Ijue Mauritania kwa Jicho la Msanii wa Kireno

Msanii wa Kireno Isabel Fiadeiro (@Isabelfiadeiro) anayeishi katika mji wa Nouakchott, Mauritania, ambako anachora na kuendesha maonyesho ya kazi ya sanaa. Fiadeiro vilevile huchora madhari kwa kuyatazama, hujaza blogu yake ya Michoro nchini Mauritania  na picha za maisha ya kila siku katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Global Voices ilizungumza na Fiadeiro kuhusu kazi yake ya sanaa na namna michoro yake ilivyomsaidia kuifahamu Mauritania.

Global Voices (GV): Umetokea wapi kiasili? Umeishi Mauritania tangu lini na kitu gani kilikupeleka huko kwa mara ya kwanza?

Isabel Fiadeiro (IF): Baba yangu ni Mreno na mama yangu ni Mhispania. Nimekulia Ureno na ninajisikia Mreno. Vile vile nimeishi Uingereza kwa takribani miaka kumi na mitano (nikiondoka na kurudi). Kwa kweli niliondoka London mwezi Machi 2003 kwa lengo la kwenda na kutulia Ureno; Nilikuwa nimemaliza Shahada yangu ya Sanaa (BA) katika Uchoraji katika Shule ya Sanaa ya Wimbledon mwaka 2000,, na nikaacha kuchora kwa miaka mitatu iliyofuata, kwa hiyo nikaamua ulikuwa ni wakati wa kuondoka.

Mwezi Novemba 2003, mimi na rafiki yangu wa Kireno tuliamua kusafiri kwenda kutembelea Guinea-Bissau kwa kutumia gari aina ya Renault 4L. Gari likaharibika tukiwa Parc National du Banc d'Arguin eneo la pwani ya Mauritania. Rafiki yangu alikaa Nouakchott na mimi nikaondoka na kundi la wa-Faransa kwenda kubaziri Eneo la Adrar.

Tulienda kwa kutumia njia zisizo rasmi na kupitia jangwani huku tukilazimika kusimama mara kwa mara katika vijiji vidogo kununua mikate na kutengeneza matairi ya gari. Nilikuwa na daftari la kuchorea na kwa mara ya kwanza nilianza kuchora kwa kutazama mazingira. Ilikuwa ni uchunguzi huu wa kufahamu zaidi kuhusu watu walioishi katikati ya maeneo haya matupu ndio ulionifanya nirudi mwezi Januari 2004, na Septemba 2004 nilihamia Nouakchott na bado ninaishi hapa.

Diallo and Mamadou, tailors in Nouakchott. Sketch by Isabel Fiadeiro.

Diallo na Mamadou, washonaji wa Nouakchott. Mchoro na Isabel Fiadeiro.

GV: Ni namna gani michoro inakusaidia kuelewa eneo?

IF: Kuchora na uchunguzi unaozaliwa na michoro unakufanya uuone ulimwengu katika namna tofauti. Unapunguza kasi, unatazama na kugundua mambo. Kwangu, kitendo hiki cvha kuchora ni aina fulani ya kumbukumbu na kujiuliza maswali.

Watu wanaokuzunguka wanakuja na kuona kile unachofanya kwa hiyo inakuwa kwa namna mbili. Unarekodi kile kilichokuvuta hisia zako, lakini kwa hatua hiyo mawasiliano yanawezekana, hata kama hauzungumzi lugha ya wenyeji.

Polisi katika maonyesho, Nouakchott. Mchoro na Isabel Fiadeiro.

Polisi katika maonyesho, Nouakchott. Mchoro na Isabel Fiadeiro.

Kwa miaka mingi ningeenda katika vijiji vya ndani kabisa kwa muda wa mwezi mzima na kukaa na familia ya wenyeji, nikichora maisha yao ya kila siku. Nilifanya hivyo katika vijiji viwili vinavyokaliwa na wavuvi katika eneo la Banc d'Arguin lakini pia Oualata, Goungel na Ouadane. Kukaa kwangu kurefu zaidi ni pale nilipokwenda Tindouf eneo la makambi ya wakimbizi katika Sahara ya Magharibi nilikokwenda kuchora wanawake na wakazi katika makambi. Watu wote waligeuka kuwa marafiki na bado tungali tunaandikiana barua na kupigiana simu na hata kukutana kama ikitokea wamefika Nouakchott.

Vilevile katika kila eneo ninagundua msamiati mpya unaohusiana na bahari au nchi au mifugo au mapinduzi.

Griots at the Fondation Malouma. Sketch by Isabel Fiadeiro.

Historia ya Malouma. Mchoro na Isabel Fiadeiro.

GV: Wewe ni mwanaachama wa jamuiya ya mtandaoni ya Wachoraji wa Mjini. Unaweza kutudokeza machache kuhusu jumuiya hiyo?

IF: Wachoraji wa Mjini ni jumuiya ya watu wasiotengeneza faida yoyote, jumuiya ya kimataifa, inayojikita kukuza sanaa ya uchoraji na upakaji rangi wa mahali fulani. Mimi ni mmoja wa wawakilishi wake 100 walioalikwa kutoka duniani kote. Lengo letu ni kuwahamasisha wengine kuchora kila siku, kwa namna hii kuboresha uwezo na uchunguzi wao.

Niliwagundua mwaka 2008, na huo ulikuwa ni ugunduzi mkuu kwa sababu mpaka wakati huo nilikuwa mkiwa nikifanya kazi peke yangu, kwa hivyo kuipata jumuiya hii ghafla kulinifanya nitake kuchora zaidi na kwa ubora zaidi. Mwanzilishi wa Wachoraji wa Mjini, Gabi Campanario, hutumia michoro kama zana ya kuhabarisha; kazi yake imechapishwa katika jarida la Seattle Times. Namna hii ya kutumia michoro kulinisisimua sana.

Discussing The Great Gatsby at a reading club. Sketch by Isabel Fiadeiro.

Majdala wa The Great Gatsby kwenye kijiwe cha kusoma. Mchoro na Isabel Fiadeiro.

Nimehudhuriamaonyesho kadhaa ya Wachoraji wa Mjini.Onyesho linalofuata linafanyika Barcelona. Sasa tuna mwakilishi wetu kutoka Mauritania, Oumar Ball, aliyeanza kuchora kwa kutumia uchunguzi miaka michache iliyopita na yeye huchapisha kazi zake kwenye mtandao wa Flickr. Baadae mwaka huu ningependa kufanya mazungumzo na warsha kadhaa kuwahamasisha watu nchini Mauritania kuchora kutokana na uchunguzi. Citymag, jarida linalosambazwa bure kila mwezi mjini Nouakchott limeanza kuchapisha michoro yangu. Huenda hatua hii itawahamasisha watu zaidi kuchukua kalamu au penseli na kuanza kuchora.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.