· Disemba, 2012

Habari kuhusu Habari Kuu kutoka Disemba, 2012

Habari za Upotoshaji Kuhusu Afrika Katika Vyombo vya Habari vya Kimataifa

 Kampeni ya kumkamata #Kony2012 ilibeba mambo yaliyorahisishwa mno kuhusu Afrika. Vyombo vya habari vya Afrika vyenyewe, hata hivyo, kwa sasa havina kinga dhidi ya ukosoaji wa aina hii. Hapa ni muhtasari wa watu maarufu, makosa na kutokuwepo umakini katika habari zinazopewa nafasi katika vyombo vya habari vya dunia kuhusu Afrika na katika vyombo vya habari vya Afrika vyenyewe

Mwandishi wa Guinea Atoweka Kiajabu nchini Angola

Yuko wapi Milocas Pereira? Swali hili linarudiwa rudiwa kupitia blogu mbalimbali kwa majuma kadhaa sasa, lakini majibu yamekuwa vigumu kupatikana. Katika mitandao ya kijamii harakati zililipuka kuzishinikiza mamlaka za nchi ya Guinea kuchunguza mazingira ya kupotea kwa mwandishi huyo na mhadhiri wa Chuo Kikuu miezi sita liyopita katika jiji la Luanda, alikokuwa akiishi tangu mwaka 2004.

Kupigia Kura Maajabu Saba ya Dunia barani Afrika

Shindano la kila mwaka limezinduliwa kwa ajili ya watu kupiga kura kuchagua maajabu saba yaliyo bora zaidi barani Afrika. Na tayari upigaji kura umeshaanza. Baadhi ya maajabu ya asili yaliondolewa katika orodha ya mwisho ya kupigiwa kura na hivyo baadhi ya wanablogu waliongeza mapendekezo yao katika blogu zao. Tazama baadhi ya picha hapa: