Walimu wa Mauritania Wavunja Ofisi ya Waziri wa Elimu

[Angalizo: Viunga vyote viko katika lugha ya Kiarabu]

Kikundi cha walimu wa shule za sekondari kilivunja na kuingia katika ofisi ya Waziri wa Elimu wakipinga kuhamishwa holela kwawalimu 120 kwenda kwenye shule nyingine. Walimu hao wamekuwa wakihamishwa kuwaadhibu wale wote walioshiriki katika mgomo wa mwaka uliopita kushinikiza kuboreshwa kwa mazingira ya kazi katika sekta ya elimu. Walimu walikichukulia kitendo hicho kama adhabu kufuatia hatua yao ya kugoma kudai haki zao na vilevile kupuuzwa kwa sheria za utumishi wa umma nchini Mauritania.

Kwa upande wake, Mohamed Ould Rabani, Katibu Mkuu wa baraza hru la walimu wa shule za sekondari, waliuponda uhamisho huo kama hatua ya hatari katika historia ya Mauratania na kuwaomba wenzake kutokutii amri ya Wizara. Katika mukhtadha huo huo, kikundi kingine cha walimu walihamishwa kiholela, walifanya maandamano mbele ya ofisi ya Waziri wa Elimu Ahmed Ould Bah, wakiupinga uamuzi huo na kudai kusitishwa mara moja hatua hiyo. Baadhi yao vile vile waliandamana mbele yamakazi ya rai huko Nouakchott na wakatishia kuacha kazi ikiwa uamuzi hautabatilika. Ikumbukwe kuwa wizara imewasimamishia mishahara ya mamia ya walimu baada ya wao kushiriki maandamano yaliyoandaliwa na baraza hilo.

Picha ya walimu wakiandamana iliyowekwa kwenye twita na

@mejdmr

Baraza la Taifa la Elimu ya Sekondari lilitoa tamko kulaani uhamisho holela:

قدمت وزارة الدولة الموريتانية للتهذيب الوطني الأسبوع الماضي على التحويل التعسفي لعشرات أساتذة التعليم الثانوي بسبب مشاركتهم في إضرابات مشروعة، وهو ما يعد انتهاكا خطيرا للحقوق النقابية، وخاصة الحق في الإضراب المكفول بموجب المادة 14 من الدستور ولاتفاقيات الدولية التي وقعتها بلادنا، مثل اتفاقية منظمة العمل الدولية رقم 87 المتعلقة بالحريات النقابية.

Wizata ya Elimu ya Mauritania imewahammisha kiholela makumi ya walimu wa sekondari kwa sababu ya ushiriki wao katika mgomo halali. hatua inayoonekana kuwa ni uvunjifu wa hatari wa haki za wanachama wa baraza hilo, hususani haki ya kuandamana, inayolindwa na ibara ya 14 ya katiba na pia inalindwa na mikataba ya kimataifa iliyotiwa saini na nchi yetu, kama Makubaliano ya Kimataifa ya Kazi namba 87, ambayo yanakuhusiana na haki za baraza.

Blogu ya Tiguend iliweka shuhuda za walimu walioathirika na uhamisho huo, zilizopewa jina “Hii ndiyo sababu kwa nini ninastahili kutimuliwa kazi” ambapo walizungumzia kukiukwa kwa haki kwa uamuzi huo:

منذ عشر سنوات وأنا أزاول مهنة التدريس في ولاية الترارزة، ولم أحصل طيلة تلك السنوات على تقويم سنوي أقل من 17 نقطة، وعملت مع مديرين مختلفين، ولم يعلق راتبي طيلة هذه الفترة إلا بسبب واحد وهو المشاركة في الإضراب، وليس لي سجل في الغياب ولا التهاون في أداء مهنتي ولله كل الحمد على التوفيق.. إلى أن جاء المدير الجهوي محمد السالك ولد الطالب وبتقرير منه شخصيا ولمدير إعدادية روصو رقم 1 الذي يخضع له ليمنحني درجة بائسة لا تتجاوز 6/20 وليزيد بي “سبحة الوشاية والنميمة” التي يعلقها منذ وصوله غير القانوني للإدارة، ثم ليجعل كل ذلك سببا في تحويلي تعسفيا ضمن 16 أستاذا في ولاية الترارزة لم يكن لهم من ذنب إلا أنهم أضربوا – والقانون يكفل ذلك والدستور يحميه – من أجل حياة كريمة وتعليم أكثر كرامة.

