Venezuela: Mwanaharakati wa mtandaoni Luis Carlos Díaz anyanyaswa na kutishwa na “wezi wa akaunti za mtandaoni”

Kwa mara ya pili ndani ya kipindi cha miezi minne tu, mwandishi wa habari wa Venezuela na mwanaharakati, Luis Luis Carlos Díaz, amenyanyaswa kupitia akaunti yake ya Twita na simu yake ya mkononi na kikundi kinachojulikana kama “wezi wa akaunti za mtandaoni”, na ambao hutumia jina la N33, na bila shaka ni kundi lilelile la watu ambao miezi michache iliyopita liliiba maneno ya siri ya akaunti za Twita na baruapepe ya karibu watu thelathini maarufu wa Venezuela, baadhi yao ni waandishi wa habari Sebastiana Barráez, Ibéyise Pacheco, mchekeshaji wa kisiasa Laureano Márquez, mwanaharakati Rocío San Miguel na mwandishi Leonardo Padrón, miongoni mwa wengine wengi. Kundi hili linajihusisha na watu wasiojulikana wanaojitapa kuwa waungaji mkono wa Rais Hugo Chávez.
Mwezi Desemba, watu maarufu kadhaa walitoa taarifa [es] kwa marais waliokuwa jijini Caracas ili kushiriki kwenye Mkutano wa CELAC ulioitishwa na Rais wa Venezuela Hugo Chávez:

Las cuentas de venezolanos con visiones críticas ante las políticas del gobierno, ubicados en distintos campos como el periodismo, la economía, la vida universitaria, los derechos humanos, la cultura y la justicia, entre otros, han sido “hackeadas” por individuos que asumen esa tarea agresora como un mecanismo de defensa del proceso político impulsado por el presidente Hugo Chávez.

Akaunti za raia wa Venezuela wanaoonekana kukosoa sana siasa za serikali, na walio kwenye fani mbalimbali kama vile uandishi wa habari, uchumi, vyuo vikuu, haki za binadamu, utamaduni na haki, miongoni mwa nyingine nyingi, zimeshambuliwa “kimtandao” na wale wanaoamini kwamba njia hii ndiyo ya kulinda mchakato wa kisiasa unaoongozwa na Rais Hugo Chávez.

Iria Puyosa (@NSC) alituma ujumbe wa Twita unaoonyesha uso wa akaunti ya Twita ambapo udhalimu huo umekuwa ukiibukia:

Tweets say: What I want you is to answer [the phone] @LuisCarlos, do you dare? Paraco [paramilitary] is your [whore] mother @luisfcocabezas @luiscarlos Answer [the phone] @LuisCarlos, I'm calling you… You're null @LuisCarlos and you're a Pirate… financed by Church, by pirate on the sense of a cheap copy of something that's original Your article is basic @LuisCarlos, coming from a so-called expert in informatic security. You're null and you're going Down

Ujumbe huo wa twita unasema: “Ninachotaka ufanye ni kujibu [simu] @LuisCarlos, je, utathubutu?”, “Paraco [askari wa kuzuia ghasia] ni mama yako [malaya] @luisfcocabezas @luiscarlos”, “Pokea [simu] @LuisCarlos, Ninakupigia…”, “Wewe ni zuzu tu @LuisCarlos na wewe ni haramia … unayepewa fedha na Kanisa, na ni haramia kwa sababu unafanya rudufu duni za kitu kilicho halisi”, “Makala yako haina lolote la maana @LuisCarlos, huku ukijidai kutoka katika hicho kinachoitwa ufundi katika masuala ya usalama ya habari. Wewe si lolote na utaangamia tu”

Díaz, ambaye licha ya kuwa mwanaharakati wa haki za binadamu na mchangiaji katika GV, vilevile anafanya kazi kama Mratibu wa Mawasiliano na Mitandao katika Kituo cha Gumilla, ambacho kinashughulika na utafiti na harakati za kijamii kinachoongozwa na Shirika la Wajesuiti nchini Venezuela.

