Habari kuhusu Habari Kuu kutoka Aprili, 2010
South Africa: Mauaji ya kiongozi wa Afrikaner Resistance Movement
Usiku wa Tarehe 3, Aprili 2010, kiongozi wa kundi la watetezi wa Waafrika Kusini wenye asili ya Udachi (Afrikaans Weerstandsbeweging (AWB), au Afrikaner Resistance Movement), Eugene Terre'Blanche, aliuawa. Je raia wa dijitali wana nini cha kusema kuhusu kifo chake na mustakabali wa mahusiano baina ya watu wa rangi tofauti nchini Afrika kusini?
Kirigistani: Mapinduzi “Yaliyowekwa kwenye Kumbukumbu”
Mnamo tarehe 6 April, nchi ya Kirigistani ilikumbwa na maandamano makubwa ya kupinga utawala ambayo hatimaye yaliing'oa serikali pamoja na kusababisha vifo vya watu wengi. Pamoja na kwamba intaneti haikushika usukani katika kuhamasisha maandamano hayo, imetumika sana katika kuhifadhi kumbukumbu za kina za maandamano hayo.
Brazili: Ulimwengu wa blogu waunga mkono sheria ya kuzuia ufisadi
Muswada wa sheria kwa ajili ya kuwazuia wanasiasa ambao wamewahi kutenda makosa makubwa ya jinai ili wasigombee nafasi za kuchaguliwa umeanza kuzua kizaazaa nchini Brazili huku karibu watu milioni 2 wakitia saini zao kama ishara ya kuunga mkono.
Indonesia: Sony yamkabili Sony
Sony AK wa Indonesia alitishiwa kushitakiwa kwa kukiuka sheria za matumiza ya nembo na shirika la Sony la Japan kama hatafunga tovuti yake binafsi yenye jina www.sony-ak.com. Suala hili lilizua mwitiko mkali katika jamii ya wanamtandao na kuilazimisha kampuni ya Sony kutupilia mbali shauri hilo.
Urusi: Habari za Mwanzo za Milipuko ya Mabomu
Utaratibu wa Jumatatu asubuhi mjini Moscow ulivunjwa leo na milipuko ya mabomu mawili mabomu ya kujiua, ambayo yaliua watu wapatao 38 na kujeruhi kwa uchache watu wapatao 70. Alexey Sidorenko anatafsiri baadhi ya taarifa za mwanzo kutoka katika ulimwengu blogu za Urusi.
Muziki Wenye Ujumbe – Video Mpya za Muziki Kutoka Tibet
Mradi wa kutafsiri Blogu uitwao High Peaks Pure Earth hivi karibuni umetupia jicho “muziki wenye ujumbe” kwa kutafsiri mashairi ya nyimbo za Tibet kutoka video za Muziki zilizowekwa kwenye mtandao. Tarehe 10 Machi mwaka huu , blogu hiyo iliweka video ya hip hop inayoitwa “New Generation” (“Kizazi kipya” kwa Kiswahili)...
Chile: Mchakato wa Ujenzi Mpya Baada ya Tetemeko la Ardhi
Mwezi mmoja baada ya tetemeko baya kabisa nchini Chile, Rais Sebastián Piñera ametangaza mpango wa ujenzi mpya wa miundombingu ya nchi na majengo, akiwataka raia wa Chile kutoa mapendekezo jinsi gani mchakato huo utekelezwe na kusimamiwa.