Brazili: Ulimwengu wa blogu waunga mkono sheria ya kuzuia ufisadi

Wakati ambapo makala haya yanakwenda mitamboni, karibu watu 1,735,000 walikwishatia saini kuunga mkono muswada wa sheria inayojulikana kama Ficha Limpa (yaani Mtu Safi au Mtu Asiye na Rekodi ya Uhalifu), na sheria hiyo inakusudia kuwazuia wanasiasa ambao wametenda makosa makubwa ya jinai kama vile matumizi mabaya ya fedha za umma, ufisadi, mauaji na kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya ili kwamba wasipate fursa ya kugombea nafasi yoyote ya kuchaguliwa.

Pengine itakuwa vigumu kwa mtu wa kutoka taifa lingine kuelewa kwa nini ni muhimu kuwekea sheria jambo la namna hii, hasa kwa kuzingatia kwamba kuna idadi kubwa tu ya wanasiasa wenye rekodi za uhalifu na walio madarakani. Kwa mfano, Makamu wa Kongresi, Paulo Maluf, ambaye hivi karibuni jina lake limetokea katika orodha ya watu wanaotafutwa na Polisi wa Kimataifa (Interpol), kwa ajili ya kula njama na kutumia vibaya fedha za umma. (Malufar ni neno lililobuniwa na raia wa Brazili kumaanisha kitendo cha “kuiba fedha za umma”.)

Lengo la kampeni hiyo, ambayo katika majuma ya karibuni ilijumuisha Avaaz.org, ilikuwa kupata sahihi zipatazo milioni 2 kabla ya tarehe 7 Aprili, yaani katika siku ambapo mradi huo hauna budi kutolewa uamuzi katika Chemba cha Wasaidizi. Kama jambo hili litapitishwa katika Chemba hiyo basi muswada utapelekwa katika Seneti.

Huku ikiwa na kauli mbiu inayosema “Kura haina bei, ila inaweza kuleta mabadiliko”, Kampeni ya Ficha Limpa ilizinduliwa mwezi Aprili mwaka 2008 na Movimento de Combate à Corrupção Eleitoral [Vuguvugu la Kupinga Ufisadi katika Chaguzi, pt] kwa lengo la kupata wagombea nafasi za kuchaguliwa wengi walio na rekodi safi:

Para isso, foi elaborado um Projeto de Lei de iniciativa popular sobre a vida pregressa dos candidatos que pretende tornar mais rígidos os critérios de inelegibilidades, ou seja, de quem não pode se candidatar.
Pessoas condenadas em primeira ou única instância ou por meio de denúncia recebida em tribunal – no caso de políticos com foro privilegiado – em virtude de crimes graves como: racismo, homicídio, estupro, tráfico de drogas e desvio de verbas públicas. Essas pessoas devem ser preventivamente afastadas das eleições ate que resolvam seus problemas com a Justiça Criminal;

Ili kufanya hivi, tuliandaa muswada wa sheria kwa kutumia maoni ya walio wengi kuhusu rekodi zilizoptia za wagombea nafasi za kuchaguliwa mbalimbali ili kukaza zaidi kuhusu vigezo vya kustahili kuchaguliwa, yaani, ili kuwachuja wale wasiostahili kugombea nafasi katika chaguzi:
Watu ambao wamewahi kushtakiwa mara moja au hata kwa malalamiko fulani mahakamani (hasa kwa wanasiasa wenye wadhifa maalumu) kwa ajili ya makosa makubwa ya jinai kama vile ubaguzi wa rangi, mauaji, kubaka, kusafirisha dawa za kulevya na matumizi mabaya ya fedha za umma. Watu wa aina hiyo hawana budi kuzuiwa kabisa kushiriki kwenye chaguzi ili kwamba washughulikiwe katika namna ya kutafuta haki kwa mkondo wa mahakama.
Moja ya mabango mengi ambayo yamepata umaarufu katika ulimwengu wa blogu.

Moja ya mabango mengi ambayo yamepata umaarufu katika ulimwengu wa blogu.

Ukiachia mbali saini milioni 1.6 zilizokusanywa katika ngazi ya watu wa kawaida na wanaharakati na makundi ya makanisa, mradi huo ulivutia hisia za ulimwengu wa blogu kwa kiasi kikubwa. Mwezi Oktoba mwaka jana, Arthurius Maximus [pt] alichapisha bango hilo hapo juu akiwaasa wasomaji kushiriki katika kampeni hiyo akisema kwamba wakati ulikuwa umefika wa kusahau tofauti zote za kiitikadi na kuwasukuma Wabunge kupitisha muswada huo wa sheria:

Esqueça […] as ofensas costumeiras do embate ideológico. Esqueça a Copa do Mundo, as Olimpíadas ou o BBB. Esqueça que seu time pode ser campeão ou ser rebaixado. Esqueça que seu professor é um chato ou que seu aluno não quer nada com estudo. Esqueça que seu chefe não te valoriza ou o empregado preguiçoso. Esqueça tudo… menos das vezes em que você se sentiu humilhado e traído ao ver um homicida, um traficante ou um corrupto notório e condenado em diversos processos (mas ainda “inocente até que se prove ao contrário”, em processos que se arrastam por décadas, levados por advogados espertalhões e pagos com o seu dinheiro suado, devidamente roubado dos cofres públicos).