 

Kwenye Twita, watu wameandika maoni ya kupinga unyanyasaji anaofanyiwa Luis Carlos:

@Jogreg: @N33DOS està acosando telefonicamente al pana @LuisCarlos. Ya basta!

@N33DOS mnamnyanyasa rafiki yangu @LuisCarlos kwa simu. Mkome!

@NSC: Parapolicías le ofrecen “trato VIP” a @LuisCarlos http://bit.ly/x9jvIL Si se equivocan x allí la respuesta también será VIP y global.

Ni vema Polisi wa usalama wampe @LuisCarlos “Matunzo ya hadhi ya juu”. http://bit.ly/x9jvIL Kama watashindwa kufanya hivyo, matokeo yake pia yatakuwa ya kiwango hichohicho cha hadhi ya juu tena ya ulimwengu.

@acianela: El inaceptable acoso a @LuisCarlos RT @IPYS Venezuela: Periodista y ciberactivista es amenazado telefónicamente

Unyanyasaji huu usiokubalika dhidi ya @LuisCarlos RT @IPYS Venezuela: Mwandishi wa Habari na mwanaharakati wa mtandaoni anyanyaswa kwa simu.

Luis Carlos Díaz aliwahi kuandika kuhusu matukio kama haya siku za nyuma. Kupitia makala yake [es], ya mwezi Septemba, 2011 alisema:

La acción dejó de ser una travesura cuando el grupo N33 emitió un comunicado, leído en el canal del Estado, VTV, en el que “aclaraban” que accionaron por razones políticas en contra de cuentas que criticaban al presidente de la República y por lo tanto cualquier opositor con visibilidad mediática estaría en la mira.

Kitendo hicho hakikuwa tena uzushi baada ya kundi la N33 kutoa tamko, ambalo lilisomwa kupitia luninga ya Taifa, VTV, ambapo “walifafanua” kwamba walikuwa wakitenda hivyo kwa sababu za kisiasa, wakishambulia akaunti zilizomkosoa Rais na kwa hiyo mpinzani yeyote aliyekuwa akifuatiliwa na vyombo vya habari naye pia angeshambuliwa.

Imeelezwa kwamba, kundi hilo hata limejiita “wezi wa akaunti za mtandaoni”, wala hawapaswi kujiita hivyo, hasa kwa kuzingatia kwamba walipata seti za mwanzo za maneno ya siri (au nywila) ya akaunti kwa kutumia mbinu kama vile uhandisi wa kijamii kwa kubuni maneno ya siri ambayo mtu angeweza kuyapata kirahisi. Hata hivyo, kwa vile wameteka nyara akaunti ya mwizi wa Venezuela wa akaunti za mtandaoni “white hat” RaFa Núñez, hivi sasa kuna mashaka kwamba huenda wanashirikiana na Shirika linalotoa huduma za intaneti ambalo linamilikiwa na serikali ya Venezuela.
Katika ujumbe kwa umma [es] ambao umerudiwarudiwa katika blogu mbalimbali za raia wa Venezuela, Luis Carlos amesema:

Nos enfrentamos a una nueva forma de ciberguerra más focalizada, de desactivar individuos sin mancharse mucho las manos, de afectar la libertad de expresión en Internet y acabar con las críticas gubernamentales. Este es una suerte de paramilitarismo digital, en el cual se buscan personas externas, e incluso espontáneos, para que eliminen gente en redes sociales.

Tunakabiliana na wimbi jipya ya vita vya mtandaoni, vilivyo makini zaidi, vya kuwafutilia mbali watu mitandaoni pasipo kuchafua sana mikono yao, kwa kuathiri uhuru wa kujieleza kupitia Intaneti na kukomesha ukosoaji dhidi ya serikali. Hii ni aina ya uaskari wa miamvuli ya kidijitali, inayowalenga watu wasio sehemu ya serikali, na hata wale wanaotetea, kuwamalizia mbali wale walio kwenye mitandao ya kijamii.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.