Bolivia: Mshindi wa Zamani wa Mashindano ya Urembo Atangazwa Kugombea Ugavana wa Jimbo la Beni

Kwa wengi, taarifa ya kuwa rais wa Bolivia Evo Morales angemtaja aliyekuwa mshindi wa urembo nchini Bolivia Jessica Jordan, 25 kuwa mgombea ugavana kwa tiketi ya Chama Cha Ujamaa (MAS) ilichukuliwa kama masihara ya Siku ya Wasio na Hatia ( ambayo ni sawa na Siku ya Wajinga Duniani nchini Bolivia). Hata hivyo tangazo hilo liliporasimishwa katika mkutano na wanahabari uliotangazwa moja kwa moja kwenye televisheni, watu waliitikia mara moja kwenye twita, kadhalika yakaandikwa maoni kuhusu maoni yaliyotolewa.

Picha ya Jessica Jordan iliyopigwa na Hugo Miranda na kutumika kwa ruksa maalum

Picha ya Jessica Jordan iliyopigwa na Hugo Miranda na kutumika kwa ruksa maalum

Maoni ya awali kwenye Twita yalikuwa ni ya kutoamini kwamba aliyekuwa mshindi wa urembo angependekezwa kushiriki uchaguzi katika ngazi ya juu namna hii. Diego Arrazola (@darrazola) aliandika:

ni pa concejal JESSICA JORDAN puej pa GOBERNADORA! q esta pasando? siguen en la jodita de los inocentes?

Si kwa uanachama wa manispaa JESSICA JORDAN, bali kwa UGAVANA! Je nini kinachotokea? Je bado ni siku ya Wasio na Hatia?

Mariela Castrillo (@ardilla_ilusa) aliandika:

Lo de Jessica Jordan es hilarante….no hay más gente en Beni? no hay más jóvenes con sueños? q pena…

Inachekesha hii habari ya Jessica Jordan… hakuna watu wengine huko Beni? Hakuna vijana wengine wenye ndoto? Aibu gani..

Kulikuwa na jumbe kama hizo za kutoamini, wengi waligusia ukweli kwamba Jordan alikuwa ni Mshindi wa Urembo wa Zamani nchini Bolivia. Hata hivyo wengine walifikiri kuwa haikuwa sawa kwa watu kung’aka katika namna hii. Patricia (@arquiteca) anapinga:

que les pasa? ven normal que un feo acceda al poder, pero cuando una bella candidatea, se rayan… machistas!

Mna matatizo gani nyie watu? Mnaona ni sawa kwa mtu mwenye sura mbaya kuchukua madaraka, lakini mgombea akiwa mzuri wa mwili, mnalalamika… huo ni mtazamo dume!

Jaime Duran wa blogu ya Economía Política, Desde el Lado Gracioso [es] anawakosoa wale ambao tayari wamekwishamuondoa akilini mgombea:

Están también los que olvidandose de sus posiciones de género han dicho muy sueltos de cuerpo que la niña será muy bella, pero que es poco probable que la cabeza le sirva para algo más que peinarse. Viendo la calidad de gobernadores que hasta ahora ha tenido el Beni, dudo mucho que se pueda criticar a la bella Jessica Jordan, por este tema. Por mi parte, estoy seguro que dictará cátedra en los temas en los que se ocupe, pues siempre he creido que belleza e inteligencia no son para nada incompatibles.

Kuna wale wanaosahau misimamo yao kuhusu usawa wa jinsia, wale wanaosema kuwa kwa kweli yule msichana ni mzuri, lakini haonekani kuwa kichwa chake kina manufaa yoyote zaidi ya kujitengeneza nywele zake. Nikiangalia viwango vya magavana ambao Beni imekwishawahi kuwa nao mpaka hivi sasa, sina hakika kama kuna mtu atakayeweza kumkosoa mrembo Jessica Jordan kwa hilo. Nina uhakika ataonyesha uwezo katika mambo anayoyakabili, Siku zote nimekuwa nikifikiri kuwa uzuri na akili haviendi pamoja.

Moja ya maswali makuu yanayozushwa na pendekezo hili ni “Ni nini watakachokipata MAS?” Beni ni Jimbo la Bolivia ambalo kiutamaduni limekuwa chini ya mikono ya upinzani. Kumuweka mtu anayejulikana taifa zima, ambaye hajawahi kuwa mwanachama wa chama au kushiriki katika siasa kunaongeza mvuto wa nchi nzima na kunaweza kugeuza mkondo katika eneo hilo. Hugo Miranda wa Angel Caido [es] anaongeza mawazo yake:

Y bueno esto merece un comentario, quizas resulte obvio que el MAS esta usando a figuras publicas de los departamentos donde aun no domina para tratar de ganar las Gobernaduras y Municipios, de esta forma tener el control total de todo Bolivia.

Quizas para algunos Jessica este siendo utilizada para estos fines del todopoderoso Evo Morales.

Pero queda la duda, y creo que Jessica se merece eso por que ella quiere mucho a Bolivia.

Ni vyema kutoa maoni juu ya suala hili, pengine ni wazi kuwa chama cha MAS kinawatumia watu maarufu katika majimbo ambayo haina utawala, ili kushinda viti vya Ugavana na Umeya, na kwa njia hii waweze kupata uwezo wa kutawala Bolivia yote.

Labda kwa baadhi, Jessica anatumiwa kwa ajili ya malengo hayo na yule mwenye nguvu zote, Evo Morales.

Mashaka bado yanabaki, na ninafikiri kuwa Jessica anastahili yote hayo kwa sababu anaipenda Bolivia sana.

Mkakati huu unaonekana kufanya kazi kwani baadhi ya wanablogu ambao hawajihusishi na siasa, au hata wale walio katrika upinzani dhidi ya chama cha MAS wanaanza kumuunga mkono Jordan. Japokuwa baadhi wanaweka wazi kuwa uungaji mkono ni kwa ajili ya mgombea, na si kwa chama cha siasa. Hata wale watu ambao hawana sifa za kupiga kura katika Jimbo hilo wanaelezea hamu yao ya kumsaidia mgombea. Kama mkakati huu utafanya kazi katika uchaguzi ulipangwa kufanyika Aprili 4, 2010, ni jambo linalosubiriwa.

Miranda ambaye hajawahi kuwa mshabiki wa chama cha MAS, anaandika kuwa mgombea mmoja ambaye atamuunga mkono ni Jordan hata kwa kuweka matangazo ya bure ya kampeni kwenye tovuti yake. Na Duran anamalizia:

Creo que la elección del Beni será la más interesante de todas las que presenciaremos en abril del 2010. Asimismo, desde esta palestra anuncio que estoy dispuesto a trasladarme a la bella tierra oriental para colaborar en tareas de campaña

Nafikiri uchaguzi kule Beni utakuwa ndio wa kuvutia zaidi kati ya chaguzi zote za Aprili. Na kwa kuongezea, kutoka katika jukwaa hili (blogu yake) Ninatangaza kuwa niko tayari kusafiri kwenda kwenye nchi ya kupendeza ya (Beni) kusaidia katika kampeni.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.