Habari kuhusu Habari Kuu kutoka Septemba, 2014
Waandamanaji Wanaodai Demokrasia Wageuza Hong Kong Kuwa Bahari ya Miamvuli
Yakiwa yamepewa jina la utani la "mapinduzi ya miamvuli" na baadhi ya vyombo vya habari, maandamano ya Hong Kong yatawaliwa na waandamanaji wanaojikinga na mabomu ya kutoa machozi kwa kutumia miamvuli.
Video ya Kuonesha namna Mlima Ontake Ulivyolipuka
Mtu mmoja amethibitika kufa, wakati wengine wapatao hamsini wakiwa wamejeruhiwa vibaya, na wengine kumi hawajulikani walipo baada ya Mlima Ontake, ulio maarufu kwa ukweaji mlima, katikati ya Japani, kulipuka
Kimbia! Waislamu Wanakuja!
Mtazamo wa vyombo vikuu vya habari mara nyingi unaonesha “Waislamu” wenye sura moja kubwa, ambayo haikosi kuwa na ghasia. Kwenye kichekesho hiki kisicho na maana yoyote, Mchekeshaji wa ki-Pakistani Sami Shah anakuletea makundi makuu ya “waislamu”.
Video Ioneshayo Mtoto Akiokolewa Kutoka Kwenye Kifusi cha Jengo Lililolipuliwa kwa Bomu Nchini Syria
Bomu lililaharibu makazi ya Ghina na kupelekea kifo cha mama yake. Aliweza kuokolewa akiwa hai pamoja na kufukiwa na kifusi akiwa peke yake.