni wapi tunapoweza kununua huduma ya intaneti yenye uhakika na kwa bei nafuu… kwa hiyo jambo pekee ninaloweza kufanya ni kuendelea na wakala wangu wa intaneti huku nikiitazama mashine wakati ikipakua kurasa kwa kasi inayoamua yenyewe huku nikiwaza kuwa siku moja ndoto yetu itatimia.

Akitoa maoni katika blogu ya Mtanania Issa Michuzi [SW}, mdau pia anahofu juu ya gharama, japokuwa ana matumaini makubwa ya baadaye:

Asanteni sana kwa huo mkonga. Sasa kutandaza fibre-optic cables kwenye miji mbalimbali tunaanza lini? Manake kuwa na inter-country connection wakati within the country hatuna connection nzuri bado gharama zitakuwa juu na kwa maoni yangu tutakuwa tuna-under utilise capacity ya hiyo under sea cable. For the moment, well done! For the future, we have to work had!

Kwa Jellyfish, ambaye anayatupilia mbali masuala ya gharama kwa kusema kuwa ongezeko la kasi la kiasi hicho na kiwango cha huduma mkwa kawaida huenda sambamba na ongezeko la bei, ujio wa Seacom ni jambo zuri:

Katika tukio lililoratibiwa na kutangzwa sana SEACOM iliwasha funguo ambayo mara moja ilieneza Terabiti za upana wa masafa katika kasi ya mwanga kupitia nyuzi za vioo zilizotengenezwa na kupigwa msasa katika kiwango cha hali juu.

Na kwa mwanablogu wa Afrika Kusini Aki Anastasiou, “Hii ni MB ndogo kwa talakilishi yangu ya mapajani, TB moja kubwa kwa Afrika.”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.