Nukuu 8 za Kushangaza Zilizopata Kutolewa na Wanasiasa wa Malaysia

Balik Cina ni tovuti mpya ambayo hukusanya baadhi ya nukuu za kuchekesha na za ajabu zinazotolewa na wanasiasa wa Kimalysia.

Nukuu nyingi zinazowekwa kwenye mtandao huo huwa zinatumwa na watumiaji wa mtandao. Nukuu huunganishwa na kungo cha chanzo cha habari kinachotoa undani na mukhtadha wa suala husika.

Balik Cina kwa hakika ni maarufu sana nchini Malaysia. Hapa unaweza kuona sababu za kwa nini tovuti hiyo imeitwa Balik Cina:

Balik Cina ina maana ‘rudi China’ kwa lugha ya Kibahasa Malaysia. Neno Balik Cina lilikuzwa na mkuu wa shule ya sekondari ya Shah Alam mwezi Julai 2013. Neno hilo na yanayofanana nayo yamekuwa yakitawala mijadala ya mtandaoni nchini Malaysia. Tukiwa tumehamishwa na ubora wa matamshi yanayotolewa na wanasiasa wa Malaysia, tulianzisha tovuti ya BalikCina.com kuweka kumbukumbu sawa ya maendeleo ya siasa zetu.

Balik Cina inahamasisha kukusanywa kwa nukuu zote nzuri na zenye hamasa zinazotolewa na wanasiasa wa Malaysia na watu maarufu wa nchi hii.

Aizyl Azlee wa mtandao wa The New Forward anapitia tovuti hiyo na kuthibitisha kuwa wanasiasa wa Malysia mara nyingine hutoa kauli za kijinga:

Wanasiasa wa Malaysia husema mambo ya kijinga mara nyingi kiasi kwamba hatuwezi hata kuyashika yote wanayoyasema. Kabla hatujamaliza kucheka kwa ujinga mmoja, ujinga mwingine tayari unakuwa umeshasemwa na unasambaa mtandaoni. Ni ujinga mwingi kiasi kwamba hatutaweza kabisa kukumbuka hata nusu tu ya yale tuliyoyacheka.

Hapa chini unaweza kusoma mifano minane ya baadhi ya nukuu za kukumbukwa na kwa hakika za kushangaza zilizowahi kutolewa na wanasiasa wa Malysia katika miaka ya hivi karibuni:

1. Waziri wa Mipaka Tengku Adnan Tengku Mansor ameibua utata wakati alipofananisha /a> uthamanishaji wa ardhi na wanawake. Ameomba radhi kwa matamshi yake lakini amelaumu vyombo vya habari kwa kumnukuu isivyo.

makeup

2. Waziri Mkuu Najib Razak, mtumiaji mkubwa na maarufu wa mitandao ya kijamii nchini Malaysia, ameweka picha inayomwonyesha akiwa na mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg. Ila inaonekana alidhani alikuwa kwenye makao makuu ya Twita.

najib_fb

3. Ukiacha nguo zenye shingo ya V, mwongozo wa mavazi umetahadharisha kuwa ‘kupenda kuvaa mavazi yaliyobana na yenye rangi zinazong'aa sana’ ni ishara ya ushoga.

gay

4. Mwezi uliopita, tovuti huru ya mtandaoni ilinyimwa ruhusa ya kuchapisha kwa sababu ya mantiki ifuatayo:

newspapers

5. Kiongozi wa Upinzani Anwar Ibrahim huenda alidhani angeweza kutumia janga la ndege ya MH370 kuendelea kushusha hadhi ya serikali. Serikali imejibu mapigo.

anwar

6. Mbunge anataka kufuatilia matumizi ya mtandao ili kuwafurahisha ndugu wa wahanga wa ndege iliyopotea ya Malaysia ya MH370. Alishutumu kutokudhibitiwa kwa habari kama chanzo cha hasira ya ndugu hao.

censor

7. Zile pamba za wanawake lazima ziwe chanzo cha maovu yote mabaya duniani.

sanitary_pads

8. Malaysia, taifa lenye waislamu wengi, lina sheria inayopiga marufuku wasio waislamu kutumia neno Allah wakimaanisha Mungu wa Wakristo.

ali

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.