Samahani, Siongei Kiingereza. Naongea kwa Picha

Mpiga ngoma akiwa katika mtaa wa Detroit, Michigan, Marekani. (Picha na mwandishi na imechapishwa kwa ruhusa).

Kuongelea maana ya kuhama kunaweza kuwa kugumu, labda muda au umbali huwasaidia kuona vizuri zaidi mchakato mzima wa kuhama kuwa una mambo mengi. Kila hadithi ya kuhama ni pekee, lakini hujumuisha mambo ambayo hupitiwa wakati wa kuhama ambayo ni sawa na hadithi nyingine katika maisha.. Je, ushauri huu unaweza kuwa wa faida yoyote kwa watu wanaojikuta katika mchakato wa kuhama nyumbani kwao, au ambao tayari wameshahama? Kwa watu hawa hakuna maneno yenye nguvu kiasi cha kuwa faraja yoyote au kuwa ushauri. Hakuna hata mmoja ambaye anakuwa amejindaa vizuri kuondoka.

Katika Venezuela ambapo niliondoka , nilikuwa sehemu ya hadithi iliyoongelewa na kundi zima la watu ambao hawakuhitaji maelezo kutoka kwangu. Kila kitu kilikuwa rahisi kukisoma: ishara, utaratibu, hatari, yaliyopita na yajao—hata kama yalikuwa yamefunikwa na ukungu wa hali mbaya ya kisiasa. Kwa sababu utambulisho wa mtu binafsi na kundi ilikuwa wazi sana katika shughuli zetu za kila siku, maswali yamimi ni nani au wao ni akina nani hayakuwepo kwangu. Kipindi kilekiwango cha uhamaji kutoka Venezuela kilikuwa hakijafikia idadi ya kutisha kama tunayoiona leo, na kuhama kulikuwa bado ni mapenzi ya mtu: kwenda nje ilikuwa na maana ya moja kwa moja kuwa na maisha mazuri katika nchi hiyo mpya.

Venezuela ambayo ilianza kujijenga uhamishoni tangu mwaka 1999 ilikuwa haikueleweka kwa wanavenezuela ambao walikuwa wameachwa nyuma. Manung’uniko ya wahamiaji juu ya hali ya maisha yao yalikuwa hayakubaliki na ndugu zao ambao muda huo walikuwa wanateseka na kile kinachojulikana leo kama hali mbaya ya kisiasa, kiuchumi na haki za binadamu katika historia ya sasa ya Venezuela. Kwa sababu hiyo, wahamiaji hawakuwa na la kusema juu ya tatizo lolote: maoni ya kisiasa ya nchi zao yalipuuzwa kutokana na umbali na ugumu uliotokana na mabadiliko ya maisha yao. Imani kuwa nchi mpya ingewapa maisha bila ya matatizo ukilinganisha na matatizo waliyokuwa wanayapata waliobaki Venezuela yalijaa kwenye mawazo ya wale waliokuwa wanawaangalia wakiwa nyumbani. Wakati huo, nchi iliyowapokea wahamiaji haikujali ukosoaji na maoni yao kuwa ni haki, na zaidi haikuwaruhusu kufanya shughuli za kisiasa.

Hali nyingine halisi ya nje na nchi zisizoingilika

Mwaka 2011 kipindi cha kiangazi wakati ninawasili Marekani nilikuwa sijui chochote juu ya mambo ambayo ninayazungumzia sasa. Wakati ule kwa kushindwa kuongea lugha ya kiingereza, nilikuwa natamka maneno machache katika kusalimia na kuomba msamaha. (Chaguo la kuwaeleza rafiki zangu waliokuwa bado Venezuela haikuwa chaguo tena).Ili kuanzisha mazungumzo yoyote mapya, nilihitaji msaada wa mume wangu kuniandikia, kusoma na kutafsiri kile ambacho nilikuwa nawambia watu na halafu yeye akitafsiri kile walichosema.

Picha iliyopigwa wakati wa tamasha la bendi ya Detroit. Nyuma ya huyu mama kijana ambaye anaangalia kamera bila ya aibu, kuna mpingaji wa kidini anayezungumzia kusamehewa na kutubu. Hii ni kinyume kabisa kusimama mbele ya kamera yangu bila mimi kumuomba kufanya hivyo. (Picha na mwandishi na imetolewa kwa kuruhusa).

Kwa ufupi, kipindi cha umri wa miaka 26, nilikuwa kama mwanamke asiyejua kusoma na kuandika ambaye anategemea sana mme wake kwa kuwasiliana. Uoga huu ulifanya kujifungia nyumbani, ukiambatana na upweke wa muda mrefu. Kadhia kubwa wakati mtu anapoondoka kutoka nchini mwake na ambayo inakatisha tamaa sana katika nchi ya ugenini inaweza kuwa kutumbukia katika hatari ya kukosekana kwa usalama kabisa.

