Taarifa ya raia mtandaoni ya Advox inatoa picha ya haraka kimataifa juu ya changamoto, ushindi na mienendo inayoibuka katika haki za kimtandao duniani.
Udhibiti mtandaoni na ukandamizaji wa watumiaji wa mitandao ya kijamii unafikia kilele kipya katika Venezuela ambapo wananchi wanaendelea na kupinga vikali uchumi na hali ya afya ya wananchi vilivyosabishwa na mgogoro wa kisiasa unaoendelea .
Imekuwa ni vigumu sana kwa waandishi wa habari kuchapisha habari kwa kuwa wanakabiliwa na kukamatwa mara kwa mara kwa “kuvuruga amani ya umma” au “kutishia mapinduzi”. Watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wanajishughulisha na mambo mapana ya kiraia ya wananchi nao wamelengwa.
Katikati ya mwezi Mei, Pedro Jaimes ambaye ni mtumiaji maarufu wa Twitter ambaye huchapisha habari juu ya utabiri wa hali ya hewa kwa wafuasi wapatao 80,000, alipotea . Muda mfupi kabla ya kupotea kwake Jaimes alituma ujumbe kupitia Tweetter kuhusu njia ya ndege iliyokuwa imembeba Rais Nicolas Maduro wa Venezuela, habari ambayo inapatikana kwa umma kupitia kituo cha habari mtandaoni cha Efecto Cocuyo.
Tarehe 15 Juni, zaidi ya mwezi mmoja baada ya kutoonekna, Jaimes aliwapigia wanafamilia kuwataarifu kwamba alikuwa amewekwa kizuizini ndani ya El Helicoide ambacho ni kituo cha jeshi kiligeuzwa gereza na mali ya huduma ya taifa ya kiintelejensia ya Bolivaria. (SEBIN).
Upatikanaji wa jukwaa la mawasiliano mtandaoni kwa sasa ni mgumu sana. Kususua kwa umeme wa gridi kutokana na ukosefu wa ukarabati na kutowashwa kwa muda katika harakati za mgao wa umeme umefanya upatikanaji wa mtandao kutokuaminika. Lakini bado habari za mtandaoni na mifumo ya mawasiliano vinahitajika sana kama njia pekee ya wanavenezuela kubadilishana na kupata habari ambazo sio za serikali.
Mapema mwezi Juni tovuti ya vituo vikubwa vya habari ambavyo ni La Pitilla na El Nacional, vilifungwa , pamoja na mtandao wa Tor ambao huwezesha watumiaji wa mtandao kukwepa udhibiti wa mtandaoni. Tovuti kubwa za picha za ngono zimefungwa nazo pia katika kile kinachoweza kuwa ni harakati za kujaribu uwezo wa kudhibiti mtandao wa taifa. Katika baadhi ya nchi hatua hizi zimekuwa zikitangulia katika harakati za kuongeza udhibiti mtandaoni.
Waandishi wapalestina wamelengwa kuvamiwa na kunyang’anywa simu za mkononi
Waandishi wa habri wanaochapisha habari za maandamano ya haki za kazi katika Gaza tarehe 19 Juni waliitaarifu MADA (kituo kwa maendeleo na uhuru wa vyombo vya habari Palestina) kwamba walivamiwa na simu za mkononi na kamera zao aidha kunyang’anywa au kuharibiwa na watu waliokuwa wamevaa sare wanahusiana na kikundi cha Hamas ambacho kinatawala ukanda wa Gaza.
Kwenye maandamano ya tarehe 15 katika mji wa West Bank, Ramallah, waandishi wa habari walitaarifu kuwa vikosi vya mamlaka ya usalama vya Palestina vilitumia mbinu zilezile katka jitihada za kuwakataza kupiga picha na kutochapisha habari juu ya maandamano hayo.
Mwanafunzi wa Nigeria asimamishwa masomo kwa kulalamia miundo mbinu ya shule
Kunle Adebajo, mwanafunzi anayesomea sheria katika Chuo kikuu cha Ibadan Nigeria alisimamishwa mihula mbili ya masomo kwa kuandika habari ambayo iliyoonekana ni kali kwa uongozi wa chuo. Tarehe 20 mwezi Aprili, Kunle Adebajo aliandika waraka wenye maoni, “juu ya hali ya kutisha ya paa na vyumba ”, ambapo ilieleza hali ya kusikitisha ya miundo mbinu ya mahali wanapoishi wanafunzi katika chuo kikuu hicho chake. Uongozi wa chuo ulimuita Adebajo kwenye kamati ya nidhamu ambayo ilieleza waraka wa debajo kuwa “ni wakukejeri, kashfa na kudharau uongozi” na kamati ilimsimamisha masomo.
