Kirigistani: Mapinduzi “Yaliyowekwa kwenye Kumbukumbu”

Mnamo tarehe 6 Aprili, nchi ya milima milima ya Kirigistani huko Asia ya Kati ilikumbwa na maandamano makubwa ya kupinga utawala [ENG] ambayo yaliishia kuing'oa serikali. Wakuu wa mikoa walikamatwa na waandamanaji, huku jeshi na polisi wakiamua kuunga mkono upande wa upinzani na kumwacha Rais Kurmanbek Bakiev akiwa karibu hana uungaji mkono kabisa.

Siyo kwamba maandamano hayo yalikosa umwagaji damu – la hasha – mpaka sasa tukio hilo la maandamano makubwa la hivi karibuni limeacha takribani watu 74 wakiwa wamekufa na zaidi ya 500 wakiwa majeruhi – hii ni tofauti na mapinduzi yaliyopita yaliyopachikwa jina la “Tulip Revolution” [ENG] ya mwaka 2005. Mapinduzi haya mawili hayafanani. Miaka mitano tu iliyopita, ilikuwa Bakiev aliyekwenda katika viwanja vya wazi vya Ala-Too katikati ya mji mkuu wa Kirigzi akidai kujiuzulu kwa aliyekuwa Rais wakati huo, Askar Akayev. Safari hii ni Bakiev mwenyewe aliyepaswa kutimua mbio katika jiji hilo katikati ya umati mkubwa ulioongozwa na kiongozi wa upinzani Roza Otunbaeva.

 Migawanyiko ya kiutadamaduni na kisiasa katika Kirigistani. Ramani kutoka Wikimedia.

Migawanyiko ya kiutadamaduni na kisiasa katika Kirigistani. Ramani kutoka Wikimedia.

Vyanzo vya mapinduzi ya sasa vipo kadhaa: mapambano kati ya Kusini na Kaskazini (Bakiev anatoka Kusini, wapinzani wanatoka Kaskazini), ufisadi na serikali inayogandamiza watu (katika miaka ya karibuni raia wa Kirigistani wameshuhudia kila aina ya ugandamizaji kutoka ule wa kufungiwa magazeti [ENG] hadi kuuwawa kwa waandishi wa habari wasioegemea upande wowote [ENG]), Mchezo mkubwa wenye maslahi kwa Urusi, Ortega-y-Gasset'ian “mapinduzi ya watu” n.k.). Pasipo kujali sababu za mapinduzi hayo ni zipi, mapinduzi ya watu wa Kirigistani ya 2010 kwa kuyachukulia kwa uzito wake yamekuja ghafla, yakiwa na nguvu ya ajabu, ya kumwaga damu na … yamehifadhiwa vema.

Dhima ya vyombo vipya vya habari safari hii ilibadilika kidogo kulinganisha na matukio yenye kushangaza (kama maandamano ya kupinga utawala ya Moldova au Irani). Blogu na Twita hazikutumika kama nyenzo kuu za kuhamasisha umma hasa kwa kuzingatia kwamba intaneti bado ni changa katika nchi ya Kirigistani (imefikia asilimia 15 tu mpaka mwaka 2009). Hata hivyo, vyombo hivyo vipya vya habari vilikuwa na nguvu ya kutosha kuchukua matukio yote muhimu na kutoa picha za video zilizo kamilifu tangu yalipoanza pale Talas, mlipuko wa watu kule Bishkek na matukio ya unyang'aji yaliyofuatia vurugu hizo. Wakati huo huo vyombo vipya vya habari vilitumika kwa ufanisi mkubwa na upande wa upinzani uliokuwa unajaribu kuvuta macho ya jumuiya ya kimataifa na kugeuza mwelekeo wa maoni ya umma kwa upande wa waandamanaji. Kiongozi wa upinzani, Roza Otunbaeva (@otunbaeva), kwa mfano, alifungua akaunti yake ya Twita mara tu bibie huyo aliposhika wadhifa wa kiongozi wa mpito wa serikali. Siku nyingine, mtoto wa Rais Bakiev, Maxim alifungua LiveJournal ili kupata sehemu ya kusemea maoni yanayoiunga mkono serikali.

Kama alivyohitimisha Asmolov [RUS], haikuwa “journalists 2.00 waliokuwa na ufanisi mkubwa katika kuchukua habari za matukio ya nchini Kirigistani bali walikuwa “editors 2.00. Wanablogu ambao kwanza wanaijua nchi na pili walikuwa nje ya nchi ili kuweza kuona vizuri zaidi matukio ya ndani ambapo walikusanya picha, video na taarifa zilizotumwa kwa Twita. Wanablogu wawili waliokuwa na taarifa za karibu kabisa walikuwa nje ya nchi: Yelena Skochilo anayeishi Marekani (akifahamika pia kama LJ user morrire) na Vyacheslav Firsov anayeishi Kazakistani (akifahamika pia kama lord_fame). Hawa wawili walifaulu kukusanya kikamilifu kabisa picha, video na hata nyakati.

“Washindi” wengine katika uchukuaji taarifa za matukio hayo ni blogu za ndani ya nchi kama vile namba.kz, kloop.kg, issyk-kulpress.kg (vilevile tovuti za habari za kawaida ama vile internews.kg, neweurasia.net na 24.kg), jukwaa la diesel.elcat.kg na kamera ya mtandaoni isiyotoa maneno (webcam) ikionyesha viwanja vya wazi vya Ala-Too (picha zake zilinaswa na kutumwa na wanablogu wengi). Hashi za Twita #freekg (ambayo ndiyo hashi kuu ya tukio zima) #bishkek, #kyrgyzstan na #talas, ingawa imejaa Twita zilizotumwa upya na uchokozi mwingi, vyote viliwezesha wafuatiliaji wanaozungumza lugha ya Kiingereza kufuatilia yale yaliyokuwa yakiendelea.

