Habari kuhusu Habari Kuu kutoka Aprili, 2014
Ni “Udhaifu” wa Serikali, Yasema Ripoti ya Ajali ya Kivuko cha Korea Kusini
Zimetimu siku 14 tangu kivuko cha Sewol kizame na watu 205 wamethibitika kupoteza maisha. Wanasiasa wanatumia tukio hilo na habari zisizosahihi za vyombo vya habari kuchochea hasira miongoni mwa Wakorea Kusini.
Win Tin: Mfungwa wa Kisiasa wa Myanmar Aliyefungwa kwa Muda Mrefu Zaidi Afariki Dunia
Mwandishi wa habari na mwanaharakati Win Tin ni mmoja wa viongozi wa harakati za kutetea demokrasia.
Nukuu 8 za Kushangaza Zilizopata Kutolewa na Wanasiasa wa Malaysia
Balik Cina ni tovuti mpya ya habari inayokusanya nukuu za kuchekesha na za ajabu zinazotolewa na wanasiasa wa Malaysia.
Watu 28 Wafariki, 268 Bado Hawajulikani Walipo Baada ya Feri ya Korea Kusini Kuzama
Feri ya Korea Kusini iliyokuwa ikielekea kwenye kisiwa cha mapumziko ilizama ikiwa na mamia ya abiria. Mwongoza mferi hiyo na wafanyakazi wa feri hiyo waliokolewa kwanza, kabla ya abiria wengi kupata msaada
Chanzo cha Maji nchini China Chawekwa Kemikali Inayosababisha Kansa
Benzene, kemikali inayosababisha kansa kwa haraka kabisa, imegundulika kuwepo kwenye chanzo cha maji cha Jiji la Lanzhou , wakati fulani ilipimwa na kukutwa kwa kiwango cha mara 20 zaidi ya kile kinachofahamika kuwa ni salama kwa matumizi.
Mazungumzo ya GV: Nini Kimewakuta Wanablogu wa Iran?
Huenda kublogu hakujafa, lakini kuko mbioni? Arash Kamangir na Laurent Giacobino wanatuletea utafiti wa kina kuhusu hali ya blogu mashariki ya kati.
Mazungumzo ya GV: “Mtandao wa Twita” wa Siri wa Kimarekani Nchini Cuba
Mpango wa siri wa Marekani wa kubadili utawala nchini Cuba wenye huduma ya ujumbe inayofanana na Twita iitwayo ZunZuneo sasa unaangaliwa kwa mashaka baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa maelfu ya wa-Cuba walidanganyika kujisajili kupata huduma hizo. Je, kutakuwa na madhara kwa wanaharakati wa kidijitali duniani kote? Wengine wana mashaka...