Chegou a hora do “bom combate”. Chegou a hora de esquecer as diferenças ideológicas e de primar por uma nova era na política nacional. […]
Como é de se esperar (no Congresso Nacional, mais de um terço dos congressistas ficariam inelegíveis imediatamente caso o projeto fosse aprovado), os políticos se articulam para barrar, modificar ou tornar inócuo o projeto.

Tusahau […] midahalo tuliyoizoea ya itikadi za kutukanana. Tusahau kuhusu Kombe la Dunia, Olimpiki au hata Onyesho la Big Brother la hapa Brazili. Sahau kwamba timu unayoshabikia ya soka itakuwa mshindi au inaweza kutelemshwa daraja. Sahau kwamba mwalimu wako anatia uvivu kumsikiliza au kwamba wanafunzi wako hawaelekei kujali masomo yao. Sahau kwamba bosi wako hakujali au sahau kwamba wafanyakazi wako ni wavivu. Sahau kila kitu … isipokuwa nyakati zile ulipohisi kusalitiwa au kunyanyasika kwa kuona mwuaji, mfanyabiashara wa dawa za kulevya aliyekubuhu au hata mtu maarufu aliye fisadi,watu ambao wamewahi kukutwa na hatia za jinai mara kadhaa (lakini “wakiwa hawana hatia mpaka ithibitishwe vinginevyo” mara nyingine katika kesi ambazo zinaendeshwa kwa miongo kadha, huku wakitetewa na wanasheria washenzi na ambao wanalipwa na fedha ambazo wewe unazitolea jasho sana, ambazo zimeibwa kutoka kwa umma). Wakati wa “kupigania kilicho chema” umefika. Wakati wa kusahau tofauti za kiitikadi na kung'ara katika zama mpya za siasa za kitaifa. […] Kama mlivyotarajia(Katika Bunge la Wawakilishi, zaidi ya theluthi moja huenda wataonekana kukosa sifa endapo muswada huo utapitishwa), wanasiasa wanafanya kila juhudi ili kuuzuia, kuurekebisha au kufanya muswada huo usiwe kizuizi kwao.
Saini ya kumalizia mbali ufisadi. Bango ambalo limewekwa na Renato Hirata

Saini ya kumalizia mbali ufisadi. Bango ambalo limewekwa na Renato Hirata

PedroHutsch Balboni [pt], ambaye mara nyingi huwa haandiki makala za kisiasa kwenye blogu yake, hapa anakuja na mtazamo tofauti ili kushajiisha upigiaji debe wa yale yaliyo kwenye Avaaz hata kama kura pale sio za kweli:

É lógico que essa votação não é aberta ao público, para nós ficam causas muito importantes como o desarmamento ou não, enquanto a escolha de “se queremos políticos corruptos ou não” é feita somente por deputados (vejam só, são políticos!). Mas há também, no meio dessa sujeirada, bons deputados, que realmente estão interessados no futuro do país, e que são contrários a corrupção na política.

Bila shaka, watu hawataweza kupigia kura jambo hili, tumebakiwa na visababishi muhimu kama vile pendekezo la [2005] la kupiga marufuku bunduki, ambapo kuchagua “kama tunataka wanasiasa mafisadi au la” linakuwa jambo la kutolewa uamuzi na Wasaidizi/Wabunge (Je, unaweza kuamini jambo hili, wanasiasa!). Lakini katikati ya uchafu huu wapo wanasiasa safi, ambao kwa kweli wana nia njema kabisa na hatma ya nchi hii, ambao wanapiga vita ufisadi katika siasa.

Si kila mmoja anashabikia upitishaji wa muswada wa sheria wa Ficha Limpa. Fernandinho Brasileiro [pt] anafikiri kwamba mradi kama huo katika nchi kama Brazili unaonekana kama utani mbaya:

O MCCE tenta em vão aprovar esse projeto de lei que esbarra na própria constituição não desperta o menor interesse por parte dos políticos. Afinal de contas, o deputado do Castelo,o deputado que está se lixando para a opinião pública,os mensaleiros,os sanguessugas,estão totalmente contrários a esta lei,pois serão diretamente atingidos por ela. A lei ficha limpa não olha o sistema político e econômico que impera no país.

