Muziki Wenye Ujumbe – Video Mpya za Muziki Kutoka Tibet

Mradi wa kutafsiri Blogu uitwao High Peaks Pure Earth hivi karibuni umetupia jicho “muziki wenye ujumbe” kwa kutafsiri mashairi ya nyimbo za Tibet kutoka video za Muziki zilizowekwa kwenye mtandao.

Tarehe 10 Machi mwaka huu , blogu hiyo iliweka video ya hip hop inayoitwa “New Generation” (“Kizazi kipya” kwa Kiswahili) wa kundi maarufu liitwalo “Yudrug” kwa ki-Tibet (Mnyama wa kubuni aina ya “Dragon wa kijani” kwa Kiswahili). Yudrug waliiachia video yao katika blogu yao mwezi uliopita. Kwa mujibu wa High Peaks Pure Earth:

Aina hii mpya ya kujieleza kimuziki inayosikika katika “New Generation” imeleta mtafaruku katika mtandao wa wazi wa Tibet huku wanablogu wa Tibet wakiwasifu Yudrug kwa ujasiri wa mashairi yao lakini baadhi yao pia waliwakosoa Yudrug kwa kutumia mtindo ambao ni “wa Kimagharibi mno”. Bila kujali kionjo chako cha muziki, huwezi kukana kuwa wimbo huu una msukumo na nguvu ukiwa na kiitikio:

Kizazi kipya kina utajiri uitwao ujana
Kizazi kipya kinajivunia kitu kiitwacho kujiamini
Kizazi kipya kinamuonekano uitwao Burudani
Kizazi kipya kina majaribu yaitwayo uhuru

Ni kweli kuwa “New Generation” wa Yudrug ni dhihirisho la muibuko wa wanaharakati wa mtandaoni juu ya U-Tibet, kama ilivyoelezwa mapema katika makala ya blogu ya High Peaks Pure Earth. Muziki huo umejaa majivuno na kujiamini. Hapa pata video yenye tafsiri katika maandishi ya Kiingereza:

New Generation” wa Yudrug ( Dragon wa Kijani) kutoka HPeaks katika Vimeo

Ukiachana na Yudrug, High Peaks Pure Earth imemtambulisha pia mwimbaji chipukizi wa Tibet, Tashi Dhondup, kwa wasomaji wake. Tashi Dhondup anatokea katika eneo la Amdo katika tibet na kwa sasa anatumikia miezi 15 ya elimu rejea kwa kufanya kazi kutokana na “makosa” yanayohusiana na muziki wake. CD yake ya mwaka 2008 “Torture Without Trace” (mateso bila vielelezo) iliuzwa kwa maelfu ndani ya Tibet. Ifuatayo ni video ya miziki yake:



1958 – 2008″ wa Tashi Dhondup kutoka HPeaks katika Vimeo.

Unable To Meet” wa Tashi Dhondup kutoka HPeaks katika Vimeo.

“For That I Shed My Tears” by Tashi Dhondup kutoka HPeaks katika Vimeo.

Torture Without Trace” wa Tashi Dhondup kutoka HPeaks katika Vimeo.

No Regrets” wa Tashi Dhondup kutoka HPeaks katika Vimeo.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.