Nimekuwa nikifundisha kwa miaka 10 katika mkoa wa Trarza na sijawahi katika kipindi chote hicho kupata chini ya alama 17 [kati ya 20] katika Tathmini ninayofanyiwa. Nimefanya kazi na waratibu mbalimbali na mshahara wangu haujawahi kusimamishwa isipokuwa wakati huu kwa sababu ya kushiriki mgomo. Sina rekodi ya kukosa au kuzembea majukumu yangu na kila kitu kiko sawia, namshukuru Mungu, mpaka mratibu Mohamed Ould el Talib alikuja na kutuma ripoti kwa mratibu wa Rousou School ambaye ni mkubwa wake wa kazi, akimwomba anipe alama 6 kati ya 20 na kunituhumu kupiga umbeya na majungu, tabia ambayo amekuwa akijidai nayo tangu ameteuliwa kwa namna inayotia mashaka kuwa mtawala wa elimu. Haya yote ndiyo yamekuwa sababu ya mimi kuhamishwa kienyeji pamoja na wenzangu 16 hapa Trarza ambao kosa letu pekee ni kushiriki mgomo tukijua kabisa kuwa sheria zinailinda haki hii na katiba ya nchi nayo inatulinda kwa ajili ya maisha na elimu ya kuheshimika.

Tovuti ya Mauritan.net inasema kwamba uhamisho ni matokeo ya malalamiko, yakiwatuhumu walimu kwa “kulazimisha mgomo na kufanya siasa”:

قد جاء نقل الاساتذة بناء على تقارير المدرين الجهويين عن طريق الولاة، وكانت رسائل الولاة تتضمن أن هؤلاء الأساتذة “يحرضون على الإضراب، ويمارسون السياسة”.

Uhamisho wa walimu ulizingatia taarifa za waratibu elimu kupitia kwa Magavana na barua za Magavana zilieleza kwamba walimu hao walifanya siasa kwa kushiriki mgomo huo batili.

Dedda Cheikh Brahim anakosoa namna utawala wa Mauritania unavyoshughulikia maandamano hayo ya walimu:

@dedda04 في ديمقراطية العسكر الاحتجاجات لها عقوبتها والأساتذة يدفعونها الآن بطريق قانونية #موريتانيا

Katika demokrasia ya Kijeshi, maandamano huadhibiwa na walimu sasa wanalipa gharama ya kwa mujibu wa sheria

Anaongeza:

@dedda04 الأساتذة تم تحويلهم بعد أن قرروا المطالبة بحقوقهم. لك الله أيها الموريتاني

Walimu walihamishwa baada ya kuamua kudai haki zao. Mungu yupo ewe Mmauritania

Mwandishi Mohamed Ould Salem alimlaumu Waziri wa Elimu kwa kusababisha mzozo katika sekta ya elimu:

@medsa20 لا يتنفس ولد باهية الأكسجين العادي وإنما يعيش من صناعة الأزمات والظلم ولذلك قرر عقاب 108 من خيرة الأساتذة لأنهم شاركوا في إضرابات مرخصة

Ould Bah havuti hewa iliyozoeleka bali huishi kwa kuminya haki za watu na kutengeneza mizozo. Ndio maana aliamua kuwaadhibu walimu bora 108 kwa sababu tu walishiriki kwenye mgomo uliofuata sheria.

Anaongeza:

@medsa20 موعد جديد مع عام مأزوم في التعليم 108 أستاذ يرفضون التحويل العقابي ونقابات تعليمية تتعهد بإسقاطه، ووزير يبدع في صناعة الأزمات ومراكمة الفشل

Tarehe mpya imeingia kwenye historia kwa mgogoro katika sekta ya elimu ambapo walimu 108 wamegomea uhamisho wa adhabu na baraza la elimu likiahidi kufutilia mbali uamuzi huo pamoja na waziri huyu mbunifu katika kutengeneza matatizo na kulimbikiza makosa

Nasser Al Hachemi alitwiti:

@n_nasser56 إنه الإذلال والتعسف. قلبي معكم يا حَملة النور

Ni unyanyasaji na uimla. Moyo wangu uko nanyi enyi wabeba taa

Mwanaharakati Mejdi Ahmed pia alitia neno katika suala hili:

@mejdmr الأساتذة إعتصمو بالأمس في مباني وزارة التعليم لمطالبة السلطات بالعدول عن قرار تحويلهم والذي وصفوه بالجائر

Walimu waliandamana jana katika maeneo ya Wizara ya Elimu wakiiomba (Wizara) kubatilisha uamuzi wa kuwahamisha -uamuzi waliouchukulia kuwa haukuwa wa haki.

Al Cheikh Ould Horma alitwiti:

@Cheikh_Horma في #موريتانيا: الأساتذة يصرون على أدلجة الصراع مع الوزارة التي تصر بدورها على أدلجة مطالب الأساتذة !

Nchini Mauritania walimu wanasisitiza kuufanya mgogoro huu kuwa wa kiitikadi na waziri muhusika akijibu mapigo kwa kuyafanya madai yao kuwa ya kiitikadi

Alimalizia:
<

a href=”https://twitter.com/Cheikh_Horma/status/251075845123366914″ target=”_blank”>@Cheikh_Hormaالسنة الدراسية على الأبواب في #موريتانيا والمعركة تبدأ من جديد بين الوزارة والنقابات.. حرب بسوس !

Mwaka wa masomo unakaribia kuanza nchini Mauritania na vita ndio kwanza vimeanza kwa mara nyingine baina ya Waziri na baraza la walimu. Ni vita hatari

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.