Marekani ya Kusini:Taarifa,Twita kwa Waandishi wa Habari Yapata Umaarufu

Mafanikio ya huduma ya twitter (twita)yameweza kuleta mvuto mkubwa katika tovuti nyingi za habari,zinazotaka kuiga kanuni hii:taarifa fupi fupi, kutoka katika kila aina ya zana, kwa ajili ya kadamnasi fulani teule.Tovuti moja ambayo inafuata mfano huu ni Reporting on, aina ya Twita kwa wanahabari,ambayo umekuwa ikifanya kazi katika majaribio tangu mwaka jana. Kama ukijisajili utaona ni jinsi gani tovuti inavyofanikiwa miongoni mwa waandishi wa habari wa Kilatino.

Muundo au utaratibu wake ni sawa na ule wa Twita; tunaweza kuandika herufi zisizozidi 140, na watumiaji wengi wanautumia utaratibu huo ipasavyo kwa kuandika habari katika mtindo wa vichwa vya habari. Kila kipande cha habari kinaweza kuunganishwa katika maneno mengi. Katika upande kushoto tunaweza kupata viunganisho maarufu.Tunaweza kutoa maoni katika kila bandiko pia kujibu maoni hayo,lakini hatuwezi kumfuatilia mtumiaji au kuchuja habari isipokuwa katika viunganisho.

Pablo Mancini alifanya mahojiano na Ryan Sholin ambaye yupo nyuma ya mradi huu, anabainisha kuwa Reporting On “ni mradi usiolenga katika faida unaofadhiliwa na Knight News Challenge ili kuimarisha habari za ndani, kuunganisha watu ambao huwa hawasemezani vya kutosha na wengine”. Anaongeza zaidi kuwa: “pindi tovuti ikianza kufanya kazi na kwa kutumia idadi nzuri ya zana au miundo, nitaufanya msimbo kuwa wa wazi kwa kila mtu na kuwakaribisha waendelezaji na waandishi wa habari kuuimarisha ili waweze kutengeneza matoleo yao ya tovuti hii.

Pia kuongelea kuhusu Reporting on:Block de periodista(kihispania);The Exploding News room;Random Mumblings; na Linchepen At Digidaye unaweza kupata mahojiano mengine kwa Sholin

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.