· Oktoba, 2008

Habari kuhusu Habari Kuu kutoka Oktoba, 2008

Chile: Mkutano wa McCain na Pinochet Mwaka 1985

  28 Oktoba 2008

Mwaka 1985, Mbunge wa bunge la Marekani aitwaye John Mccain alizuru nchini Chile na kukutana na mtawala wa kiimla Augusto Pinochet, akiwa na viongozi wengine wa serikali. Mkutano huo ambao haujawahi kuripotiwa hapo awali umewekwa wazi na mwandishi wa habari John Dinges, ambaye amechapisha habari hiyo kwenye blogu yake CIPHER [es], kadhalika katika blogu ya Huffington Post, ambako huwa anaandika masuala yanayomhusu John McCain "ambaye amekuwa akishutumu vikali dhana ya kuketi na watawala wa kiimla bila ya masharti yoyote, inaonekana kuwa alifanya jambo hilo hilo analolipinga.

Misri: Sisi sote ni Laila

  26 Oktoba 2008

Sisi sote ni Laila, ndivyo wanavyosikika kusema kwa sauti moja wanablogu wa kike wa Misri. Hivi, huyu Laila ni nani na kwa nini wasichana na wanawake wa kiMisri wanapenda kufananishwa naye? Hebu endelea kusoma ili uone ni kwa namna gani wanablogu wa Misri wanavyojihangaisha ili kuvunjilia mbali vikwazo vya jinsia na kufanya sauti zao zisikike.