MCCE inajaribu pasipo kuwa na mafanikio kupitisha muswada huu ambao kwa kweli unagus katiba yenyewe na wala hauvuti mshawasha wowote miongoni mwa wanasiasa. Zaidi sana, Bwana “Msaidizi wa Kasri” [Soma habari inayojenga usuli], ambaye ni msaidizi/mbunge ambaye wala hajali maoni ya umma, wale ambao hupokea rushwa, wanyonyaji, wanapinga kabisa muswada huu wa sheria, kwani wataathiriwa moja kwa moja na sheria hiyo. Ficha Limpa haikuzingatia mfumo wa kisiasa na kiuchumi unaotawala nchi hii.

Wanablogu wengine wanajiuliza kuhusu uwezekano wa kufanya mradi kama huo ufanye kazi kikwelikweli. Ricardo RicBrSp [pt] anasema wazo si baya sana, lakini kwa kuwa haamini kwamba itafanya kazi sawasawa badala yake kuleta vurugu tu, basi anapendelea kupigia kampeni ya Kura isiyoangukia kokote:

Se isto vier a acontecer o Brasil todo vai ficar sem rumo, sem chefia, sem poder executivo, pois ele só consegue operar nas condições atuais, movido a corrupção.

Kama jambo hili litafanikiwa basi Brazili nzima itapoteza mwelekeo, hakutakuwa na uongozi, hakutakuwa na serikali, kwa sababu vyote hivyo vinawezekana katika mazingira tuliyo nayo sasa tu, mfumo unaoendeshwa na ufisadi.

Kusambaa kwa haraka katika mitandao ya kijamii (kama virusi)

Licha ya mitazamo hasi ya wengine, kadiri siku zinavyozidi kuyoyoma katika Chemba ya Wasaidizi, muswada huo ulileta sokomoko, ukizunguka huku na huko na hata kutokea mara nyingi tu katika Twita ukigota vichwa cha habari vya mada za Brazili. Twita zilizo nyingi zilipigia chapuo Avaaz, lakini Tico Santa Cruz alionyesha mgongano katika sheria za Brazili, ambazo zinawazuia watu wenye rekodi ya kuwa na makosa ya jinai hawaruhusiwi kugombea nafasi za utumishi wa umma:

@Ticostacruz: Ñ pode fazer concurso Público qm Ñ tem Ficha LIMPA então a lógica é a mesma p qm quer ser Polítco http://bit.ly/b2SVXu – ASSINE! Já assinei

@Ticostacruz: Wenye rekodi ya kuwa na makosa ya jinai hawaruhusiwi kuomba kazi kama watumishi wa umma, kwa hiyo mantiki hiyo inafanya kazi kwa wanasiasa pia http://bit.ly/b2SVXu – Iandikishe! Nina!

Hata hivyo, wengi hawadhani kwamba muswada huo utapitishwa kuwa sheria. @jrkbza ni mmoja wao[pt]:

@jrkbza: será que estão acreditando que essa Lei Ficha Limpa será aprovada pelos deputados? eu espero que sim, mas sei que não.

@jrkbza: je, kweli wanafikiria kwamba kampeni hii ya muswada wa Ficha Limpa itapitishwa na wasaidizi? Ningependa iwe hivyo, lakini sidhani kama watafanya jambo hilo.

Hata wabunge wenyewe hawana imani nao sana. Mbunge Chico Alencar [pt] anayeunga mkono mradi huo anauasa umma kwa kusema:

@depchicoalencar: ‘Ficha limpa’ esta semana na Câmara. Fiquem atento(a)s: vão tentar “aprimorar”(= tornar inócuo) o PL, ou adiar a votação…

@depchicoalencar: Wiki hii ‘Ficha limpa’ inaingia kwenye Chemba. Fuatilia: ama watajaribu “kuuongezea ubora” muswada huo wa sheria (=kuufanya uwapendelee) au wataahirisha upigaji kura …

Hata hivyo, kuwa na uungwaji mkono wa pande zote mbili, vyama vya mrengo wa kushoto na ule wa kulia kwa kiwango fulani, mradi huo bado unawapa watu matumaini, kama vile Adriana Christina [pt], anayeamini kwamba watu wanaweza kuleta mabadiliko katika mhimili wa madaraka kwa njia ya kura:

@adryanacristina: Vamos pressionar os deputados conseguindo 2 milhões d assinaturas p mostrar que se eles não votarem pela “Ficha Limpa” não votaremos neles!

@adryanacristina: Hebu tuwatie shinikizo hawa wasaidizi kwa kupata saini milioni 2 ili kuwaonyesha kwamba kama hawaungi mkono “Ficha LImpa” basi hatuwapigii kura!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.