· Aprili, 2011

Habari kuhusu Habari Kuu kutoka Aprili, 2011

Misri: Mubarak awekwa Kizuizini

Miezi michache tu iliyopita, raia wengi wa Misri walitamani sana kumwona aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Rais Mubarak, akitupwa jela, hata hivyo, pengine ni wachache miongoni mwao waliofikiri kwa uhakika kabisa kwamba siku moja jambo hili lingetimia. Hata hivyo, mnamo Jumatano ya tarehe 13 Aprili, 2011, raia wa Misri waliamka na mapema asubuhi ya siku hiyohiyo kukutana na habari zinazohusu Mubaraka kutupwa kizuizini. Hapa chini tunawaletea jinsi habari hizi zilivyopokelewa katika ulimwengu wa uandishi wa habari wa Kijmii miongoni mwa Wamisri.

Côte d'Ivoire: Kuanguka kwa Laurent Gbagbo

Laurent Gbagbo alikamatwa katika makazi yake ya Cocody, pamoja na mkewe, Simone, na msafara wa watu wa karibu. Miezi mitano baada ya kukataa kukabidhi madaraka kwa rais anayetambuliwa kimataifa kama rais mpya wa Côte d'Ivoire, Alassane Ouattara, mgogoro nchini humo hivi sasa unaelekea kufikia hitimisho.Mtiririko wa matukio yaliyopelekea kukamatwa kwa Gbagbo yaliorodheshwa kwa kina kwa njia ya video za kwenye mtandao ambazo zilitolewa maoni kwenye mtandao.

Côte d'Ivoire: Gbagbo agoma, Waafrika waandamana

Wakati Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Rais Laurent Gbagbo akiwa bado amejichimbia ndani ya handaki nchini humo, akigoma kukamatwa kwa kuendelea kukataa kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2010, ushiriki wa Ufaransa katika harakati za kumng’oa zinasababisha miitikio miongoni mwa wanasiasa na raia wa Ufaransa, pamoja na jamii ya Waafrika waishio Ufaransa.

Côte d'Ivoire: Abijani kwenye masaa ya kudhoofu kwa utawala wa Gbagbo

Siku mbili zilizopita zimekuwa na utajiri katika misuguano na mivutano nchini Côte d'Ivoire. Vikosi vinavyomtii Ouattara, vilianza mashambulizi kuelekea Kusini na Magharibi mwa nchi hiyo. Katika siku zisizozidi tatu, walifanikiwa kuikamata miji ya Douékoué na kufika Yamoussoukro tarehe 30 Machi. Wa-Ivory wanatoa maoni yao kuhusu wafungwa kutoroka, kufungwa kwa televisheni ya taifa na sehemu aliyo Gbagbo:

Japan: Jijini Tokyo baada ya Tetemeko la Ardhi

  10 Aprili 2011

Makala hii ni sehemu ya habari maalumu za Tetemeko la Japani 2011. Siku ya Ijumaa, Machi 11, 2011 saa 8:46:23 mchana kwa saa za Japani, , tetemeko lenye kipimo cha 8.9 liliikumba Japan, hili ni tetemeko kuwahi kutokea katika historia iliyorekodiwa. (Wakati makala hii inaandikwa kwa mara ya kwanza ilikuwa)...