VIDEO: Namna Watu Wawili Tofauti Walivyopinga Dhuluma na Kushinda

Mkhuseli “Khusta” Jack anatoka Afrika ya Kusini na Oscar Olivera anatoka Bolivia; wote wawili wametoka katika mabara tofauti lakini wanayo historia inayofanana: wote wawili walipambana na dhuluma na wakashinda.

Mwaka 1985, Khusta alisaidia kuukomesha ubaguzi wa rangi kwa kuandaa na mgomo wa kununua bidhaa za makaburu mjini Port Elizabeth, Afrika Kusini. Miaka kumi na mitano baadae, mwaka 2000, Olivera alihusika kwa kiasi kikubwa katika vuguvugu la upinzani lililomaliza jaribio la ubinafsishaji wa maji mjini Cochabamba, Bolivia.

Jitihada hizi mbili, zilizotokea kwa tofauti kubwa ya miaka na katika mabara tofauti, ni ushahidi wa nguvu ya maandalizi ya kimkakati na upinzani wa kiraia usiotegemea matumizi ya vurugu.

Mwaka huu, Khusta na Olivera walikutana nchini Mexico katika Shule ya Uandishi wa Weledi. Kundi la wanazuoni na maprofesa kutoka katika shule hiyo waliandaa video yenye masimulizi ya watu hawa, ambayo ilizinduliwa hivi karibuni na kituo cha televisheni kiitwacho Narco News TV.

Mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu Rumbidzai Dube, aliyesaidia kuandaa video hiyo, anaongeza taarifa zaidi kuhusu jitihada hizo mbili za watu wawili:

Akiwa kijana na mwenye nguvu, Khusta aliandaa mgomo wa kiuchumi dhidi ya biashara zinazomilikiwa na makaburu kushinikiza madai ya watu weusi ya kuheshimiwa -kuheshimiwa utu wao na serikali ya makuburu wa Afrika Kusini.

Katika milima Cochabamba, Bolivia, mwaka 2000, Oscar Olivera akishirikiana na wengine walianzisha vuguvugu maarufu la upinzani lililokuja kufahamika kama Vita ya Maji Cochabamba -Mapambano dhidi ya hatua ya Bolvia kubinafsisha maji; ikiwa ni pamoja na maji ya mvua.

Anahitimisha:

Watu hawa wawili walihamasisha, waliwakusanya watu wao kuwa na msimamo, walisimamia walichokiamini. Walihatarisha maisha yao; Mapambano yao yalikuwa ni uthubutu, ukizingatia ukweli kuwa walikuwa wanashughulika na masuala ya kufa na kupona. Lakini je walikuwa na uchaguzi gani mwingine? Je, maisha bila maji ndilo lingekuwa chaguo lao? Je, maisha bila uhuru, heshima na haki lingekuwa chaguo? Na ni kwa sababu hiyo walijitolea maisha yao, si tu muda wao na nguvu zao bali maisha yao; na wote wawili wakashinda.

Mwandishi wa Habari Arzu Geybulla pia alikutana na Khusta na Olivera. Anaandika katika blogu yake kwamba watu hawa “wanatia hamasa kama ilivyo hadithi ya mafanikio yao.”

Blogu ya ki-Mexico Hazme el Chingado Favor [es] ilitundika uchambuzi mfupi kuwahamasisha wasomaji wake kuisambaza video hiyo:

Este video no es una comedia como las otras que hemos hecho, pero creemos tanto en su mensaje que estamos motivados para compartirlo con todo el mundo y quisieramos pedir su apoyo con su difusión. El tema del video se explica por si solo.

Video hii si ucheshi kama wengine walivyodhani, bali tunaamini sana katika ujumbe wake kiasi kwamba tunahamasishwa kuisambaza duniani kote na tungependa kuomba mtuunge mkono katika kuisambaza. Maudhui ya video hii yanajieleza yenyewe.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.