Habari kuhusu Habari Kuu kutoka Novemba, 2010
Myanmar: Hatimaye Suu Kyi Amekuwa Huru
Amekuwa kifungoni kwa miaka 15 katika miaka 21 iliyopita, lakini hivi sasa hatimaye yuko huru. Kiongozi wa upinzani na alama ya wapenda demokrasia nchini Burma, Aung San Suu Kyi aliachiwa huru kutoka kizuizini mchana siku ya Jumamosi na serikali inayoungwa mkono na jeshi la Myanmar
Mexico: Mwanamke wa Miaka 20 ni Mkuu Mpya wa Polisi katika Mji wa Kaskazini mwa Mexico
Valles García ni mwanamke aliyeolewa mwenye umri wa miaka 20 anayesoma masomo ya makosa ya jinai na uhalifu; vile vile ni mkuu mpya wa polisi wa Práxedis, Chihuahua, mji uliopo umbali wa kilometa 100 (maili 62) kutoka Ciudad Juárez, mji wenye uhalifu zaidi nchini Mexico.