Je, Baada ya miaka 50, Chama Tawala cha Malaysia Kitashinda Uchaguzi?

Maudhui makuu katika Uchaguzi Mkuu wa 123 nchini Malaysia uliofanyika Mei 5, 2013 yamekuwa ni matarajio ya mabadiliko, au ‘ubah’ (mabadiliko ya Malay). Kauli mbiu maarufu kubandikwa kuhusu ni ‘ini kalilah, ubah’ ambayo hutafsiriwa kama ‘wakati huu, mabadiliko yanakuja’.

Kwa kusema hayo, haijawa wazi bado jinsi uchaguzi utakavyo kuwa, na Kituo cha Habari cha Asia kimetangaza kwamba Muungano wa chama tawala Barisan Nasional (BN) bado una nafasi kubwa ya kushinda, lakini kwa tofauti ndogo ya kura. Chama cha BN kimetawala Malaysia kwa kipindi cha nusu karne.

Shufei  alijenga hoja ya ulazima wa mabadiliko ya serikali:

Mimi sio mtu yw siasa kivile. Naichukia kusema kweli, na hunifanya kuwa na hisia za hasira zaidi ya kitu kingine chochote. Najijua. Huwa nasisimka kwa urahisi na kupandwa na hasira ninaposoma kuhusiana na mambo ya upendeleo, chuki,  mbinu chafu, tabia zisizokubalika, rushwa. Chochote chenye uharibifu kwa utu wa mwanadamu lakini hichohicho ndicho kinachotumika kuua watu ninaoamini ndio wamebeba mustakabali wa nchi yangu.

Lakini je, huoni kuwa tulistahili kuwa na hiari ya kuamua tukitakacho? Mfumo wa vyama viwili ili tuwe na uwezo wa kuchagua tukipendacho kama serikali inakuwa imetopea kwenye vitendo vya ufisadi? Je hiyo si ndiyo maana ya demokrasia? Si kunyamazishwa kwa sababu ‘wao wamefanya mambo mengi kwa ajili yetu’. Ndiyo, wamefanya mambo kwa ajili yetu, lakini wao ni serikali yetu. Ni, samahani kwa kuwa mkweli,  ni kazi yao

Glam pia alitoa wito kwa wasomaji wao kupiga kura kwa ajili ya mabadiliko katika serikali, kwa kutumia video kadhaa.

Anil Netto pia aliweka video ya wapiga kura huko Penang  wakitoa wito kwa mabadiliko katika nchi.

 Watu wamekwisha amua. Hii haikuwa juu ya watu kutoa wito kwa kujengwa barabara milimani, barabara kuu mijini na nyumba za kifahari; ilikuwa ni juu ya watu kutoa wito wa kumalizwa vitendo vya kifisadi katika nchi na kwa ajili ya mabadiliko ya kisiasa katika ngazi ya nchi.

Thomas alimwelezea Waziri Mkuu Najib Razak kama ‘Mbabe’ katika siasa za Malaysia:

Nchini kote, kwenye mabango mengi ya chama cha BN, machapisho na matangazo ya runinga na habari, kile unachoona ni sura yenye tabasamu zuri lenye upole la Najib. Haijawahi kutokea katika historia ya uchaguzi mkuu katika nchi yetu kutokea uchaguzi kutawaliwa na tashasha za mtu fulani badala  ya tafakuri au maono ya chama kwa ajili ya nchi. Lakini Najib Razak ni ‘mbabe’, ambaye haiba yake imejengwa asasi zenye utaalamu mkubwa wa mahusiano ya umma kama APCO kwa msaada wa matangazo mengi pamoja na machapisho kibao kwenye vyombo vya habari. Yeye alikuwa na uhawilishaji uliokithiri ambao ulimbadilisha kutoka mwanasiasa wa ki-Malay hadi kuwa mtu anayetangazwa kuwa mtu wa umoja na mtunzaji wa tunu za Malayasia.

Malaysia has been swamped with campaign materials such as banners, flags, posters and billboards. Photo by Hon Keong Soo, Copyright @Demotix (5/2/2013)

Malaysia imefurikwa na viwezeshaji vya kampeni kama vile mabango, bendera, vipeperushi na mabango makubwa mitaani. Picha kwa hisani ya Hon Keong Soo, haki miliki @Demotix (5/2/2013)

Hii ni mara ya kwanza kuruhusiwa kwa upigaji kura kupitia posta katika uchaguzi wa Malaysia. Chelliah, M-Malaysia aishiye nchini Uingereza, aliandika kuhusu furaha yao katika uwezekano wa mabadiliko katika serikali:

 Ninapoandika taarifa hii jua linatokea nchini Malaysia siku mpya na mimi ntakuwa na kwenda kulala mapema kwa sababu ni siku ndio inaishia hivyo hapa nchini Uingereza. Kuna kitu cha kushangaza kuhusu hilo. Mimi nilitoka Malaysia miaka 32 iliyopita na ingawa mimi sasa naishi maelfu ya maili nina msisimko katika matarajio ya ‘Ubah’ (‘mabadiliko’ katika lugha ya Malay) kuwa ukweli mnamo 0505.

Uchaguzi au GE13 kama unavyojulikana sasa, ninahisi, itakuwa ni hatua ya kisiasa kwa ajili ya udhihirisho wa umoja wa wa-Malaysia duniani kote. Sidhani niko peke yangu katika matumaini kwa Ubah wakati huu ninapoishi katika nchi ya kigeni. Unaweza kushangaa kwa nini suala hili ni muhimu kwa mtu ambaye hana uzoefu wa maisha ya kila siku chini ya utawala ambao Wa- Malaysia wengi  kwa tajiriba yao wanauona kuwa umejaa ufisadi na wenye udikteta. Siishi huko sasa lakini mimi niliishi maisha hayo yakiwa ni sehemu ya maisha ya kila siku kwa miaka mingi.

Katika jijini Melbourne, jarida la JOM, linalohudumia jumuiya ya Malaysia, ilitengeneza video juu ya siku ya kupiga kura kwa njia ya posta, uliofanyika wiki moja kabla ya Mei 5.

Pia kuna video ya wapiga kura Malaysia katika jiji la London:

Pamoja na vyombo vya habari vya kijamii kutumika sana, siyo jambo la kushangaza kwamba uchaguzi huu umekuwa ukijulikana kama   Uchaguzi wa vyombo vya habari vya kijamii

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.