Kongo Brazzaville: Uchaguzi wa Rais Wakatisha Tamaa


Siku ya Jumapili, Julai 12, watu wa Jamhuri ya Kongo walipiga kura katika uchaguzi ambao ulisusiwa na viongozi wa Upinzani kwa madai kwamba usingekuwa huru wala wa haki. Denis Sassou N’Guesso, ambaye ameitawala Kongo kwa takribani miaka 25 kama mkuu wa nchi, anatafuta kipindi kingine cha miaka saba madarakani.

Pamoja na malalamiko kutoka upinzani, waangaliaji wa uchaguzi walisema kuwa upigaji kura ufanyika kwa amani, na kwamba idadi ya watu waliojitokeza kupiga kura ilikuwa ndogo. Kwa mujibu wa chama kikuu cha upinzani, “asilimia 90” ya wapiga kura hawakujitokeza kupiga kura. Rais anayemaliza muda wake Denis Sassou N’Guesso na chama chake cha Rassemblement de la majorité présidentielle (RMP) anatabiriwa kushinda uchaguzi huo wakati ambapo tume ya uchaguzi inajiandaa kutangaza matokeo wakati wowote kuanzia Jumatatu jioni.

Mwandishi wa BBC anadai kuwa alishuhudia fedha zikitembezwa katika vituo vya upigaji kura kusini mwa mji mkuu, kwa watu ambao baadae walisema kuwa waliombwa kumpigia kura Bw. Sassou-Nguesso.”

Mwangalizi mmoja wa uchaguzi, akizungumza kwa masharti ya kutokutajwa jina, aliliambia shirikala habari la Ufaransa (AFP), “Kuna waangalizi wengi kuliko wapiga kura.”

Katika kituocha habari cha Ufaransa cha France 24, watoa maoni wachache kutoka Kongo wametoa maoni yao kuhusu uchaguzi. Hapa chini ni sehemu ndogo ya maoni hayo:

Maloumbi kuhusu kutishiwa kwa wapiga kura:

Dans certain villages et districts, les populations ont vote sassou nguesso suite aux intimidations. mon frere Jean Ibinga dans le district de Nyanga a reçu 1.000.000 Cfa de la part de membre de RMP pour convaincre aux vielles personne d'aller vote moyenant une somme de 2500 cfa. Les elections ne ce sont pas passees d'une maniere convenable et certains prefets, deputes ont intimider la population de voter leur maitre Sassou. Pour moi c'est une election qui avait ete deja jouee a l'avance. Je demande a la communaute internationale d'anuler les elections du 12 juillet et oblige a sassou de faire un gouvernement national pouvant debattre les affaires du pays sinon il y'aurait une guerre dans le futur. l'opposition actuellement se prepare pour une eventuelle guerre.

Katika vijiji na wilaya fulani fulani watu walimpigia kura Sassou Nguesso kwa sababu ya kutishwa. Kaka yangu Jean Ibinga katika wilaya ya Nyanga alipokea cfa 1 000 000 [Sawa na dola la kimarekani 1 800] kutoka kwa wafuasi wa RMP ili awashawishi wazee waende kupiga kura kwa kuwapa kiasi cha cfa 2500 [Dola za Kimarekani 4.5]. Uchaguzi haukwenda kwa namna inayokubalika, na baadhi ya viranja na manaibu waliwatisha watu ili wampigie kura mtawala wao Sassou. Kwangu huu ulikuwa uchaguzi wenye matokeo yaliyofahamika kabla ya muda. Naiomba JUmuiya ya Kimataifa iutangaze uchaguzi wa Julai 12 kuwa ni batili na kumlazimisha Sassou kuunda serikali ya Kitaifa itakayokuwa na uwezo wa kujadili masuala ya nchi, vinginevyo vita vitatokea huko mbeleni. Upinzani uliopo unajiandaa kwa uwezekano kwa vita.

Yoka kutoka Pointe Noire kuhusu kujtokeza kwa idadi ndogo ya wapiga kura:

je suis congolais et je réside à pointe noire (capitale économique du congo et deuxième ville du pays). Je peux vous dire que les bureaux de vote sont restés vide du matin jusqu’ au soir . les habitants de pointe noire sont fatigués, des promesses de mr sassou, alors que de cette ville qu’ est tiré le pétrole qui constitue la première richesse du pays. Plus de 95% des congolais n’ ont pas voté. c’ est une réalité que le régime brutal et absurde de brazza doit reconnaitre. Du coup son régime est illégitime. les congolais du nord, du sud, de l’ est et de l’ ouest ont dit NON à sassou.

Mimi ni Mkongo na ninaishi Pointe Noire (Mji mkuu wa kiuchumi wa Kongo na jiji la pili kwa ukubwa). Ninaweza kuwaambia kwamba vituo vya upigaji kura vilikuwa vitupu tangu asubuhi mpaka jioni. Wakaazi wa Pointe Noire wamechoshwa na ahadi za Bw. Sassou wakati jiji hili linalozalisha mafuta ni la kwanza kwa utajiri nchini. Zaidi ya asilimia 95 ya wa-Kongo hawakupiga kura. Ni ukweli ambao utawala huu wa kikatili na kijinga nchini Brazzaville wanapaswa kuutambua. Kwa sababu ya hilo, utawala huu ni batili. Wakongo kutoka Kaskazini, Kusini, Mashariki na Magharibi wamesema HAPANA kwa Sassou.

