· Januari, 2010

Habari kuhusu Habari Kuu kutoka Januari, 2010

Haiti: Ramani za Kwenye Mtandao Zaonyesha Uharibifu Pamoja na Jitihada za Kusambaza Misaada

  19 Januari 2010

Marc Herman anaziangalia kwa karibubaadhi ya ramani ambazo watoaji misaada wanazitumia ili kuwasilisha hali inayobadilika kila wakati katika maeneo ya tetemeko la ardhi nchini Haiti. Karibu ya juma moja baada ya janga kutokea - na matetemeko yaliyofuatia ambayo yalifanana na matetemeko mengine makuu – ramani na taswira za setilaiti zinajidhihirisha kuwa ni taarifa pekee ambazo zinaweza kutegemewa.

Haiti: Uenezaji Habari na Taarifa

  17 Januari 2010

Sisi tulio nje ya Haiti tunaweza tu kujenga picha kichwani kuhusu hali halisi ya maisha ya kila siku yalivyo huko baada ya tetemeko baya la ardhi - lakini katikati ya juhudi za kuwatafuta wapendwa ndugu, juhudi za kuwahudumia waliojeruhiwa na jukumu zito na gumu la kuwafikishia msaada wa kiutu wale wanaouhitaji zaidi - wanablogu walio huko Port-au-Prince na maeneo ya jirani wanawasiliana na ulimwengu wa nje, ambao nao unahangaika kutaka kupata taarifa kutoka kwa wale waliokuwa katika eneo lenyewe kabisa la janga.

Haiti: Madhira ya Tetemeko la Ardhi

  14 Januari 2010

Mpaka sasa taarifa za majeruhi wanaotokana na tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti zimejikita kwenye takwimu za kutisha, lakini ni majina machache tu ndiyo yameambatanishwa kwenye namba hizo. Katika makala hii tunapata simulizi za wale walionusurika kutoka kwenye janga hili la asili kama wanavyozirusha kwenye mtandao.

Baada Ya Tetemeko la Ardhi, Jumbe za Twita Kutoka kwa Walioshuhudia

  14 Januari 2010

Kutokana na janga la tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 ambalo limekikumba kisiwa cha Haiti jioni ya leo (Januari 12), “Haiti” ni mada kuu hivi sasa kwenye huduma ya Twita. Miongoni mwa lundo la jumbe zinazotumwa tena na tena za taarifa za habari kutoka za vyombo vya habari vikubwa na jumbe nyingine za twita zinazotuma sala au dua pamoja na salamu za heri kwa kisiwa hiki cha Karibea, pia kumekuwepo taarifa za mashahidi waliopo kwenye tukio kama vile mwanamuziki na mwendesha hoteli Richard Morse, ambaye anatwiti kwa jina la @RAMHaiti.

Misri: Mauaji ya Kinyama ya Naga Hammady

Wanablogu wa Misri wanaelezea kustuka kwao na hasira kwa kuuwawa kwa Wakristu wa dhehebu la Koptiki wakati wa mkesha wa sikukuu yao ya krismasi huko Naga hammady, katika Misri ya Juu. Mhalifu asiyejulikana alipiga risasi hovyo hovyo kwenye umati watu baada ya waumini kumaliza maombi na wakiwa wanaelekea majumbani kwao.