Kwa hiyo, kujificha mbali , kwa hiyo ni moja ya njia mtu anaweza kuchukua na hii ndiyo hakika niliyoitumia kwa muda mrefu.

Kipindi hiki cha kufungiwa, madirisha ya nyumba yangu yalikuwa ndiyo kamera yangu niliyoipenda. Uwazi huu mkubwa wa madirisha ulinipa nafasi kuwa karibu na mambo mbalimbali ya kijamii ambayo niliyaona. Sehemu ya kivutio katika kuwaangalia ipo kwenye maswali kuhusu ukweli wa ugenini. Pia, asili ya majibu yatolewayo kwa maswali hayo, huibua zaidi maswali yasiyojibika.
kwa kuangalia, kushangaa na kufurahia, niligundua kwamba watu niliokuwa nawaangalia walikuwa wanatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Wakati dunia hii yenye utajiri wa kutofautiana ulikuwa ukishamiri na kupanuka, kujulikana kwangu kulikuwa kunapungua. Nilikuwa sijione tena kama natoka jiji la Barquismeto, badala yake kama mtu wa Venezuela. Nilijikuta katika aina ya jamii ya watu wasioeleweka.I even fell into a category that was as new as it was incomprehensible: nilikuwa I was a latina, kitambulisho kinachopaswa kumuelezea mtu fulani kutoka Tierra del Fuego kutokuwa tofauti na mtu atokaye katika jiji la Juarez katika nchi ya Mexico.

Lakini kutokana na hayo yote nilifaidika kitu fulani.: nimetambua kuwa bila kushindwa, si wavenezuela kutoka hapa au kule, wala si wamarekani kutoka sehemu yoyote nchini anayeweza kukataa habari au matokeo yatokayo na picha au mpiga picha. Hili ndilo nililojifunza pindi nilipoamua kutoangalia kupitia dirisha langu na kwenda nje kwa mara ya kwanza na kamera yangu ya kampuni.

Kila wakati sasa ninakuwa na kamera .

Dondoo za habari za dunia

Kuna jambo limevuka mipaka katika kupiga picha. Picha iliyopigwa ni nyara ndogo ya mwizi mjanja aliyekuwa mhusika wa dondoo za habari dunia. Nafasi ya mitaa ilikuwa finyu na ishara zilikuwa muhimu, lakini kwa nia ya kumjua aliyenifanya nijifiche, badala yake nilijaribu kuzikusanya na kuzielewa zote usiku, nilipokuwa narudia picha zilizobaki siku ile.

Mimi , niliyekuwa kizuizini kwa miaka mingi, ghafla nilipata ujasiri wa kutoka nje na kuwakabili watu kwa kamera yangu. Nilipoanza kusoma vifungu vifupi vya maneno vilijumuishwa kwenye matukio ya maadhi ya watu, jambo ambalo lilikuwa msingi na lilisaidia kuongeza ubora wa picha.

Ann Arbor, Michigan. (Picha na mwandishi na imechapishwa kwa ruhusa.).

Hata wakati uwezo wangu wa kuwasiliana ulikuwa mdogo. Watu walikuwa wanakuja kuniomba niwapige picha. Ukiwa na aina hii ya uwezo katika hali hii ambayo upo katika nchi nyingine wakati muda mwingine mtu huyo angepita mbele ya dirisha langu bila kuniona na sasa ananiangalia moja kwa moja hii ilikuwa njia nyingene ya kupata uzoefu kama mhamiaji. Pia ilikuwa kama ushindi mdogo wa kukabili ukosefu wa usalama ambao wahamiaji wote wanapaswa kuuishi.

Kama mvezuela na kupitia kamera yangu, nimejitengenezea picha ya Mareakani— na kwa maisha yangu pia. Kupiga na kugawa picha zangu kulifanya iwezekane kwangu kuwasiliana kwa kutumia lugha iliyotegemea ishara zaidi kuliko sauti.
Kwa kutumia kamera, nilijifunza namna ya kusoma dunia yangu mpya. Nilijifunza kuzungumza sio kiingereza wala kispanishi, bali picha . Na muhimu zaidi, mara nyingine nilijifunza namna ya kutazamwa kwa jicho . Picha ilikuwa ni daraja ambalo kwalo niligundua kwamba mimi ni mtu mwingine katika nchi hii lakini pia kuwa tofauti ni vizuri; zaidi sana kwamba hakuna kisichoweza kupigwa picha na hakuna kisichoweza kutoa habari mpya.

Zaidi angalia picha za Natali kwenye Instagram.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.