Licha ya matatizo ya nchi nzima ya Intaneti mnamo tarehe 6 na 7 Aprili (vikosi vya serikali vilizuia tovuti maarufu kama vile “Azattyk” (REFERL), 24.kg, ferghana.ru, LJ user sabinareingold alivyotaarifu), mapinduzi ya Kirigistani yametokea kuwa yenye kuwekwa katika kumbukumbu zaidi kulinganisha na mengine. Registan.net ikilinganisha matukio ya mauaji ya Andijani, aliandika:

Taarifa zinazotoka Kirigistani huwa si za kutegemewa sana. Mara nyingi ni za kuelemea upande mmoja, zenye mtazamo finyu, zinazochanganya na zinazojipinga. Lakini bado zinatupa picha ya Kirigistani inayohitaji tuitazame vema – siyo sasa tu, lakini katika miezi na miaka inayokuja, huku tukizama nyuma katika matukio ya sasa hivi na kuunganisha vipande vipande ili kupata picha kamili ya ya kile hasa kilichotokea.

Kwa kuwa kumekuwa na taarifa nyingi mno, kwa hiyo iliandaliwa orodha iliyopangiliwa vema ya matukio na mambo yaliyokusanywa na kuchapishwa na wanablogu.

Tarehe 6 Aprili, Talas

Mapinduzi yalianza tarehe 6 Aprili huko Talas, kaskazini-magharibi mwa Kirigistani, ambapo wenyeji wa huko walivamia jengo la utawala la eneo hilo. Jambo hilo pia lilitokea Naryn saa mbili kabla ya hili. Siku iliyofuata, karibu makao makuu ya mikoa yote isipokuwa Bishkek huko Kaskazini mwa Kirigistani yalikuwa yakishikiliwa na upande wa upinzani.

  • Picha za uvamizi wa Jengo la Utawala la Jiji la Talas, Talasmost.kg

  • Picha za baada ya uvamizi wa Jengo la Utawala la Jiji la Talas, NewEurasia.net

    Tarehe 7 Aprili, Vurugu za Bishkek
    Matukio muhimu zaidi yalitokea tarehe 7 Aprili huko Bishkek. Mkutano wa upande wa upinzani uligeuka kuwa mgogoro wa wazi. Mara baada ya waandamanaji (ambao kwa namna moja au nyingine walijipatia silaha) walipoanza kuvamia makazi ya Rais baada ya kuvishinda vikosi vya polisi, walinzi wa Rais walianza kuwatupia risasi ili kujaribu kuwadhibiti. Mashuhuda walisema kwamba vitendo hivyo vilisababisha walau kuuwawa kwa watu 20 (wengine waliuwawa kwa mabomu ya kutupa kwa mkono na risasi za moto).

  • Picha za mapambano dhid ya polisi, 24.kg
  • Uvamizi wa makazi ya Rais, Internews Exchange
  • Seti kamili ya video kuonyesha vurugu za huko Bishkek, namba.kz
  • Unyang'anji katika nyumba ya Bakiev, sabinareingold
  • Seti ya picha za mapambano dhidi ya polisi, lord_fame
  • Picha za milipuko katika viwanja vya wazi vya Ala-Too, , abstract2001
  • Seti ya picha kutoka viwanja vya Ala-Too, , abstract2001
  • Picha za video za uvamizi:

    Picha nyingine ya video:

    Polisi walishindwa kuwadhibiti waandamanaji na hivyo walikimbia kuliacha jengo. Rais Bakiev alikimbilia kusikojulikana kwa kutumia ndegeyake. Mnamo tarehe 8 Aprili, kulikuwa na taarifa kwamba alikuwa amekimbilia huko Osh (Kusini mwa nchi), na kwenda katika kijiji alikozaliwa karibu na Jalalabad. Alikataa kuachia madaraka. Mkoa wa Osh ni moja kati ya mikoa ambayo bado haiko chini ya upande wa upinzani mpaka sasa. Bado haijulikani Bakiev atapatwa na nini.

    Tarehe 8 Aprili, baada ya Mapinduzi

    Baada ya vikosi vya upinzani kuwa na udhibiti kamili wa Bishkek, walikabiliana na hatari nyingine kubwa zaidi, yaani, unyang'anyi. Wanablogu kadhaa walitoa taarifa za kuwepo kwa wanyang'anyi wengi sana (mara nyingine wakiwa wamebeba silaha). Ilipofika jioni, wanyang'anyi walizuiliwa kuendelea na vitendo vyao na jeshi jipya la polisi na walinzi wa kujitolea ambao walikuwa wamejifunga beji nyeupe mkononi. Ujumbe wa mwisho kutoka kwenye blogu ulisema kwamba hali huko Bishkek ilikuwa tayari imetengemaa.

  • Picha ya watu karibu na makazi ya Rais,, Jamila Kulova
  • Set za Flickr zenye picha za mitaa ya Bishkek, Yelena Skochilo
  • Madirisha ya maduka yaliyovunjwa huko Bishkek , Vyacheslav Firsov
  • Picha za Bishkek, Valery Georgiadi
  • Anza mazungumzo

    Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

    Miongozo

    • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.