Mtoa maoni aliyeficha jina lake kutoka Kinshasa , Kongo (DRC), alijiuliza:

Peut on frauder avec seulement 15% d'électeurs qui, si nous suivons les différentes interventions, ne seraient que les partisans du Candidat Sassou, les autres ayant opté pour le boycot de l'éléction?

Hivi anaweza kweli mtu kudanganya kwa kutumia asilimia 15 tu ya wapiga kura waliojitokeza ambao, kama tukifuatilia ripoti, walikuwa ndio wafuasi pekee wa Mgombea Sassou, wakati wengine walichagua kuususia uchaguzi?

L'Africaniste:

Oui tout n'est parfait ! Oui Sasou garde le pouvoir , Oui , il n'a pas fait du congo un paradis ! Mais qu'a fait l'opposition ? Quel projet ou proposition l'opposition congolaise a t’ elle soumis au peuple ? rien sauf le boycott ! qui n'est rien d'autre qu'une ouverture à Sassou pour gagner . Alors merci messieurs les opposants d'avoir aider Sassou à gagner sans difficultés . Arrêtez des bruits pour rien sauf pour distraire le peuple!

Ndio kila kitu kiko sawa sawa! Ndio Sassou anabaki madarakani! Ndio hakuigeuza Kongo iwe ahera? Lakini wapinzani walifanya nini? Mipango ipi ya miradi ambayo wapinzani wa Kongo waliitoa kwa wananchi? Hakuna isipokuwa kususia! Kitu ambacho si kingine zaidi ya kumpa Sassou ishara ya kushinda. Kwa hiyo asanteni waungwana wa upinzani kwa kumsaidia Sassou kushinda bila ugumu wowote. Acheni makelele yasiyo na kingine isipokuwa kuwachanganya watu!

brazza-brazza kuhusu uchaguzi wa amani:

Élection bidon, mais nous avons la paix. La paix des miséreux.
Comme Bongo, Sassou sera au pouvoir pour plus de deux générations. C'est normal; nous avons la paix. La paix des soumis.
Sassou pille le Congo. Mais nous avons la paix. La paix des affamés.
Nous vivons dans le caca. Mais nous avons la paix. La paix a plus de valeur que la dignité.
Vous a l'étranger vous ne savez pas ce que la paix vaut.
Je suis d'accord avec vous que la paix permet a Sassou de piller. Et alors? C'est normal qu'il nous pille. Il es africain et il est dictateur qui fait des élections bidon pour rester dictateur.

Uchaguzi wa uongo, lakini tuna amani. Amani ya walioelemewa na ufukara. Kama Bongo, Sassou atakuwa madarakani kwa zaidi ya vizazi viwili. Ni kawaida; tuna amani. Amani ya wanyenyekevu.
Sassou anaipora Kongo. Lakini tuna amani. Amani ya wenye njaa. Tunaishi katika kinyesi. Lakini tuna amani. Amani ina thamani kuliko utu. Nyie wote mnaoishi ughaibuni hamjui kiasi cha thamami ya amani.
Ninakubaliana nanyi kwamba amani inamwezesha Sassou kupora. Kwa hiyo? Kuporwa ni kawaida. Yeye ni mwafrika na ni Dikteta ambaye amefanya uchaguzi wa uongo ili aendelee kuwa dikteta.

Kwenye Tovuti ya Libération Yanice 18 aliileta hotuba ya hivi majuzi ya Obama akiwa Ghana:

A peine hier, Obama a tenu un très bon discours sur la bonne gouvernance et la démocratie, aujourd'hui un autre autocrate africain se prépare à renouveler son bail au pouvoir pour 7 ans encore malgré ses déboires judiciaires relatifs à ses biens immobiliers en France. A voir la longévité au pouvoir, 25 ans, de ce président tout laisse à penser qu'Obama a prêché dans le désert.

Ni jana tu Obama alitoa hotuba nzuri kuhusu utawala mzuri na demokrasia, leo dikteta mwingine wa Kiafrika anajiandaa kuandikisha upya dhamana ya madaraka yake kwa miaka mingine 7 pamoja na kushindwa kwake kisheria kuhusu majengo yake nchini Ufaransa. Ukiangalia muda rais huyu aliodumu madarakani, miaka 25, inaonekana kama vile Obama alihubiri jangwani.

Na Saboun aliongeza:

Ré-election de Sassou Nguesso, aucune surprise. Je ne sais pas si vous avez remarqué, Obama n'a évoqué aucun pays d'Afrique francophone dans son discours, pure coincidence? J'en doute.

Kuchaguliwa tena kwa Sassou Nguesso, si ajabu. Sijui kama uliliona hili, Obama hakutaja nchi yoyote ya Afrika iliyowahi kutawaliwa na Wafaransa katika hotuba yake. Hivi kweli hili ni jambo lililotokea bila kukusudiwa? Sidhani.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.