Katika taarifa ya waandishi wa habari wa Sahara, Fisayo Soyombo ambaye ni mshindi wa tuzo ya mwandishi wa habari za uchunguzi na mmoja wa wanafunzi waliomaliza chuo kikuu cha Ibadan, alieleza hatua ya kinidhamu iliyochukuliwa dhidi ya Adebajo kama ni “kunyamanzisha waziwazi uhuru wa kutoa maoni.”
Mamlaka za Cuba zafuta sifa za vyombo vya habari na bloga mashuhuri
Mwanabloga wa zamani na mwanahabari wa zamani wa BBC Fernando Ravsberg ambaye ni mwandishi murugwai wa habari na ambaye amehamishia makao yake hapa Cuba tangu mwishoni mwa mwaka 1990 kwa mara ya kwanza alinyimwa sifa na masharti ya kuanzisha chombo cha habari na mamlaka za kudhibiti vyombo vya habari Cuba. Ravsberg kwa muda mrefu alitumia mapato aliyoyapata kutoka katika kazi yake kama mwandishi wa habari kutoka nje kuimarisha blogu yake mashuhuri inayojulikana kama “barua kutoka Cuba” (Cartas desde Cuba), ambapo huandika habari za kisiasa na maisha ya wananchi wa Cuba alizozifafanua vizuri, na mara nyingi akituma habari mara moja hupata maoni miamoja hivi kutoka kwa wasomaji. Hatua hiyo, Ravsberg aliiakisi katika maneno yake mwenyewe :
kwa miaka kumi iliyopita, wamenifunga kwa maneno mazuri ya ushauri, vitisho vilivyofichika na kuchekesha meno yangu , wakidai wanifukuze nchi na ‘maonyo’ yaliyoelekezwa kwa watoto wangu. Hakuna hata moja katika haya ambalo mpaka sasa limetekelezwa, lakini kuondoa sifa zangu za vyombo vya habari zimewaruhusu kuiua Cartas.
Katika Nicaragua vyombo vya serikali vinaonekana kubadili majina ya mitandao wa WIFI
Kutokana na maandamano dhidi ya serikali bado kuwa makali katika Nicaragua, mamia ya watu wametaarifu kuwa katikati ya mwezi Juni majina yao ya mtandao wa WIFI yalibadilishwa bila ya hiari yao usiku wa manane. Hao wote wanaotaarifu mabadiliko ni wale waliojiunga na Claro ambayo ni kampuni tanzu ya Kampuni kubwa ya mawasiliano ya Mexico ya America Movil.
Mtandao wa WIFI ulipewa jina lingine la “QuitenLosTranques,” lenye maana ya “simamamisha ukandamizaji” – kumbukumbu ya mbinu za kawaida za kuzuia maandamano kwa kuziba barabara. Ujumbe huu umetumika na maafisa wa serikali na waunga mkono mtandao mara kwa mara kama alama ya mitandao ya kijamii. Ukandamizaji umekuwa unaendelea karibu nchi nzima katika juhudi za kushinikiza Rais Daniel Ortega awalinde wananchi na nguvu kubwa unayotumiwa na serikali.
Programu ya India kuwapa maskini simu za mkononi bure – lakini haiwahakikishii usiri
Kuna mpango wa upatikanaji wa simu za mkononi ambao unatoa simu za mkononi bure kwa wanawake wenye familia wanaoishi chini ya kiwango cha umaskini kaskazini mwa India katika jimbo la Chhattisgarh. Ingawa simu hizo zinatolewa bure bila kutumia fedha, watu wanaojiunga na mpango huo lazima waoneshe namba za kadi za vitambulisho vyao vya taifa– vinavyohusiana utata wa Aadhaar na mpango wa vitambulisho vya taifa– na kusaini hati inaipa serikali “ridhaa ya kutumia numba hizo za Aadhaar.” Uchunguzi uliofanywa na chombo cha habari cha kujitegemea cha Scroll.in unaonesha kuwa washiriki hawajaambiwa jinsi serikali inavyoweza ikatumia namba zao za Aadhaar.
Utafiti Mpya
- Taarifa ya mwaka 2018 kwa Halmashauri ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa juu ya sheria ya Maudhui – David Kaye, mwanahabari maalumu wa Umoja wa Matiafa juu ya kulinda na kuimarisha haki ya uhuru wa kutoa maoni na kujieleza
- taarifa ya habari za Kidijitali ya mwaka 2018 – Taasisi ya Reuters
Jiunge na Taarifa zinazotolewa na Raia Mtandaoni
Ellery Roberts Biddle, Marianne Diaz, L. Finch, Oiwan Lam, Laura Vidal na Sarah Myers West wamechangia taarifa hii.