· Januari, 2012

Habari kuhusu Habari Kuu kutoka Januari, 2012

Makala za Global Voices Zilizosomwa Zaidi mwaka 2011

Global Voices haijabaki kuwa sauti pweke ya vyombo vya habari vya kiraia linapokuja suala la twita zinazotuma taarifa na posti za kwenye blogu. Bado, hata hivyo pale ambapo shauku kwa vyombo vikuu vya habari ikindelea kupungua, sisi ndio tunaojibidiisha kuendelea kuweka kumbukumbu ya kile ambacho wanablogu wadogo popote pale waliko wanahitaji dunia ikifahamu. Fahamu orodha ya makala zetu 20 zilizosomwa zaidi kwa mwaka 2011

Venezuela: Mwanaharakati wa mtandaoni Luis Carlos Díaz anyanyaswa na kutishwa na “wezi wa akaunti za mtandaoni”

GV Utetezi  25 Januari 2012

Kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha miezi minne tu, mwandishi wa habari wa Venezuela na mwanaharakati, Luis Luis Carlos Díaz, amenyanyaswa kupitia akaunti yake ya Twita [1] na simu yake ya mkononi na kikundi kinachojulikana kama cha "wezi wa akaunti za mtandaoni", na ambao hutumia jina la N33 [2], na bila shaka ni kundi lilelile la watu ambao miezi michache iliyopita liliiba maneno ya siri ya akaunti za Twita na baruapepe ya karibu watu thelathini maarufu wa Venezuela, baadhi yao ni waandishi wa habari Sebastiana Barráez, Ibéyise Pacheco, mchekeshaji wa kisiasa Laureano Márquez, mwanaharakati Rocío San Miguel na mwandishi Leonardo Padrón, miongoni mwa wengine wengi.