Chanzo cha Maji nchini China Chawekwa Kemikali Inayosababisha Kansa

Mamlaka ya jiji la Lanzhou imetoa angalizo kwa raia wake la kutokutumia maji ya bomba kutokana na maji hayo kugundulika kuchanganyikana na kemikali hatari, hali iliyopelekea maji ya viwandani kugombaniwa katika maduka mbali mbali ya jiji.

Kwa mujibu wa mamlaka ya jiji, kiasi kikubwa cha benzini, kemikali inayosababisha kansa, kimegunduliwa kwenye chanzo cha maji cha jiji hili. Wakati fulani, kiwango cha benzene kwenye maji ya bomba kilipanda hadi mara 20 ambacho ni kiwango hatari kabisa kwa matumizi. 

Lanzhou, jiji la viwanda lililopo Kaskazini Magharibi mwa China, linategemea sana mto wa njano kama chanzo chake cha maji. Miaka ya hivi karibuni, jiji hili lenye wakazi takribani milioni nne limeanza kuona matumaini ya ongezeko la uwekezaji wakati ambao taifa limebuni njia mpya za kuinua uchumi wa kanda masikini za magharibi. 

lanzhou

Wakazi wa Lanzhou wakigombania maji ya chupa mara baada ya mamlaka ya jiji kutoa tangazo la kutokutumia maji ya bomba. Picha kwa idhini ya mtumiaji wa Sina Weibo, Wangyangyagn de Xiaopengyou.

Kampuni ya Kifaransa ya utibuji wa maji, ijulikanayo kama Veolia, na wasambazaji wakuu wa maji jijini Lanzhou, ililiambia  shirika la habari la serikali la Xinhua kuwa, benzini iliyopo kwenye maji imetoka kwenye viwanda vya uchimbaji na usafishaji wa mafuta ya asili. 

Ofisi inayohusika na utoaji wa taarifa katika jimbo la Gansu, ambapo Lanzhou ikiwa ndio mji mkuu, iliweka ujumbe huu kwenye ukurasa wake rasmi wa sina Weibo ufananao na wa twitter: 

【未来24小时兰州居民不宜饮用自来水】4月11日凌晨3时起,兰州威立雅水务公司向水厂沉淀池投加活性炭,吸附有机物降解苯对水体的污染。11日上午11时,停运北线自流沟,排空受到污染的自来水。在此期间,市区降压供水,高坪及边远地区停水,限制生产性用水。未来24小时自来水不宜饮用,其他生活用水不受影响。

Kwa muda wa masaa 24 yajayo kuanzia sasa, maji ya bomba hatafaa kwa matumizi kwa wakazi wa Lanzhou. Kuanzia saa 9 usiku, Aprili 19, Lanzhou Veolia imeshaweka kemikali ya kaboni kwenye mapipa ya kampuni kwa lengo la kufyonza dutu za kioganiki kama namna ya kuyeyusha benzini iliyo kwenye maji hayo. Majira ya saa 5 asubuhi, April 11, kampuni hii ilisitisha utoaji wa huduma katika mfumo wa mabomba wa Kaskazini kwa lengo la kuyaondoa maji yaliyochanganyikana na kiasi kikubwa cha benzene. Katika kipindi hiki, kwa maeneo ya mijini, maji yatakuwa yakitolewa kupitia mbinu ya kupunguza kani eneo, lakini hakutakuwa na maji kwa mtaa wa Gaoping na maeneo mengine ya pembezoni. Utumiaji wa maji viwandani utazuiwa. Kwa kipindi cha masaa 24 yajayo, maji yanayotiririka hayatafaaa kwa matumizi ya kunywa, aina nyingine za maji hayatakuwa na shida.

Vyombo vya habari vya China vimeripoti kuwa, mwezi uliopita, wakazi wa Lanzhou walitoa malalamiko yao kuhusu harufu mbaya ya maji ya bomba, lakini viongozi wa jiji walisema kuwa ubora wa maji ulikuwa wa kiwango kilichokubalika. Raia kadhaa waliokuwa wakitoa taarifa za maji kuchanganyikana na kemikali hatari kwa kipindi hicho walijulikana kama “wavujisha tetesi” na “kushughulikiwa” kwa mujibu wa sheria. 

Tatizo la maji la Lanzhou limezidi kuchochea zaidi tatizo lisilozuilika la uchafuzi lililolishitusha taifa kipindi ambacho uanaharakati wa mazingira unaanza kushika kasi nchini China. Mwaka 2013,  mwanablogu mashuhuri na mwandishi wa habari wa zamani alianzisha  kampeni ya mtandaoni ya kuwataka watumiaji wa mtandao kupiga picha za uchafuzi wa mito katika maeneo wanayoishi.   

Uchavuzi wa maji kwa kemikali hatari huko Lanzhou imekuwa ni moja ya mada tatu zilizopewa kipau mbele katika mtandao wa Weibo siku ya Ijumaa usiku. 

Jarida la habari za Beijing liliweka taarifa hii kwenye ukurasa wake rasmi wa Weibo: 

【已切断污染源 政府免费提供安全水】兰州市应急处置领导小组基本找准了污染点,并马上予以切断。有关方面正从周边地区调运桶装水和瓶装水,将通过各区政府和辖区街道、社区,向广大市民免费提供

【Chanzo cha uchafuzi kimeshasitishwa. Serikali itaanza kutoa maji bure na yaliyo salama】. Jopo la dharura la Jiji la Lanzhou limeshafahamu chanzo cha uchafuzi wa maji na ilishatoa tamko la kukisitisha. Idara husika zimeshakusanya maji ya kwenye chupa na ndoo za maji kutoka katika maeneo ya jirani, na maji haya yatagawanywa kwa raia kupitia idara na jumuia mbalimbali..

Watumiaji wa Weibo wameikosoa serikali kwa kuruhusu kampuni isiyo milikiwa na wachina kusimamia mifumo ya maji ya jiji. Msanii wa uchekeshaji, Zhang Gang alitoa malalamiko yake:

 呼吁兰州政府调拨安全的饮用水,向市民免费发放!给出正面、准确的解释!接连不断的水污染让百姓情何以堪?洋鬼子控股的自来水厂能相信吗?把自来水厂卖给法国人,谁卖的?谁同意的?

Ninaiomba serikali ya Lanzhou ikusanye maji salama ya kunywa na iyagawe bure kwa raia wake!Yapaswa kutolewa jibu fasaha na la wazi!Ni udhalilishaji wa namna gani tatizo la uchafuzi wa maji liendelee kwa watu walewale. Tunaweza kuwa na imani na makampuni yanayosambaza maji yanayomilikiwa na wageni? Ni nani aliyeamua kuwauzia Wafaransa kampuni ya usambazaji wa maji, Ni nani alifanya hivyo?, na ni nani aliyetia saini?

Beijing Chuzi, mtumiaji wa Weibo aliye na marafiki zaidi ya nusu milioni, aliandika

这是政府做的最傻逼的一件事。最应该国营的放给外人做。我能不怀疑有人从中赚大钱么

Serikali imefanya jambo la kipumbavu kabisa. Imetoa [mamlaka ya usambazaji maji] kwa wageni wakati kimsingi mamlaka ilipaswa kuongozwa na serikali yenyewe. Nina wasiwasi kuwa mkakati huu umekuwa ni wa maslahi binafsi.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.